youngkato
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 3,638
- 3,641
SHUHUDA: Alipataje $1000 Upwork?
Ni kijana wa kawaida kabisa. Hakuwahi kufanya kazi yoyote online.
Alinitafuta akaniambia: mimi sina ujuzi wowote, na sijui nianzie wapi.”
Nikamuambia: “Sawa, usijali, kila mtu huanzia sifuri. Nitakuongoza hatua kwa hatua.”
Sasa nataka nikueleze hatua zote alizopitia mpaka kufikia kupata $1000 yake ya kwanza kwenye Upwork.
Wewe pia unaweza kufanya kama yeye! 👏👇👇👇
1. Alinifuata bila kuwa na ujuzi wowote
Alikuwa hana ujuzi kabisa. Hakujua hata maana ya freelancing.
Lakini alikuwa na kitu kimoja muhimu sana: nia ya kujifunza na juhudi.
Hii ni somo: Huhitaji kuwa mtaalamu kuanza. Unahitaji kuwa na moyo wa kujifunza.
2. Alifungua akaunti ya Upwork
Baada ya kupewa maelekezo, akaenda akafungua akaunti yake ya Upwork.
👉 Akaweka picha yake nzuri
👉 Akaandika wasifu wake (profile) vizuri
👉 Akaandika mambo anayopenda na ana nia ya kufanya
Profile yako ni kama CV yako. Iandike vizuri.
3. Alijifunza kuchagua ujuzi unaohitajika sana
Nikamshauri: “Usijifunze ujuzi tu kwa sababu unapenda, bali tafuta ujuzi ambao watu wanautafuta sana.”
Tukafanyia pamoja utafiti, tukagundua kwamba animation na 3D design ni moja ya ujuzi unaotafutwa sana duniani kwa sasa.
👉 Akaamua kujifunza huo ujuzi.
4. Alijifunza kwa mwezi mmoja tu!
Kisha akaingia kwenye safari ya kujifunza.
👉 Alitumia mwezi mmoja tu
👉 Alijifunza kupitia video kwenye YouTube
👉 Alijifunza kupitia kozi ndogo ndogo za mtandaoni
👉 Alifanya mazoezi kila siku
Kujifunza hakuhitaji miaka mingi. Kama una bidii, hata mwezi mmoja unaweza kujenga msingi mzuri.
5. Alijifunza kujitangaza (personal branding)
Baada ya kujua ujuzi, nikamfundisha jinsi ya kujitangaza kwenye Upwork:
👉 Jinsi ya kuandika profile bora
👉 Jinsi ya kuandika cover letter nzuri unapokuwa unatafuta kazi
👉 Jinsi ya kujibu vizuri ujumbe wa mteja
👉 Jinsi ya kujenga mahusiano mazuri na wateja
Kujua ujuzi pekee haitoshi unahitaji pia kujua jinsi ya kujitangaza.
6. Alianza kupata kazi na kutengeneza portfolio kali
Baada ya kujitangaza vizuri:
👉 Alianza kupata kazi ndogo ndogo
👉 Alifanya kazi hizo kwa bidii sana, kuhakikisha wateja wanaridhika
👉 Alitunza kazi bora alizofanya na kuziweka kwenye portfolio yake ili kuwaonyesha wateja wengine
Portfolio bora inasaidia sana kupata kazi nyingi zaidi.
7. Akazidi kupata wateja na kufikisha $1000 yake ya kwanza
Baada ya muda mfupi:
👉 Alianza kupata wateja wa mara kwa mara
👉 Alifanya kazi kwa ubora wa juu
👉 Alifika kiwango cha kupata dola 1000 ya kwanza kwenye Upwork!
Na hii hapa ndio email aliyotumiwa na Upwork:
“You’re a real pro! You’ve passed the $1000 earnings milestone.” 🎉
8. Somo kubwa kwako wewe unayesoma hii thread
Kama huyu kijana ameweza kuanzia sifuri hadi kufikia $1000 — na bado anaendelea kupanda zaidi — basi wewe pia unaweza!
👉 Usiseme huna ujuzi — unaweza kujifunza
👉 Usiseme ni ngumu — ukiwa na nia, utaweza
👉 Usianze bila mwongozo — tafuta mtu wa kukusaidia
9. Ningependa pia nikusaidie
Kama ungetaka pia kujifunza hatua kwa hatua jinsi ya kufanya kama huyu mwanafunzi wangu:
👉 Jinsi ya kujiunga na Upwork
👉 Jinsi ya kuchagua ujuzi mzuri
👉 Jinsi ya kujifunza ujuzi huo
👉 Jinsi ya kujitangaza vizuri
👉 Jinsi ya kupata kazi ya kwanza na kuendelea
Nitumie ujumbe kwenye WhatsApp
👉 wa.me/+255693880325
Nitakusaidia na nitakupa mwongozo.
Kama wewe uko bize, una kazi, umeridhika na maisha, unaweza kushare kwa wengine ili nao wajifunze.
Kila mtu ana nafasi ya kufanikiwa online hata wewe.
#Freelancing #Upwork #KaziMtandaoni #OnlineBusiness #KupataKaziMtandaoni