Elections 2010 Shughuli zimeanza rasmi, Mungu inusuru nchi yetu

Ujengelele

JF-Expert Member
Jan 14, 2008
1,253
22
Mabomu yawatawanya wafuasi CCM, Chadema
Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 11th October 2010

KIKOSI cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU) cha Arusha, kimelazimika kufyatua risasi hewani na kupiga mabomu ya machozi, kuwatawanya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliokuwa wakigombea kusimika bendera za vyama vyao katika eneo la soko kuu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, mkoani Arusha, Akili Mpwapwa, alithibitisha hilo na kueleza kuwa tukio hilo lilianza saa 8.00 mchana.

Alisema, inadaiwa kuwa eneo hilo lilikuwa na bendera ya CCM lakini wafuasi wa Chadema walifika na kutaka kusimika bendera ya chama chao hivyo kuamsha malumbano.

Mpwapwa alisema, baada ya malumbano hayo kudumu na kuleta vurugu, polisi walipata taarifa na kwenda katika eneo hilo na kukuta vurugu kubwa na kulazimika kuwatawanya wafuasi hao kwa kupiga mabomu ya machozi.

Alidai katika vurugu hizo, polisi waliwakamata wafuasi watatu, ambao hawajui ni wa chama kipi, ambao ni Hemed Mchomba (40), mkazi wa Sombetini, Samson Ledamini (30) mkazi wa Olgirai na mwenzao Abilah Azizi (30) mkazi wa Kwa Mromboo.

Amewataka wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa kushabikia vyama vyao bila kufanya vurugu kama hizo ambazo alisema zilizohusisha kuchaniana bendera na picha za wagombea.

Alisema kuwa polisi wataendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani na atakayepatikana na hatia atachukuliwa hatua za kisheria.
 
Back
Top Bottom