Shujaa🏉 Yafanya Comeback Ya Aina Yake Mauritius

Shujaa🏉 Yafanya Comeback Ya Aina Yake Mauritius

Ikariiah

Senior Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
191
Reaction score
280
Timu ya raga ya Kenya imetwaa ubingwa wa Africa Men’s Sevens baada ya kuichapa Madagascar 15–12 katika fainali ya Mauritius Sevens.

Kilichofanya ushindi huo kuwa mtamu zaidi ni kwamba Madagascar ilikuwa imewalaza Wakenya 26–0 katika hatua ya makundi siku moja tu kabla.

Lakini Shujaa haikuishia hapo. Kenya iliibuka na ushindi wa 15–0 dhidi ya South Africa kwenye nusu fainali, kabla ya kukutana tena na Madagascar katika fainali na kulipa kisasi.

Madagascar ilianza kwa kufunga na kuongoza, lakini Rayvon Ambale akaijibu Kenya kwa try na conversion, kabla Gabriel Ayimba kuongeza try nyingine kipindi cha pili.

Madagascar ilisawazisha 12–12, lakini katika dakika za mwisho Glacious Nganya Owino akapiga penalty iliyoiweka Kenya mbele 15–12 — na Shujaa ikashikilia ushindi hadi mwisho.

Ushindi huo umeipa Kenya taji lake la saba la Afrika, ikiwa ni mara ya kwanza tangu 2023.

Kutoka kufungwa 26–0 hadi kutwaa ubingwa ndani ya siku moja - Ni nini hasa kilibadilika ndani ya Shujaa kutoka ile 26–0 hadi ushindi wa fainali?
 
Back
Top Bottom