shukrani kwa national bureau of statistics (NBS) kwa kukubali kuwapa fursa vijana wasio na ajira

Mwigamba son

Member
Jan 11, 2012
27
6
Nakushukuru mkurugenzi mkuu wa NBS kwa uamuzi wako wa busara kwa kuwaruhusu vijana waliohitimu kidato cha nne na kuendelea, kutuma maombi ya kazi ya muda kama makarani wa sensa katika zoezi la sensa kama ilivyotangazwa katika website yenu. Mimi kama kijana nliyehitimu chuo na sina kazi nimepata tumaini jipya tofauti na mara ya kwanza ambapo waziri mkuu wa tanzania alielekeza kuwa zoezi hilo lingefanywa na walimu pamoja na watumishi wengine wa umma na kuwanyima fursa vijana.
UAMUZI WAKO UNGEKUWA NA TIJA KWA VIJANA ZAIDI YA HAPO KAMA UNGEWAHUSISHA WATU WASIO NA AJIRA PEKEE NA KUWAACHA WALE AMBAO TAYARI WANA AJIRA.,
 
Hadi sasa watendaj hawatak kupokea, tuombe mungu mana deadline is aproaching!
 
Nakushukuru mkurugenzi mkuu wa NBS kwa uamuzi wako wa busara kwa kuwaruhusu vijana waliohitimu kidato cha nne na kuendelea, kutuma maombi ya kazi ya muda kama makarani wa sensa katika zoezi la sensa kama ilivyotangazwa katika website yenu. Mimi kama kijana nliyehitimu chuo na sina kazi nimepata tumaini jipya tofauti na mara ya kwanza ambapo waziri mkuu wa tanzania alielekeza kuwa zoezi hilo lingefanywa na walimu pamoja na watumishi wengine wa umma na kuwanyima fursa vijana.
UAMUZI WAKO UNGEKUWA NA TIJA KWA VIJANA ZAIDI YA HAPO KAMA UNGEWAHUSISHA WATU WASIO NA AJIRA PEKEE NA KUWAACHA WALE AMBAO TAYARI WANA AJIRA.,
kaka nimekupata embu nipe jinsi ya kuapply
 
Sasa watendaji ukienda wanakwambia hawana taarifa sijui what is this? Ukiwaambia waangalie website ya nbs hawataki
 
Ingia humu kuna kila kitu www.jamiiforums.com/nafasi-za-kazi-na-tenda/294120-fomu-kwa-wale-wambao-wanataka-ukarani-kwenye-sensa-ikiwemo-waliomaliza-chuo-lakini-hawana-ajira-3.html#post4278424
kaka nimekupata embu nipe jinsi ya kuapply
 
wao wanatakiwa kuthibitisha wale wasio na ajira kwa kugonga muhuri wa mtendaji wa kata unachotakiwa pakua fomu kwenye tovuti ya national bureau of statistics ijaze kisha ipeleke kwa mtendaji wa kata aweze kukutambua mwisho iwasilishe kwa mwenyekiti wa sensa wilaya au wa halmashauri
 
kaka nimekupata embu nipe jinsi ya kuapply

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.

1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.

Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.

2. KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:- 2
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b) Kuhesabu watu kwa kutumia dodoso refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.

Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika, AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika, AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.

3. Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania mwenye sifa zilizotajwa hapo juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini, akiambatisha nakala za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo.
Maombi hayo yatumwe kwa kujaza Fomu Maalum ya maombi ya kazi ambayo inapatikana katika Ofisi ya Mratibu wa Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na endapo fomu haikupatikana, mwombaji atume maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia kazi na namba ya simu kama anayo.
Maombi yapitishwe kwa wakuu wa kazi kwa walioajiriwa au Watendaji wa Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa na ajira, ili maombi hayo yafike wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya ………………………..
S.L.P……………………………….……

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU

Picha​
ya​
Mwombaji​

MWENYEKITI WA SENSA (W)
WILAYA/HALMASHAURI YA…………….….
………………………………………………..…..

YAH: MAOMBI YA KUFANYA KAZI YA MUDA KAMA KARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA YA MWAKA 2012
SEHEMU YA I: TAARIFA BINAFSI ZA MWOMBAJI (Ijazwe na Mwombaji Mwenyewe)
1. Jina kamili (majina matatu):................................... .......................................................................
2. (a) Kazi ya sasa ……………………………………………………(b) Namba ya Simu…………
3. (a) Kiwango cha Elimu…………………………………….. (b) Tarehe ya Kuajiriwa……………
4. Mahali (Kijiji/Mtaa*) unapofanyia kazi (Kama una ajira) ………………………………………..……………………………………………………………
5. Anuani kamili ya mahali unapofanya kazi: (Kama siyo mwajiriwa andika anuani ya mahali unapoishi ) …………………………………………………………………………………………….………………………………………………………………………………………………………
6. (a) Mwaka wa kuzaliwa: .....................………………….(b) Wilaya uliyozaliwa……………
7. Jina, Anuani Kamili na Simu ya Mdhamini wako………………………………………………….
………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………

