Shocking: Abiria akutwa na bastola kwenye ndege | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shocking: Abiria akutwa na bastola kwenye ndege

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kizimkazimkuu, Dec 9, 2011.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Ramadhan Semtawa

  KATIKA hali ambayo si ya kawaida, Zainab Kaswaka aliyekuwa anasafiri kwa ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda London, amekutwa na bastola kwenye ndege ya Shirika la Emirates na kuzua tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Viwanja vya Ndege nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei, zimeeleza kuwa tukio hilo lilisababisha ndege hiyo iliyokuwa tayari imeanza kuruka, kutua tena kwa ajili ya kuitoa bastola hiyo na kuikabidhi kwa walinzi uwanjani hapo kabla ya kuendelea na safari.

  Kwa mujibu wa habari hizo, tukio hilo ambalo limekuwa likiumiza vichwa vigogo wa usalama wa viwanja vya ndege nchini, limetokea Desemba 2 saa 11:45 na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Insepekta Jenerali (IGP) Said Mwema ametaka maelezo ya tukio hilo. Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwananchi umebaini kwamba, Kaswaka alipanda na kukutwa na bastola hiyo aina ya Bareta yenye namba BAA197059 ikiwa na risasi nne na magazini moja ambayo alilazimika kuikabidhi kwa wahudumu wa ndege hiyo. Abiria huyo alikuwa na hati ya kusafiria namba AB00828, alipita na kukaguliwa katika mashine mbili za usalama (X-ray machines), lakini walinzi hao ambao wanatajwa walichukuliwa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga Ukonga (Air wing), hawakuweza kubaini kama katika mizigo ya abiria huyo kulikuwa na pochi yenye bastola hiyo.

  Sehemu ya uchunguzi huo ilibaini zaidi kwamba, wakati abiria huyo akiwa tayari amekwishapanda ndege hiyo, ndipo mumewe alimwarifu kwa simu kuwa ndani ya mkoba wake mdogo uliokuwa katika begi kubwa, mlikuwa na bastola. Mwananchi ilibaini zaidi kwamba baada ya kuarifiwa bastola hiyo ingemsumbua mbele ya safari, abiria huyo aliangalia mfuko huo na kuikuta, kisha kuikabidhi kwa mmoja wa wahudumu wa ndege ambaye naye aliikabdihi kwa rubani. "Baada ya rubani kukabidhiwa bastola hiyo, alifanya mawasiliano na mamlaka za usalama uwanjani kisha akageuza ndege hiyo hadi uwanjani hapo, takribani dakika kumi tangu ilipoanza kuruka kuelekea nchini Dubai,"alisema.

  Hata hivyo, uchunguzi huo ulibaini kuwa badala ya abiria huyo kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo maalumu, aliruhusiwa kuendelea na safari hiyo na sasa anasubiriwa arejee nchini ndipo atoe maelezo. Kufuatia tukio hilo la abiria kupenya na bastola, tayari kumeibuka mvutano miongoni mwa mamlaka za usalama uwanjani hapo huku polisi wakianza kutuhumiwa kwa kushindwa kumpekua abiria huyo na kubaini bastola hiyo. Lakini, polisi nao wamekuwa wakirusha mpira huo kwa walinzi waliokuwa wakifanya ukaguzi kwa kutumia mashine hizo maalumu za kubaini mizigo isiyostahili kupita na abiria kuingia nayo ndani ya ndege.

  IGP awaka
  Vyanzo vilivyo karibu na IGP Mwema, vimesema tayari mkuu huyo wa jeshi la polisi lenye ametaka maelezo ya tukio hilo kutoka kwa Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo karibu na IGP, tukio hilo limemstua na kuacha maswali mengi kutokana na kwamba kama abiria huyo angekuwa ni mhalifu angeweza kuitumia bastola hiyo kufanya mauaji na hata kujeruhi watu ndani ya ndege.Hata hivyo, IGP Mwema alilishauri gazeti hili limwulize msemaji wa jeshi hilo, Adivera Senso ambaye baada ya kuulizwa, naye akataka aulizwe kamanda Matei.

