Shitambala awania ujumbe wa NEC

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumamosi, Septemba 01, 2012 06:29 Na Pendo Fundisha, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, Kapteni Sambwee Shitambala na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amejitokeza na kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya ya Mbeya Mjini.

Shitambala alichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha ofisi za CCM wilayani humo, akiwa ni mwanachama wa 12 kati ya waliochukua fomu za nafasi hiyo kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu hiyo kwa Kaimu Katibu wa CCM wilayani humo, Julius Msaka, Shitambala alisema nia yake ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Alisema nia na dhamira ya kugombea nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi ambao kwa sasa wanahitaji mabadiliko ya kweli katika uchumi na kijamii kwa ujumla.

“Nia na dhamira yangu ni kuwatumikia wananchi na kukiwakilisha chama changu kwa nia moja ya kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi na niwahakikishie kuwa CCM bado ina nafasi kubwa ya kuongoza nchi,’’ alisema Shitambala.

Wanachama wengine wa CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Obadia Mbilinyi, Shua Mwasanguti, Aggrey Mwasanguti, Dk. Stephen Mwakajumilo, Burton Mwankunda, Frank Mahemba, Edson Kajigili, Maria Nyagawa, Fatuma Kasenge, Richard Shanghvi na Daniel Fusi.

Kwa upande wake, Msaka alisema wanachama wote wamepewa onyo la kutojinadi wala kuchumbia wapiga kura hadi siku ya uchaguzi na vikao vinavyohusika kupendekeza majina ya wagombea waliokidhi vigezo vya nafasi hiyo.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
hahahhahh namfaham huyu jaamaa ni bwana mdogo mwanasheria kigeugeu kweli, aligombea ubunge kwa tiketi ya cdm mbeya vivijini aliuza jimbooo,,, hana loolollloooooteee:A S 465:
 
[h=2][/h] Jumamosi, Septemba 01, 2012 06:29 Na Pendo Fundisha, Mbeya

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, Kapteni Sambwee Shitambala na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amejitokeza na kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupitia Wilaya ya Mbeya Mjini.

Shitambala alichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha ofisi za CCM wilayani humo, akiwa ni mwanachama wa 12 kati ya waliochukua fomu za nafasi hiyo kuwania nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu hiyo kwa Kaimu Katibu wa CCM wilayani humo, Julius Msaka, Shitambala alisema nia yake ni kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

Alisema nia na dhamira ya kugombea nafasi hiyo ni kuwatumikia wananchi ambao kwa sasa wanahitaji mabadiliko ya kweli katika uchumi na kijamii kwa ujumla.

“Nia na dhamira yangu ni kuwatumikia wananchi na kukiwakilisha chama changu kwa nia moja ya kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi na niwahakikishie kuwa CCM bado ina nafasi kubwa ya kuongoza nchi,’’ alisema Shitambala.

Wanachama wengine wa CCM waliochukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Obadia Mbilinyi, Shua Mwasanguti, Aggrey Mwasanguti, Dk. Stephen Mwakajumilo, Burton Mwankunda, Frank Mahemba, Edson Kajigili, Maria Nyagawa, Fatuma Kasenge, Richard Shanghvi na Daniel Fusi.

Kwa upande wake, Msaka alisema wanachama wote wamepewa onyo la kutojinadi wala kuchumbia wapiga kura hadi siku ya uchaguzi na vikao vinavyohusika kupendekeza majina ya wagombea waliokidhi vigezo vya nafasi hiyo.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]

Pamoja na udhaifu wa CCM lakini hawajafikia hatua ya kumchagua tapeli wa kisiasa kuwawakilisha.
 
Namfahamu huyu bwana vizur,alikuwa anatumiwa na CCM kuihujumu CHADEMA,ilifikia kipindi akishinda ubunge ana uza ushindi,ikafikia mahala akajifanya amekosea kujaza fomu.baad ya Uongozi wa CDM kumstukia akawai haraka kuhama chama kabla hajafukuzwa kwa aibu,alipofika Ccm ndio akajua kuwa CCM walikuwa wanamtumia kama kondomu,unatumia mara moja kisha hurudii tena,mpaka sasa anatapatapa na kuwatapeli watu kwenye kes uchwara
 
hhahhahhahhh anawezaa yulee ana kiswahiiliii mnooo atawashindaa
 
Namfahamu huyu bwana vizur,alikuwa anatumiwa na CCM kuihujumu CHADEMA,ilifikia kipindi akishinda ubunge ana uza ushindi,ikafikia mahala akajifanya amekosea kujaza fomu.baad ya Uongozi wa CDM kumstukia akawai haraka kuhama chama kabla hajafukuzwa kwa aibu,alipofika Ccm ndio akajua kuwa CCM walikuwa wanamtumia kama kondomu,unatumia mara moja kisha hurudii tena,mpaka sasa anatapatapa na kuwatapeli watu kwenye kes uchwara
hahhhahhh ni jeuurii yuleee atawashindaaa tuu,, ni kigeuugeuuu wawe nae maknii:flypig:
 
Pamoja na udhaifu wa CCM lakini hawajafikia hatua ya kumchagua tapeli wa kisiasa kuwawakilisha.

"Liwalo na Liwe" kama ccm watathubutu kumchagua huyu mamrukiwa kisiasa ccm watakuwa wamejipambanua jinsi walivyo haswaa katika siasa za Tz.
 
R.I.P Shitambala
kama aliuza jimbo la mbeya vivijini atashindwa kuiuza nec na kuiiingiza mjiniii alafuu anajua sheria na siasa si mchezoo yule bwana mdogo ni hatarii saanaa ,, sugu anamjua na dk, slaa na mbowe wanamfaham jeuri zake ni MNAFIKI
 
hahhhahhh ni jeuurii yuleee atawashindaaa tuu,, ni kigeuugeuuu wawe nae maknii:flypig:

anajidai anataka kuwatumikia wananchi kumbe muhuni tu,mnaweza mkamchagua mwishoni anauza ushindi,ana njaa mbaya hata 0712 Anaweza kutoa kisa kaona hera
 
kama aliuza jimbo la mbeya vivijini atashindwa kuiuza nec na kuiiingiza mjiniii alafuu anajua sheria na siasa si mchezoo yule bwana mdogo ni hatarii saanaa ,, sugu anamjua na dk, slaa na mbowe wanamfaham jeuri zake ni MNAFIKI

uhodari wake wa sheria unaishia mbeya tu,Lissu alisha anza kumbana kisheria akakimbia chama,jeuri yake na uhatari wake si kitu chocho kwa nguvu ya umma. Chitambala ni mtu mwepesi mno! Nafuu hata ya shibuda ukiwalinganisha kilo
 
Orodha yote uliyoiweka hapo nawafamu vizuri sana,mimi nimefanya kaz mbeya kwa kipindi cha miaka 4 na ninakama miez 7 sasa nimehama huko,kwaa taarifa wote hao hakuna msafi hata mmoja,pamoja na kuwa CCM hakuna msafi hao wameoza,mtu kama Balton kwanza sizani kama yupo sawa kiubongo,inaonekana anakaso frani hiv,we uje ukae nae mdiscuss mambo utaniambia
 
Haahaahaaaa!!! ameibukia NEC ya Ccm? na alivyochoka anatia huruma sana.R.I.P
 
Kutoka Mkoa mpaka wilaya kweli Shitambala kawa tambal bovu pole kaka wewe wamekuharibia hao mumiani waliokutumia
 
Back
Top Bottom