Show ya Mtoko wa pasaka ya WASAFI MEDIA Roze Muhando simsikii kwenye promo

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,200
Wakati ambapo mashabiki wa muziki wa injili tukisubiri kwa hamu kubwa show kamambe ya muziki wa injili inayoandaliwa na kituo cha habari cha WASAFI inayokwenda kwa jina MTOKO WA PASAKA, kumekuwa na wasiwasi kubwa miongoni mwa mashabiki kutokana na kutoendelea kusikika tena kwenye matangazo kwa mmoja wa wahusika wakuu wa show hiyo Rose Muhando.

Show hiyo itakayofanyika siku ya Pasaka inayotangazwa kuongozwa na waimbaji vinara Christina Shusho pamoja na Rose Muhando na kujumuisha waimbaji mbalimbali imeendelea na matangazo ya kuipromoti huku ikitumika sauti ya Christina peke yake bila Rose hali inayotia wasiwasi kwa mashabiki wa mwimbaji huyo kwa atakuwepo au la!
Maana hata nyimbo za kupromoti show zinatumika zaidi za Christina na si za Rose!

Bado hakuna ufafanuzi wowote kutoka kituo hicho cha habari kwamba ni kwa nini sauti za mwimbaji nguli huyo na muhusika mkuu wa onyesho hilo kutotumika kwenye matangazo!!

images
 
NI LEO TU ASUBUH NIMESIKIA WIMBO WA UMEHARIBU AJENDA WA ROSE BAADAE UKAFUATIA WA SHUSHO... HATA JANA USIKU PIA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom