mhh patamu hapo, ila mimi nastill maintain
Kuna siku mume wa demu wangu wa zamani aliwahi kuniita tukutane mahali ana jambo la kujadili nami. Bahati nzuri tunafahamiana kiasi kwani wakati anamchumbia huyo demu bado nilikuwa nae, tulikuwa chuoni na mambo yangu yalikuwa hayajawa na msimamo, kwa hiyo demu aliponieleza kuna mtu kaonesha interest nimpe msimamo wangu, tukakubaliana aendelee nae. Hata hivyo hakuwa amemwambia tuna uhusiano, kwa hiyo jamaa akawa ananiita "shemeji". Tukakubaliana na yule msichana kuwa tuwe kaka na dada, na tumeendelea hivyo hadi leo. Basi hiyo siku jamaa alivyoniita (ilishapita miaka 4 na walikuwa na mtoto), kwa kuwa hatukuwa tumepanga lolote, "chale" likanicheza nikampigia "dada" simu, akanijibu hana habari kuwa mwenzie ana kikao nami, nikajua kuna mtego. Nimefika pa kukutania nikamkuta yuko peke yake, keshaagiza nyama choma na bia, tukaendelea. Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi?
Kama ni wewe ungemjibu nini "shemejio" huyo?
Pamoja na hayo yote lakini mi naona inategemeana na mazingira mliyoachania au kutengana.