8. OMBI:
Ninaomba kufanya kazi ya muda kama KARANI /KARANI MWANDAMIZI* wa Sensa ya Watu na Makazi, 2012 na ninaahidi kuwa nitatimiza masharti na maelekezo yote yatakayotolewa na Serikali ili kufanikisha kazi hii. Sahihi ya Mwombaji……………………………………………. Tarehe………………
SEHEMU YA IIA:UTHIBITISHO KWA WALIO NA AJIRA(Ijazwe na Mkuu wa Sehemu ya Kazi)
9. Ninathibitisha kuwa mtajwa hapo juu ambaye cheo chake ni …………………………………… anafanya kazi katika kituo cha ……………………………………………………….... na ni mkazi wa Kijiji/Mtaa* ……………….…………………….. Kata ya ……..……………………………………………………… 10. Ninathibitisha kuwa taarifa zilizojazwa ni sahihi. Mwombaji huyu afikiriwe/asifikiriwe* kuwa Karani wa Sensa (kama asifikiriwe, taja sababu) …………………………………………………………………..…
………………………………………………………………………………………………………….
Jina la Mkuu wa Sehemu ya Kazi ……………………………….…… Cheo……………………………
Sahihi na Muhuri ………………………………………………………………………………………....
SEHEMU YA IIB:UTHIBITISHO KWA WASIO NA AJIRA(Ijazwe na Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa)
11. Ninathibitisha kuwa mtajwa hapo juu ni mkazi wa Kijiji/Mtaa* ……………….……………………… Kata ya …………....…………………………………………………………….… 12. Ninathibitisha kuwa taarifa zilizojazwa ni sahihi. Mwombaji huyu afikiriwe/asifikiriwe* kuwa Karani wa Sensa (kama asifikiriwe, taja sababu) ……………………………………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………..…….
Jina la Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa* ………...……………………… …………..……………….…………
Sahihi na Muhuri ………………………………..… Tarehe…………………………..……………

[SUP]*[/SUP] Futa lisilohusika
 
Ndugu,tangazo kutoka kwenye website ya NBS limekua tofauti na ambalo nimelikuta katika ofisi za Municipal ya Dodoma,bahati mbaya sikupata kopy yake lakini linataka waombaji wawe na vyeti vya ualimu angalau daraja la pili na wawe wanafundisha shule zilizopo ndani ya Municipal ya Dodoma mjini.
Nimelisoma had nikaishiwa nguvu na kwa condition hiyo si dhan vijana ambao sio walimu kuwa watapata fursa hiyo kwa hapo Dodoma.
Ningepata copy ya tangazo lile ningewawekea hapa jamvin mjionee wenyewe,au kama kuna mdau humu ndani yupo Dodoma Mjini anaweza kushuhudia kwenye mbao za matangazo za Municipal ya dodoma.
 
Naomba kuuliza etiii makarani wanachanguli wilayani au kwenye ofsi za ser/za mitaaaa?
 
Ndugu,tangazo kutoka kwenye website ya NBS limekua tofauti na ambalo nimelikuta katika ofisi za Municipal ya Dodoma,bahati mbaya sikupata kopy yake lakini linataka waombaji wawe na vyeti vya ualimu angalau daraja la pili na wawe wanafundisha shule zilizopo ndani ya Municipal ya Dodoma mjini.
Nimelisoma had nikaishiwa nguvu na kwa condition hiyo si dhan vijana ambao sio walimu kuwa watapata fursa hiyo kwa hapo Dodoma.
Ningepata copy ya tangazo lile ningewawekea hapa jamvin mjionee wenyewe,au kama kuna mdau humu ndani yupo Dodoma Mjini anaweza kushuhudia kwenye mbao za matangazo za Municipal ya dodoma.

wewe umechukua lile la kwanza kabisa ambalo lililenga walimu, nenda ofis za watendaji sasa ivi wamepatiwa form.
 
Anayetakiwa kukuthibitisha kama huna ajira ni afisa mtendaj wa serikal ya mtaa siyo kata
wao wanatakiwa kuthibitisha wale wasio na ajira kwa kugonga muhuri wa mtendaji wa kata unachotakiwa pakua fomu kwenye tovuti ya national bureau of statistics ijaze kisha ipeleke kwa mtendaji wa kata aweze kukutambua mwisho iwasilishe kwa mwenyekiti wa sensa wilaya au wa halmashauri
 
hilo ni jambo mahsusi hususan kwa vijana wa f6 ,f4 na chuo wasonakazi, nashauri f6 na chuokikuu wa2mike so wazembe wngn
 
NBS asante sana Nina hakika ASILIMIA MIA baada ya kujaza fomu nitapata hiyo kazi ya Ukarani ya Muda wa sensa. Kumbe huwa mnasoma hata maoni yetu huku JF. Mimi niliposti kuomba serikali itufikirie sisi vijana wa fomu six na university tusio na kazi na tunaweza kulitumikia taifa angalau mtupe hiyo nafasi mkakubali. Naomba pia hata za kuchambua hizo data za sensa na kuingiza kwenye Komputer mlete tena kwa watendaji wetu ili tuombe. Asante DG wa NBS.
 
Back
Top Bottom