Shoka la TRA latua CHADEMA

Akikwepa Patel na Manji sawa lakini mzawa hata akiomba msamaha wa kodi apewi,duh! kweli CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi tena.
Lazima tudhibiti wakwepa kodi ili kukuza uchumi wetu.
 
TRA inapokuwa REACTIVE badala ya kuwa PROACTIVE. Yaani mpaka CHADEMA wasema TRA ina madudu mengi ki utendaji wao nao wanakuja na mambo ya kukomoana.

Kwangu mimi hii ni FAILURE kubwa sana kwa chombo nyeti kama TRA, yaani miaka yote hiyo hawakujua kwamba CHADEMA hawalipi kodi hadi juzi tu DR. Slaa alipotoa shutuma kwao? this country bwaaaana mifumo yoote haifanyi kazi yaani imekufa na kuzikwa.

Naanza kuamini kama wewe ni mfanyabiashara mkubwa basi uwe ndani ya CCM, vinginevyo watakuwambia hujawahi kulipa kodi miaka yote tangu uanze biashara zako na hawakawii kukufilisi. Kwa sababu hii ni issue ya kisiasa sasa tutaona nani zaidi - Ngumu ya Umma au Serikali ya Kikwete -- Pigeni filimbi mtanange uanze.
 
Kwanini huwa hamfikirii kabla ya kuandika na kutenda mlikuwa wapi msiwafuatilie miaka kumi au mnataka kuwadanganya wananchi ili kuwachafua CHADEMA. Acheni kupoteza muda kwa kusikiliza muongozo mnaopewa na wanaowala na kuwanyonya. Badala ya kuungana pamoja kujenga nchi mnaungana kubomoa Shame on you.

And let me tell mmeshachelewa kwani wananchi wameshafunguka macho na ni ngumu kuwageuza tena. Kakateni kodi na Trilioni za Shimbo basi
 

Pia ikumbykwe kama hawa ndio vinara wa vita juu ya ufisadi...amakweli nyani haoni kundule. Kuna mtu mmoja alininon'goneza kuwa hawa wanaiasa ni njaa tu zinawasumbua.

Kikwebo.
 
Hivi makelele yote akina Mbowe kuhusu ya posho za vikao vya BUNGE na kurudisha gari kuna tofauti gani kama katibu ana lipwa posho kubwa hivi na tena eti ni kwa ajili Slaa tu ila kama katibu akibadilika na posho pia inabadilika. What's specials Slaa contains? Kukwepa kodi huko ni picha halisi kwa wasiowafahamu
 
mwaga mboga nami nimwage mchuzi.

kazi ipo.
 
Kama chadema hawakulipa kodi faini ni haki yao swali lipo palepale JE CCM MMEKUWA WAAMINIFU TOKA LINI NA JE MMELIPA NA NINYI???
 
<br />
<br />

Chadema lazima waelewe kuwa Posho ni Fedha!
 
CCM wanaanzisha ugomvi wa mawe wakati wanakaa kwenye nyumba ya kioo. Wait and you will see. Wanachofanya ni sawa na kukata tawi la mti ulilolikalia.
 

Kaka hapa ndipo patamu na hizi tuhuma zikithibitika watz tikubali tutakuwa hatuna akili, yaani Budget ya nchi ni trilion 11 mtu anamiliki trilion 3 tena hazina kazi kaziweka tu Bank!? kazipata wapi? kwa kazi ipi? au ndio maana vile vitisho vya kabla ya uchaguzi nini?
 
Kama ni kweli ni vema CDM walipe lakini issue ni pale watakapoguswa kama TLP n.k.siku zote mti unaotoa matunda ndio hupondwa mawe, serikali na iwe extremely clean kwa hili vinginevyo tutarajie kuibuliwa kwa makubwa zaidi ya hayo.
 
Naamini ingekua kweli basi habarileo wangeandika,....
Nipashe wangeandika
Mwananchi wangeandika
Tanzania daima wangeandika
Dira wangeandika
Majira wangeandika.....

Lakini uhuru?????
Hata kama ni kweli i never trust anything written in uhuru news paper
 
NUKUU: Siasa ni mchezo mchafu. Hapo ni uchafu wa kuichafua chadema. Nao wawe makini na wakitaka amani wakiri au wakanushe jambo hili itasaidia kuweka mambo bayana.
 
Uhuru + jamba leo = MAGAMBAZ WORK. Hivi chama cha magamba wanalipa kodi??
 
Ukiona hivyo jua kuwa jamaa wanawachafulia ili wasishinde ubunge wa Igunga.
 
Hawa nao wamezidi kila siku Chadema CHADEMA, yaani wakikosa cha kufanya wanakurupuka tu! MASABURI hakukosea kusema kuna watu wanafikiria kwa kutumia mat@''#@
 
acha kulalama. chadema niwakwepa kodi wazuri. tena ukizingatia inaongozwa na wale ndugu zetu wanaolifilisi taifa hili tangu uhuru.
 
Ni mfano mbaya sana kutokulipa kodi huku unasema serkali haifanyi kitu, ingekuwa nchi za wenzetu wangeburuzwa mahakamani

Wnaotakiwa kulipa kodi hii inayoongelewa (PAYEE) ni wafanyakazi wala si chama au taasisi! Hapo ndo tunapopotoshana.

Anayelipa kodi ni mwajiliwa na si mwajili.Sasa mbona wanaituhumu chadema wakati wao(CHADEMA) ni waajili tu?
 
<br />
<br />

HZO RECORDS NI MASUALA YA KIUSALAMA..
 
Hivi Viongozi woote wa CCM mfano Mh. Nape wanalipa kodi? Nakumbuka ezi za chama kimoja ukiwa mfanyakzi wa CCM haukuhitaji kulipa kodi

CCM, to survive there must be a TAX loophole as they way they provide to foreign companies...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…