  Hatua zachukuliwa
  Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei alithibitisha tukio hilo na kusema tayari hatua kadhaa zimechukuliwa kwa watu waliokuwa kwenye mashine hizo za ukaguzi. Kwa mujibu wa kamanda Matei, wanajeshi wote waliokuwapo zamu kwenye mashine hizo siku ya tukio, wamerejeshwa kambini kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu. Kamanda Matei alisema, baada ya tukio hilo na ndege kurejea tena uwanjani hapo, vyombo vya ulinzi na usalama vikiwamo polisi na usalama wa taifa, walikutana na kujadili hilo ikiwamo kuangalia picha za abiria walivyokuwa wakipita kwenye mashine hizo. Alifafanua kwamba baada ya kuangalia picha hizo, ilibainika tukio zima lilitawaliwa na uzembe kwa walinzi hao kutoka JWTZ ambao walikuwa katika mashine hizo, kwani hawakuwa makini kuona namna abiria huyo alivyokuwa akipita na bastola iliyokuwa katika pochi hiyo.

  Matei ambaye alifafanua tukio zima kwa uwazi, alisema ndege hiyo ilipaa katika njia maalumu iitwayo 'runway five' na kuongeza kwamba hadi sasa tayari kumechukuliwa hatua mbalimbali za maboresho ya udhibiti wa mfumo wa ukaguzi na usalama unaofahamika kama 'quality control.' Kwa mujibu wa Kamanda Matei, baada ya tukio hilo, pia wameamua walinzi wanaofanya ukaguzi kwenye mashine hizo, wasiwe na simu za mkononi kwani imebainika kuwa simu ni moja ya sababu zinazowafanya kukosa umakini katika kazi uwajibikaji wao. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu hatma ya abiria huyo, alisema imebainika hakuwa na kosa lolote kwani alipita tu na bastola yake pasipokufahamu wala hakuwa na nia mbaya.

  Silaha hiyo inashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege. Kamanda Matei alieleza kuwa abiria huyo ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam eneo la Jangwani Mtaa wa Swahili na alikuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea London, kwa shughuli zake binafsi.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,174
  Trophy Points: 280
  Walinzi wa kibongo wakikuangali na kukuona mama mama type fulani hata hizo X-Ray wanafanya routine tu.

  This is embarassing.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,407
  Trophy Points: 280
  walikuwa na ma ipad ma i phone 4s wapo bussy kubrowse,,,hivi wanajeshi hao walikuwa na visimu vyao wanafanya nini? Wapo JF? FB? Au wanaandikiana meseji na malaya ..
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hili suala la kucheza na simu wakati wa kazi inabidi liangaliwe sana..siku hizi si ajabu unaenda benki, ofisi za umma au hata traffic anayeongoza magari eti na yeye unamkuta yupo bize na kasimu kake ka mchina, hii ni hatari si tu kiusalama bali pia upotezaji muda, mara nyingi unakuta mteja unasubiria halafu mtoa huduma yuko bize na simu eti umsubirie..jamani mkiambiwa acheni uvivu na uzembe mnakasirika. Kama unataka uwe unapokea na kuchat kwene simu 24/7 fungua ofisi yako, kwene ofisi za umma waachieni watu walio punctual na wanaonjali wateja. Watu HR tumieni taaluma zenu kuongeza productivity, productivity ktk nchi hii ipo chini sana kiukweli thanks to uswahili kaa huu ambao ni rahisi sana kuudhibiti.
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hahaha, tz zaidi ya uijuavyo! Ukipita umepauka na mkorogo umekuunguza sura kila saa unarudishwa wapige x-ray vindala vyako! Last wk niliona kali, eti ukipita alarm ikalia mlinzi anakuambia leta hiyo pete, anaishikilia unarudi tena. Kama maigizo vile! Na abiria akasepa vile vile,si ajabu mumewe alikuja kupick kibastola chake kama anaria vile! Mweh!
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii yote inaonyesha namna Watanzania tunavyobeza kazi. Uzembe makazini upo sana, si hospitali, posta wala ulinzi.

  Tujirekebisheni kidogo aggggrrr
   
 7. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mh aibu sana,
   
 8. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ramadhan Semtawa

  KATIKA hali ambayo si ya kawaida, Zainab Kaswaka aliyekuwa anasafiri kwa ndege kutoka jijini Dar es Salaam kwenda London, amekutwa na bastola kwenye ndege ya Shirika la Emirates na kuzua tafrani kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Kamanda wa Viwanja vya Ndege nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei, zimeeleza kuwa tukio hilo lilisababisha ndege hiyo iliyokuwa tayari imeanza kuruka, kutua tena kwa ajili ya kuitoa bastola hiyo na kuikabidhi kwa walinzi uwanjani hapo kabla ya kuendelea na safari.

  Kwa mujibu wa habari hizo, tukio hilo ambalo limekuwa likiumiza vichwa vigogo wa usalama wa viwanja vya ndege nchini, limetokea Desemba 2 saa 11:45 na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Insepekta Jenerali (IGP) Said Mwema ametaka maelezo ya tukio hilo. Uchunguzi wa kina uliofanywa na Mwananchi umebaini kwamba, Kaswaka alipanda na kukutwa na bastola hiyo aina ya Bareta yenye namba BAA197059 ikiwa na risasi nne na magazini moja ambayo alilazimika kuikabidhi kwa wahudumu wa ndege hiyo. Abiria huyo alikuwa na hati ya kusafiria namba AB00828, alipita na kukaguliwa katika mashine mbili za usalama (X-ray machines), lakini walinzi hao ambao wanatajwa walichukuliwa kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga Ukonga (Air wing), hawakuweza kubaini kama katika mizigo ya abiria huyo kulikuwa na pochi yenye bastola hiyo.

  Sehemu ya uchunguzi huo ilibaini zaidi kwamba, wakati abiria huyo akiwa tayari amekwishapanda ndege hiyo, ndipo mumewe alimwarifu kwa simu kuwa ndani ya mkoba wake mdogo uliokuwa katika begi kubwa, mlikuwa na bastola. Mwananchi ilibaini zaidi kwamba baada ya kuarifiwa bastola hiyo ingemsumbua mbele ya safari, abiria huyo aliangalia mfuko huo na kuikuta, kisha kuikabidhi kwa mmoja wa wahudumu wa ndege ambaye naye aliikabdihi kwa rubani. "Baada ya rubani kukabidhiwa bastola hiyo, alifanya mawasiliano na mamlaka za usalama uwanjani kisha akageuza ndege hiyo hadi uwanjani hapo, takribani dakika kumi tangu ilipoanza kuruka kuelekea nchini Dubai,"alisema.

  Hata hivyo, uchunguzi huo ulibaini kuwa badala ya abiria huyo kuwekwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo maalumu, aliruhusiwa kuendelea na safari hiyo na sasa anasubiriwa arejee nchini ndipo atoe maelezo. Kufuatia tukio hilo la abiria kupenya na bastola, tayari kumeibuka mvutano miongoni mwa mamlaka za usalama uwanjani hapo huku polisi wakianza kutuhumiwa kwa kushindwa kumpekua abiria huyo na kubaini bastola hiyo. Lakini, polisi nao wamekuwa wakirusha mpira huo kwa walinzi waliokuwa wakifanya ukaguzi kwa kutumia mashine hizo maalumu za kubaini mizigo isiyostahili kupita na abiria kuingia nayo ndani ya ndege.

  IGP awaka
  Vyanzo vilivyo karibu na IGP Mwema, vimesema tayari mkuu huyo wa jeshi la polisi lenye ametaka maelezo ya tukio hilo kutoka kwa Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo karibu na IGP, tukio hilo limemstua na kuacha maswali mengi kutokana na kwamba kama abiria huyo angekuwa ni mhalifu angeweza kuitumia bastola hiyo kufanya mauaji na hata kujeruhi watu ndani ya ndege.Hata hivyo, IGP Mwema alilishauri gazeti hili limwulize msemaji wa jeshi hilo, Adivera Senso ambaye baada ya kuulizwa, naye akataka aulizwe kamanda Matei.

  Hatua zachukuliwa
  Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ulrich Matei alithibitisha tukio hilo na kusema tayari hatua kadhaa zimechukuliwa kwa watu waliokuwa kwenye mashine hizo za ukaguzi. Kwa mujibu wa kamanda Matei, wanajeshi wote waliokuwapo zamu kwenye mashine hizo siku ya tukio, wamerejeshwa kambini kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu. Kamanda Matei alisema, baada ya tukio hilo na ndege kurejea tena uwanjani hapo, vyombo vya ulinzi na usalama vikiwamo polisi na usalama wa taifa, walikutana na kujadili hilo ikiwamo kuangalia picha za abiria walivyokuwa wakipita kwenye mashine hizo. Alifafanua kwamba baada ya kuangalia picha hizo, ilibainika tukio zima lilitawaliwa na uzembe kwa walinzi hao kutoka JWTZ ambao walikuwa katika mashine hizo, kwani hawakuwa makini kuona namna abiria huyo alivyokuwa akipita na bastola iliyokuwa katika pochi hiyo.

  Matei ambaye alifafanua tukio zima kwa uwazi, alisema ndege hiyo ilipaa katika njia maalumu iitwayo 'runway five' na kuongeza kwamba hadi sasa tayari kumechukuliwa hatua mbalimbali za maboresho ya udhibiti wa mfumo wa ukaguzi na usalama unaofahamika kama 'quality control.' Kwa mujibu wa Kamanda Matei, baada ya tukio hilo, pia wameamua walinzi wanaofanya ukaguzi kwenye mashine hizo, wasiwe na simu za mkononi kwani imebainika kuwa simu ni moja ya sababu zinazowafanya kukosa umakini katika kazi uwajibikaji wao. Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu hatma ya abiria huyo, alisema imebainika hakuwa na kosa lolote kwani alipita tu na bastola yake pasipokufahamu wala hakuwa na nia mbaya.

  Silaha hiyo inashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Uwanja wa Ndege. Kamanda Matei alieleza kuwa abiria huyo ni mkazi wa jiji la Dar es Salaam eneo la Jangwani Mtaa wa Swahili na alikuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea London, kwa shughuli zake binafsi.
   
 9. m

  mbweta JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 600
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Usikute x-ray ilishajifia tangu zaman pale zuga 2.
   
 10. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Mweeeh,lazima pale dubai wangegundua tu,tena anakwenda Uk,na hivi ni mwislamu angeshukiwa anataka kuiteka ndege ya kwenda UK.
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Du. This is very dangerous
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wala hatutashangaa! Kama kuna wa kumulikwa ahamishiwe international airport of lindi
   
 13. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi zile 'asshine zinafanya kazi? Mi najua huwa zinaona perfume na deo spray tu, hasa ile ya mwisho ile. Hii ya kwanza haifanyi kazi. That one i can bet on it.
   
 14. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Na wewe acha unafiki kupotosha watu. Habari iko wazi halafu wewe unataka kuipindisha. Yule HAJAKUTWA na bunduki bali ALISALIMISHA mwenyewe baada ya vilaza pale airport kushindwa kubaini. Yaelekea anafanya zoezi na ameconclude kuwa it is possible kupita na silaha. Katika hali kama hiyo mzembe ni abiria au walinzi. Utashangaa wanamzonga mama wa watu badala ya kuwaminya wale walinzi vilaza
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Mbona hii habari tulishaipata hapa JF wiki moja iliyopita na tumeshaijadili! yaani gazeti ndio wanairipoti leo? kweli JF kiboko kwa style hii hakuna haja ya kununuwa magazeti ni bora kulog in JF basi, na habari zote muhimu utakuwa wa kwanza kuzipata.
   
 16. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 160
  True..!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  this is a shame really......... wanatunyanganya after shave na maji ya dasani kumbe bastola zinakatiza??\

  I cant imagine how many other things huyu mama alikua navyo ambavyo ni illegal as far airtravel is concerned
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hahaaa mtakatifu Ivuga taratibu tafadhali....unaikosea heshima ipad ya shemeji yako bana...swalama lakini?
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  huyo mama awekwe chini ya ulinzi kwa kosa lipi?
   
 20. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  .....Unafiki maana yake nini? na nimempotosha nani? Na ni wapi nimesema mimi ndio Ramadhani Semtawa (mwandishi wa mwanachi aliyeripoti hii habari). The fact ni kuwa abiria alikuwa na bastola ndani ya ndani, kama alikutwa/ alijikuta/aliisalimisha is immaterial hapa; bastola imefika ndani ya ndege na haikupaswa kutokea. POLISI mmmeshindwa kazi, na kama style yenyewe ni kukurupuka kama hivi; hatutarajii mabadiliko leoala kesho!
   
Loading...