Shukrani haiombwi wala haidaiwi, subiri ukumbukwe

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
53,742
2,000
Kidawa alizaliwa wazazi wake wote wawili wakiwa vijana, walikua wapenzi tangu wakiwa shuleni. Baada ya uzazi wa Kidawa walihangaika sana kupata mtoto wa pili. Mama kidawa alifanya maombi mengi kwa Mungu, alibarikiwa kumpata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Alex. Wakati huu Kidawa akiwa kigori wa miaka 13. Bahati mbaya uzazi wa Alex uliondoa uhai wa mama yake.

Kidawa na baba yake walishirikiana kumlea mtoto Alex. Baba Kidawa alipata ajali na kufariki aliwaacha Kidawa akiwa na miaka 15 na Alex miaka miwili. Kidawa alimlea Alex kwa msaada wa ndugu na wasamaria wema.

Kidawa alifika darasa la 12, hakupata alama za kutosha kuendelea na shule. Alipata kibarua cha kuuza duka na kuendelea kumlea mdogo wake. Alex alikua na akili nyingi. Alifaulu na kuendelea na kidato cha tano. Mpaka chuo kikuu alisoma Civil Engineering.

Baada ya kumaliza shule Alex alipata kazi nzuri kwenye shirika la Wazungu wachimbaji madini. Kidawa alimtembelea Alex na kukuta nyumba anayoishi, ina swimming pool, garden, na vyumba vitatu vya kulala.

Kidawa aliona maisha ameuapatia. Na kazi ya kuuza duka aliacha na kuamua kula mema ya nchi nyumbani kwa Alex. Alitaka mfanya kazi amfulie, ampikie na kumuoshea vyombo. Akidai isingekua yeye Alex asingefika hapo alipo.

Alex alipofunga ndoa, Kidawa ilibidi aishi na wifi yake. Alimhesabia mtoto wa watu mpaka vikombe vya chai anavyokunywa asubuhi. Mke wa Alex alipenda kumpikia mume wake, hakutaka mfanyakazi aingie jikoni. Chakula kikiiva Kidawa alipakua wa kwanza, anakula akiwa anaangalia tamthilia na akimaliza sahani anaacha hapo hapo kwenye sofa.

Tabia ya Kidawa ili imkera mno wifi yake. Alex akisafiri akirudi na zawadi Kidawa anataka kuona wifi yake amenunuliwa nini. Mwisho wa yote kutokana na tabia mbaya za Kidawa, Alex alimtoa nyumbani kwake na kumpangishia nyumba, mke wa Alex alimuomba wawe wanakutana kwenye shughuli tu hakuna haja ya kutembeleana.

Shukran haiombwi wala kulazimishwa, subiri ufikiriwe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom