Shukrani kwenu wote kwa kunifariji baada ya kufiwa na mtoto kwenye ajali ya Lucky Vincent

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,199
8,756
Habari zenu ndugu wadau.

Ni siku nyingi kidogo tokea tumekuwa pamoja hapa.
Ila nimegundua kuwa bado tuko pamoja sana kimawazo.

Nawashukuru sana wadau wote wa hapa JF kwa support na wishes njema wakati wa shida kubwa sana iliyonipata ya kupotelewa na mtoto kwenye ajali ya wanafunzi kule Karatu, 06.05.2017.

Nilipata Calls nyingi, msg nyingi za simu na jumbe nyingi sana hapa jf toka kwa kila mmoja wenu.
Pia kuna baadhi ya staff walienda material zaidi kwa kunichangia hata senti ili niweze kuhimili gharama zilizoniangukia. Wote basi, kwa ujumbe huu nawashukuru sana.

Kwa ufupi tatizo nililolipata lilikuwa zito sana na lenye machungu mno kwangu. Wengi wenu kwenye thread wamejaribu kulivaa tatizo lile kwenye miguu yao, wakakiri kuwa lilikuwa oversize.

Lakini Mungu kwa upendo wake na rehema alituwezesha kukabiliana nalo, na taratibu tunaendelea kupata nguvu na kuzowea maisha mapya ya kuishi bila mtoto wetu mpendwa.

Nimalizie kwa kuwashukuru tena, na kuwasihi kuwa tushirikiane zaidi katika majanga yanayoizipiga familia zetu. Asanteni sana wadau.
 
Habari zenu ndugu wadau.

Lakini Mungu kwa upendo wake na rehema alituwezesha kukabiliana nalo, na taratibu tunaendelea kupata nguvu na kuzowea maisha mapya ya kuishi bila mtoto wetu mpendwa .. ..

Mkuu PakaJimmy naomba nikung'ate sikio hapo nilipoweka bold.
Rekebisha kama inawezekana au kama haina noma waweza acha tu.

Ila tumia mlango wa 6th sense wa fahamu.

Maana naona kama hapa huyu namba .... ana kuhusu wewe.

NB: asante sana mkuu kwa kunielewa , ni nime edit bandiko langu,
kwa pamoja tuijenge JF.
 
Back
Top Bottom