Shukrani.......

ram

Platinum Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,385
Reaction score
8,648
Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, kwa kuwa rehema zake hazikomi
Ni mpya kila siku asubuhi, uaminifu wako ni mkuu
Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, kwahiyo nitamtumaini yeye.
Maombolezo 3:22-24

Wapendwa wana JF, Mungu wetu ni mwema sana, yeye hutoa kwa majira na nyakati, naye hutwaa kwa majira na nyakati atakapo yeye, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa yote anayotufanyia katika maisha yetu. Nimekuja hapa kuwashukuru ninyi nyote mlioneshwa kuguswa na misiba iliyonipata within two weeks, katika hali ya kibinadamu ni ngumu lakini kwa kuwa Mungu wetu ni mwena yatupasa tushukuru kwa yote.

Ninawashukuru sana kwa faraja miliyonipa ktk kipindi chote cha msiba, faraja zenu zilinitia moyo na kunipa nguvu hata nikajiona siko peke yangu katika matatizo haya, narudia kusema tena kwangu JF ni zaidi ya mtandao wa kijamii. Mungu awabariki wote mlionisaidia kwa hali na mali wakati wa matatizo haya.

Kipekee nikushukuru sana charminglady, Mungu akubariki mamii, umekuwa nami kwa kipindi chote cha matatizo haya, ahsante kwa kuleta taarifa hizi hapa Mungu akubariki sana sana, sina cha kukulipa ila Mungu atafanya kitu kwako

Ahsante wote wote na Mungu awabariki sana sana
Pamoja sanaa....!!!!
 
Last edited by a moderator:
Karibu tena Jamvini ram.. na pole sana kwa kufiwa
Singida hawajambo mama?
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ram
Pole na karibu tena rafiki.

Nimekumisi saha hapa jamvini na wozap kule.

Mungu awarehemu marehemu wote
 
Reactions: ram
Pole sana na Karibu tena. Ni jambo jema sana kushukuru.
 
Reactions: ram
Tupo pamoja ram
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ram
yatupasa kushukuru kwa kila jambo kwani yatokeayo ni kwa mapenzi yake. Pole sana ram na Mungu akutie nguvu. Karibu tena jamvini. Wimbo wa Ambasodor "yatupasa kushukuru" (sjui kama nimeuquote vizur) ukuburudishe.
 
Last edited by a moderator:
''1 Samweli 7:12 - Eben-ezeri - Hata sasa BWANA ametusaidia''

Mungu na aendelee kuwa Eben-ezer maishani mwako...!!!!:amen:
 
Reactions: ram
Ahsante sana Mapi


yatupasa kushukuru kwa kila jambo kwani yatokeayo ni kwa mapenzi yake. Pole sana ram na Mungu akutie nguvu. Karibu tena jamvini. Wimbo wa Ambasodor "yatupasa kushukuru" (sjui kama nimeuquote vizur) ukuburudishe.
 
Last edited by a moderator:
Moyo usio na shukrani hunyausha
Baraka Zote !
 
Reactions: ram
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…