lusaka city
Senior Member
- Mar 17, 2015
- 146
- 116
SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU MKOA WA MBEYA.
Ndugu Viongozi wa CCM ngazi zote.
Ndugu Viongozi wenzangu wa shirikisho la vyuo vikuu taifa, mikoa na matawi.
Ndugu wanachama wenzangu wa chama cha Mapinduzi.
Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Awali ya yote namshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma kwa kutuwezesha sote kuifikia siku ya leo,tuna kila sababu ya kufanya hivyo kwani sote ni mashahidi yakuwa wenzetu wengi walikuwa na mipango mingi juu ya siku hii lakini haikutimia kwa sababu wamekwisha tangulia mbele ya haki,tuendelee kuwaombea kwa mwenyezi Mungu awape pumziko la milele, nasi tuendelee kumuomba Mola wetu aendelee kutujaalia afya njema, amani na mshikamano ili tuendelee kulitumikia kwa ustadi taifa letu na kukiimarisha chama chetu cha Mapinduzi.
Ndugu viongozi na wanachama wenzangu wa Chama cha Mapinduzi
Alhamisi ya tarehe 16 Disemba 2016 kati ya saa 2 mpaka saa 3 usiku Ndugu ALEX JULIUS KINYAMAGOHA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoa wa Mbeya, kupitia akaunti yake ya mtandao maarufu wa kijamii wa Facebook inayotumia jina la ALEX KINYAMAGOHA, na kupitia makundi mbalimbali ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp alisambaza waraka unaopinga mabadiliko yaliyojadiliwa na Halmashauri kuu ya CCM taifa iliyokutana mwanzoni wa juma hili Ikulu jijini Dar es Salaam, aidha, pamoja na mambo mengine Ndugu Alex Kinyamagoha alihoji uhalali wa uteuzi wa Mhe. Humphrey Polepole mkuu wa wilaya ya Ubungo kuteuliwa kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Ndugu Viongozi wenzangu wa Chama cha Mapinduzi na wanachama.
Sisi shirikisho la vyuo vikuu mkoa Mbeya tunasikitika kwa waraka ule uliosambazwa, hatujawahi kufanya kikao chochote cha kujadili mabadiliko yaliyopendekezwa na halmashauri kuu ya CCM taifa, hivyo waraka ule sio wa Shirikisho la vyuo vikuu bali ni wa kwake yeye.
Tunaomba radhi kwa viongozi wa CCM ngazi zote, wanashirikisho na wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi kote nchini kwa hiki kilichofanyika.
Tunawaomba muendelee kupuuza waraka huo kwa sababu sio wa shirikisho la vyuo vikuu.
Tunatambua madhara yaliyotokana na waraka huo, hatuna namna ya kufanya zaidi ya kuendelea kushikamana na kushirikiana, kusimamia na kutekeleza kwa vitendo kanuni zetu hasa zile kanuni za maadili.
Shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa Mbeya tunaunga mkono uteuzi wa Komredi Humprey Polepole, tunakupongeza Mhe. Mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Joseph Magufuri, wajumbe wa Kamati kuu na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa kwa vikao muhimu mlivyovifanya mwishoni mwa juma la jana na mapema juma hili tunalolimaliza.
Tunawahakikishieni kuwa tuko pamoja bega kwa bega kwenye kila hatua na mabadiliko yanayopitiwa na Chama chetu.
Tutaendelea kutoa ushirikiano wetu wa kila hali kuhakikisha chama chetu kina imarika zaidi na tunaendelea kushika dola.
Mungu kibariki chama cha Mapinduzi,
Mungu bariki Shirikisho la vyuo vikuu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Oddo Aidan Ndunguru,
Katibu wa Siasa na Uenezi,
Shirikisho la Vyuo Vikuu,
MKOA WA MBEYA