Ramsy Dalai Lama

Senior Member
Apr 5, 2021
147
540
Nakumbuka nikiwa mdogo jinsi nilivyotamani kuishi kwenye nyumba ya kifahari kama ambazo walikua wakiishi rafiki zangu ambao walikua watoto wa matajiri na wengi walikua waarabu..Baba zao walikua wenye company za ASAS, F.M Abri, Estate Co, OilCom, Temeke Bakery na wengineo ikiwemo na baadhi ya ndugu zangu waliokua wanauwezo...at the time sisi tulikuwa middle class but baadae mzee alipiga mshindo, alipiga hela nyingi sana bcoz alikua boss wakitengo fulani serikalini (I'm not proud of that).

Sasa alikua na rafiki yake mzungu akachukua ile hela yake aliyopiga akanunua nyumba kwa yule mzungu. ilikua nyumba mikocheni ambayo ni two (2) story Luxury house. kwa kweli was typically larger Luxury homes offer incredible master suites na kulikua na AC at each room including kitchen Yan hakukua na fan kabisa, na pia ilikua na high premium materials such as granite countertops, marble floors, and premium kitchen appliances. pia kulikua na automatic generator na nje garden kubwa with big parking lot.

Basi tukahamia kwenye ile nyumba. Kwa kweli ilikua ile dream house ambayo nilitamani kuishi siku moja japo iliku si yangu lakini at least niliishi kwenye hiyo nyumba kama ambazo walikua wakiishi marafiki zangu.

Miaka kadhaa baadaye, nilizoea kuishi humo na kuanza kuona ya kawaida sana na ile furaha ikaisha kabisa tena zaidi nilianza kuwa bored bcoz mtaa wenyewe ulikua kimya sana. halafu nyumba haikua na watu wengi na ndugu hawakua wakija kwenye ile nyumba walikua wakienda ile ya zamani na mzee alipenda kukutana nao huko. Na hata baadae nilikuja kugundua hata marafiki zangu walikua wanaona kawaida na hata mda mwingine wana stress zao kwa kutamani mambo mengine kabisa.

Lakini ukiachana na hivyo kwa upande wangu the worst scenario ule mshindo baadae ulimletea mzee matatizo kiasi kulazimishwa kustaafu kabla ya muda wake. Regardless alilipwa malupulupu yake na bado analipwa pension zake.

long story short, ngoja niwaambie kitu marafiki zangu wa JF, siku moja mambo yote unayotamani leo hayatakuwa na maana tena kesho utakapo yapata.

Baadhi yetu tunatamani msichana au mvulana mzuri ambaye pengine tunaacha wanaotupenda na kuchukua asiye na mapenzi na wewe kisa tu kutamani uzuri wake. Baada ya muda utajiona mjinga.

Ipo siku, utapata kazi ambayo ilikufanya ulale na boss na kuuza utu wako lakini ukishapata unaweza kujiona mjinga.

Siku moja utapata gari, simu ama chochote ambacho ulikitamani kikakufanya kujaribu kufanya kitu cha kipumbavu ama cha kukuhatarisha ili tu upate hicho kitu lakini ukipata baada ya muda waweza kujiona mjinga

Nini hamu yako kubwa zaidi leo? Nyumba? Gari? kwenda abroad? Pesa? mpenzi mzuri? Vyovyote itakavyokuwa unatamani leo yawezekana siku moja ukipata utaviona vya kawaida kuliko ulivyodhani.

Tafadhali tulia na nenda taratibu. Pigania ndoto zako lakini isikufanye ukose furaha leo au kufanya jambo utakalo jutia baadae ama kukuingiza kwenye matatizo. Niamini mimi hivyo unavyovipigania leo especially material things si kwamba vitakupa meaning of life hapana...your well being is what really matters to you.

Asante kwa kusoma
 
Back
Top Bottom