Should we not to...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Should we not to...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Oct 16, 2009.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ndoa/Mahusiano ya wakati huu kusema kweli yamekuwa magumu kuliko yale ya enzi za wazee wetu (at least ndivyo ninavyoamini mimi). Hali hii imenifanya niwe nawaza kwa mtindo wa what if angekuwa vile na si hivi. Nikajikuta nashawishika kuamini pengine ingekuwa tofauti ingawa sina uhakika.

  Kwa kuwa nimeshuhudia miparanganyiko kwa couple ambazo either mmoja au wote wa wenzi hao ni kama ni:

  mwanamke:
  Ni mrembo wa sura, msomi, anakazi na kipato kizuri au ametoka katika familia bora kifupi ni mtu ambaye ni BORA.

  Mwanaume:
  Ni mzuri wa sura aka handsome/ana kazi nzuri na kipato kizuri/famous anajulikana na yeye mambo safi

  couple nyingi zenye combinations za namna hii au mmoja anayo sifa ya aina hii ( kwa experience yangu) huwa zinatend kuwa na migogoro ya mara kwa mara hadi nafikia kuamini kuwa ni bora tunapochagua wenzi tukajaribu kuavoid extremes i.e. msichaguane wazuri sana, wasomi sana, mwenye kipato sana au anayejulikana sana (after all hii itasaidia kupunguza gap kati ya haves and have-nots no?)

  au najidanganya?

  Naomba mnisaidie:eek:
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unajua vijawa wa siku hizi tunaangalia wasifu wa nje sana kuliko wandani amesoma sana, maisha mazuri, lakini kuna yale mambo ya ndani huwa hatuyaoni wala hatuna muda wa kuyaangalia, upendo, ukaribu, upole kiasi yani matunda ya upendo thats why ndoa nyingi za siku hizi zina matatizo.

  Ndoa za zamani zilidumu kwa sababu wazazi ndo walikuwa wanakuchagulia mke au mume, na wanaangalia uoe au uolewe na ukoo gani, na kama familia zinaendana kwa kipato na hali ya maisha ndo mana ndoa zao zilidumu walivumiliana.

  wala hujidanganyi dada ukichagua wakati huu zingatia hivyo vigezo hapo juu, lakini pia wakati mwingine ni tabia ya mtu mwenyewe. mwombe Mungu katika hilo
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  mmh..MJ1 nahisi unajidanganya lol

  not least kama ukichukuliwa kuwa mapenzi hayabagui, hayana ukabila, sura, wala kipato,,

  lakini kwa upande mwingine,, kama mmoja yuko juu zaidi ya mwingine kuna hatari ya kujisikia na kuanza kuwa na kiburi ambayo ndo mama wa matatizo mengi ndani ya ndoa,,
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa kaka yangu usemayo lakini ukiangalia nyakati za sasa hakuna kitu cha mapenzi ya kweli hayo uyasemayo (at leasi wengi hata kuyajua hatuyajui) wengi tunaoa/olewa kutimiza taratibu za jamii ituzungukayo au kufuata mkumbo. Sasa panapokuwa na mapenzi yaliosimamia katika misingi ya aina hii ya "mradi nami nimeondoa nuksi" ukioa/olewa na mtu aliyeko kwenye extremes si kujitafutia presha tu?

  Au niseme kuwa ninavyoona mimi kwa wasomi, wenye nazo, wenye sura na wale wanaofahamika sana hakuna mapenzi ya kweli ukilinganisha na wasio na visifa hivyo au?
   
 5. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #5
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe kabisa but unafikiri hali ni sawa kwa wote? kuwa hata wale ambao ni wa kawaida, kipato cha kawaida au masikini, sura za kawaida n.k. ndoa zao zina migogoro kama za hawa?
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  MJ1, ukiona hivyo ujue hapo hakuna ndoa in the first place, na matokeo yake ni kitu kilichotarajiwa...talaka na manyanyaso mengine hayataepukika na wala hatutashangaa kwa hayo yakitokea....
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  We are getting married by CHANCE and not by CHOICE
   
 8. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yeah ndo maana mm msimamo wangu wa kuoa mwanamke mwenye sura mbaya na kavu kama anapuliza moto wenye Moshi mkali upo pale pale ukioa mrembo Mapapa au Mapedeshee wanaanza kukugongea aku hivi hivi ya nn ufe kwa kiholo MJ1,Nyamayao?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndoa ni zaidi ya hayo uliyoweka ila kuna ukweli kwamba bibi au bwana mwenye sura nzuri mara nyingi huwa vivutio vya mazingira hatarishi kwenye ndoa
   
 10. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #10
  Oct 16, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  .........Ok but I hope hutakuwa unamfungia ndani ukitoka kwenda viwanja. Muambatane na wala si kumtanguliza/au kutangulia mbele
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Oct 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...sifa zote hizo hazikamilishi ubora wake bila TABIA NZURI ikiwemo; mpole/mchangamfu, mwenye imani/huruma, mcha mungu, mcheshi/mkimya, hodari, muaminifu, msikivu/mnyenyekevu, ...mwenye busara/hekima...

