Mzee Mwanakijiji,
Mkuu wangu unayafanya haya kwa nia nzuri sana lakini sidhani kama utaratibu wa Asylum unakwenda hivyo, pamoja na kwamba barua yako ni nzito kichizi.....
Kwanza si wanatakiwa watoke nje, na wafike huko waendako wachukue hiyo asylum au unataka kunambia serikali ya Tanzania italazimishwa kuwapa visa na ticket hao Albino waondoke nchini baada ya kuwa granted asylum wakiwa ndani!.. Sijawahi kusikia wala kuona utaratibu kama huu!
si lazima kuwa hivyo. Endapo serikali ya mojawapo ikatambua kuwa kundi fulani ndani ya nchi fulani liko katika hali ya wasiwasi basi wanaweza kuwapa nafasi hiyo. HIlo limetokea kwa Wasomalia na Wasudan ambao ndani ya nchi zaoo walikuwa wanaangamizwa.
Kinachotakiwa ni hilo kundi kuwa designated kama ni "threatened group" au kitu kama hicho. Marekani ilihamisha mamia ya Wasudan na Wasomalia kutoka nchini mwao (kupitia Kenya) baada ya kuwatambua, kuwapa taarifa zote sahihi.
Hata hivyo, mimi nadhani msaada mkubwa utapatikana ndani nchini yaani sisi wenyewe na vyombo hivyo vya kimataifa NGOs wanaweza kuwasaidia hawa jamaa zetu na suluhu ya maswala ya Albino yapo ndani chumbani mwetu..
Hilo ni kweli, lakini katika historia ya maisha ya wanadamu mahali popote ambapo maisha hayo yanatishiwa basi watu na jamii inayohaki ya kuwalinda watu hao. Hii ndiyo sababu kuna watu ambao kuanzia wakati wa mapinduzi ya Bolshevik, vita ya pili ya dunia, n.k Nchi mbalimbali zilitengeneza utaratibu wa kutambua na kuwapokea watu ambao maisha yao yanakuwa hatarini.
Zaidi ya hivyo naamini sisi hatuna uwezo wa kuzuia mauaji ya albino kwa kadiri ya kwamba serikali iliyopo ndiyo inatakiwa kusimamia sheria hizo. Inapofikia serikali ya fedha nyingi, vyombo vingi vya ulinzi inafikia mahali kuagiza UVCCM na Sungusungu kufanya kazi za kipolisi na kiusalama kana kwamba vyombo hivyo vimeapishwa kufanya mambo hayo ina maana moja tu. Tumeshindwa.
Hawa sii kizazi kinachokwisha kesho kiasi kwamba tufikirie kuwatenga na sisi wananchi kukubali kuwa Tanzania sii mahala pao isipokuwa huko nje.
Hii siyo tafsiri sahihi. Tunachofanya ni kusema kuwa "sisi tumeshindwa kuwalinda, na hivyo tunaomba wengine watusaidie kufanya hivyo". Kukiri upungufu huo siyo kukosa uzalendo au kutokuwa mtaifa bali ni kupima kipi kilicho juu kati ya kutaka waendelee kukaa Tanzania wakati mchana na usiku wanawindwa kama paa au kuwapatatia nafasi na mahali ambapo ujinga wa imani za kishirikina hauna nguvu hiyo? Ni uzalendo kuwalinda maalbino na vikongwe mahali popote pale.
Hawa ni raia, solution ni LAZIMA itoke ndani ikiwa sisi sote tunaamini kuwa serikali imeshindwa kuwalinda..
Na nikirudi ktk usemi huu wa serikali kushindwa kuwalinda, inaonyesha pia sisi wananchi tumeshindwa kuwalinda hivyo unapopingana na usemi wa waziri mkuu ni bora uje na suggestion ya kitu gani wananchi wanatakiwa kukifanya tofauti na waziri mkuu..
Nimeshatoa suggestion yangu kuhusu hilo. Kuna thread nimeanzisha mbili na moja wameanza kufanyia kazi lakini kiuvivu. Hawana dhamira ya wazi na ya makusudi ya kukomesha mauaji haya zaidi ya amri za kukurupuka na maagizo ya kihalifu.
Laa sivyo itaonyesha sisi sote tumejiunga kuwabagua hivyo wanapochukua asylum nje tutajumuishwa sote na serikali yetu kuwa tumewatenga...
Huo ndio ushauri wangu!..
Hapana atakayefikiri tumewatenga sidhani kama tunaweza kumzuia. Kama serikali imeshindwa imeshindwa. Kwa mtu albino haitaji kuambiwa kuwa anatengwa au la, anahitaji kujua kuwa yuko salama. Tukiendelea kuacha mambo yaendelee hivi hivi tukiamini kuwa ati kuna wana usalama wenye uwezo wa kuzuia mauaji haya tunajidanganya.
Tunachofanya ni kuishika ile tunu iliyotuunda sisi kama taifa kuwa "binadamu wote ni sawa" na ya kuwa "kila mtu ana haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake". Katika hayo yote hatujasema "kila raia" ni sawa au "kila raia ana haki..."
Tumesema binadamu na mtu. Kwa maneno mengi haki zetu kama binadamu ni za juu zaidi kuliko haki zetu kama raia. Unaweza ukapunguza au kuzuia baadhi ya haki za raia, lakini kuzia haki za binadamu ni karibu haiwezekani. Na haki ya kwanza ya msingi na kubwa kabisa ambayo ni haki ya binadamu ni haki ya kuwa hai.
Jamii inaposhindwa kuilinda haki hiyo au kuhakikisha uwepo wake basi jamii hiyo haiwezi kuwa kikwazo kwa yule ambaye uhai wake unatiishiwa kuamua kutafuta njia nyingine ya kulinda maisha yake.
Naamini kuwafungulia mlango katika nchi za magharibi ni jaribio la kufanya hivyo.