  Mwj'1 kuna ulazima kuwa na checklist wakati mna date, kila siku una tick boxes kama ni unsatisfactory, fair, au excellent... siku ya siku unamfanyia 'performance appraisal' kabla ya kumwambia 'I do!'
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Oct 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...aisee mbona unataka kuharibu sura za watoto bana? mbaya zaidi wageni wakija nyumbani watamkonfyuzi mama watoto na 'hausigeli'...
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Oct 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Duuh na watoto wa siku hizi wanavyojua kuzuka wakigundua una fedha ama handsome basi kazi ipo.Hata kama huna kipato utalelewa tu
   
 14. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #14
  Oct 16, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wengine tunapuliza moto na kamrija/bomba, huwa tunakuwa wazuri zaidi.
   
 15. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,744
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni sawa sawa na wito. Wengi wanaingia kwenye ndoa bila kufahamu nini maana ya ndoa.Ndoa si mtazamo wa nje kuna mengi sana katika ndoa kwa hivi kabla hujafikia uamuzi wa kufunga ndoa ni vyema ukatafakari kwa makini kwamba je huyu ni mtu ambaye nitakuwa naye miaka 20 ijayo kwa mazuri na mapungufu yake aliyonayo na yatakayojitokeza siku za mbeleni.Watu wengi siku hizi wanadanganyika na elimu,kipato na mtazamo wa mtu(uzuri wa sura na umbo) lakini wengi wameishia njia panda. kwa wale wanaotegemea kutafutiwa waume au wake hiyo ni misalaba mnabeba..mwenza tafuta mwenyewe sio kutafutiwa "Don get married by chance but by your choice"
   
 16. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #16
  Oct 16, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Haya mambo ya ndoa ukifikiri sana yanachanganya, muhimu pata mtu mliopendana na kufanana kitabia kazi kwishaa.
   
 17. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  I think you are right dear Pretty, mengineyo ni matokeo tu.
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,110
  Likes Received: 24,158
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo inapokuwa ngumu. Unaweza kutafuta mpaka umri unapita. By the way Nimeipenda hiyo Pretty is senorita kwenye avatar yako. Ni 75%uhakika wa jinsia yako. Hahahaha!
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  MJ one umesikia habari ya ndoa iliyofungwa Arusha some six weeks ago? Ilikuwa ni harusi kubwa kweli kweli,mme mhaya mke mchaga na imevunjika exactly after 4 days,kwa kifupi imevunjika wanandoa wakiwa bado kwenye fungate na bi harusi akayeya zake na kurudi majuu akimwacha mume solemba. Hiyo couple wote ni 'nshomile mpaka no class',both families wana mihela kede kede,u beauty na u handsome wa hao jamaa no comment,lakini ndo hivyo hardly a week ndoa ikasambaratika jumla. You could be right MJ1 in your analysis make na hawa jamaa wana fit hiyo bill.
   
 20. B

  Baba Mkubwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 770
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mke/mume ni tabia, wakati huohuo uwe tayari kuoa/kuolewa na huyo ulie nae. Tatizo ni kwamba.....Before marriages all our emotions zinakuwa zimekufa. Sasa itafika point ambayo emotions zitaanza kufufuka, hapo ndipo kazi marumbano yanaanza. Emotions hufufuka kutegemeana na wanandoa walivyozizika hizo emosions. Uzikaji hutofautiana, maana kuna wengine huzizika moja kwa moja na haziji fufuka, ila kunawengine huzizika (sijui miguu huwa nje) kwa mwezi, zina kuwa zimefufuka

  Nikiangalia umri wangu unakimbilia 30, nikifikilia mke wangu atakuwaje huku nikishuhudia baadhi ya matukio ya ndoa BASI huwa namwambia Mungu "Wewe ndie unaeweza, naimani utanipa mke ambae tutasaidiana katika vitu vyote ..............................."

  Nilikuwa nafikilia nikioa niweke "Marriage constitution". Na hii constitution iwe inafahamika na pande zote mbili, mimi na huyo mke wangu. Na iwe imeandaliwa kabla ya ndoa. Na tuwe tumeandaa wote wawili, tukiweka na adhabu pale mtu avunjapo....
  Wana JF ninachowaza kinawezekana au?
   
Loading...