Shirikisho EAC janja ya nyani!

Shirikisho EAC janja ya nyani!

mathabane

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2013
Posts
2,405
Reaction score
1,898
Wakati Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi wamo katika mazungumzo ya kuunda shirikisho la kisiasa na kuitema kando Tanzania, ni wazi kabisa hiyo ni ujanja wa kuitisha Tanzani ili ikurupuke na kujiunga kichwakichwa kwa hofu ya kutengwa. Haiwezi kuwa EAC pasipo Tanzania. Kinacho fanyika sasa ni hasira za mkizi za hawa viongozi masalia walafi wanao waburuza raia wao. Lazima ifahamike wazi kuwa mlengwa mkuu ktk kile kilicho tarajiwa kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki si mwingine bali Tanzania na rasilimali zake. Asilimia kubwa ya Wanachama wa EAC mathalan Rwanda,Burundi hawana cha maana kuchangia zaidi ya kutegemea kufaidi fursa na rasilimali za watanzania. Nawapongeza Serikali ya Tanzania kwa kutokukurupukia Shirikisho la "kichovu" na badala yake mkakati uelekezwe SADC kwenye mataifa yenye "akili" na nia ya dhati kuwaondoa wanachama katika umaskini. Fikiria mfano ambapo EAC mnaondoa vikwazo vya usafiri na makazi: Watutsi wote, wakenya, warundi na waganda watalundikana Tanzania kuliko nchi yeyote katk umoja huu wa kinafiki. Mfanö rahisi ni utitiri wa wahamiaji haramu kutoka mataifa hayo ambao hawataki kurudi katika nchizao za halali. Kama vikwazo havijaondølewa hali ndio hii, je pasina vikwazo wakaachiwa waingie tu hali itakuwaje? Je, mtanzania anaweza anaweza kupata ardhi Kenya, Rwanda, burundi kirahisi, ilhali raia husika familia yake haijawahi kumiliki ardhi? Angalia mfumo/aina ya utawala/serikali ya Kigali na Kampala(dictatorship form of governments) kisha linganisha na Kenya na Tanzania hapo utaona ni sawa na kufuga kuku,kunguru na bundi kwenye tundu moja kitu kisichøwezekana. Wacha "waungane" japo muungano wao hautadumu maana ni mungano unao weza kufananishwa na sherehe ya fisi, wageni watarajiwa wamo mbuzi, swala, simba na nyka. "URAFIKI WA MASHAKA"
 
Dua la kuku alimpati mwewe. watu wako wanapiga kazi kuinua uchumi wa nchi wanachama.
wewe uko unajifariji .
 
Ukijitambua mwenyewe ni rahisi kumtambua adui yako theni ushindi. Taka ustake, hakuna shirikisho pale bila ya Tz. Hawa jamaa imewaudhi sana Tz kukataa kujiunga nao so wanacho kifanya ni sawa na mtu anae jamba kwa hasira kumkomoa mbaya wake matokeo yake anajinyea kutokana na kutumia ngvu nyingi kujamba. Ona raia wao walivo jazana kwetu. Tutaendelea kuwathamini kama majirani zetu, tutapiga nao story barazani ila chumbani hawakaribishwi.
 
Too much talking kwa watanzania, too much doing kwa wenzetu. Mzee Sitta pale Yuko kwa maslahi binafsi anawaza urais 2015 badala ya kupeleka hizi ajenda mezani. Huyu mzee Samwel Sitta Ni janga la kitaifa. Ndo matatizo ya JK kuweka washkaji katika wizara muhimu wanashindwa kutimiza wajibu.
 
Mi naamini Tanzania tunaweza kuendelea bila ya huo muungano....... kwani nchi zote zilizoendelea duniani zilikua kwenye muungano? kha!
 
Wakati Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi wamo katika mazungumzo ya kuunda shirikisho la kisiasa na kuitema kando Tanzania, ni wazi kabisa hiyo ni ujanja wa kuitisha Tanzani ili ikurupuke na kujiunga kichwakichwa kwa hofu ya kutengwa. Haiwezi kuwa EAC pasipo Tanzania. Kinacho fanyika sasa ni hasira za mkizi za hawa viongozi masalia walafi wanao waburuza raia wao. Lazima ifahamike wazi kuwa mlengwa mkuu ktk kile kilicho tarajiwa kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki si mwingine bali Tanzania na rasilimali zake. Asilimia kubwa ya Wanachama wa EAC mathalan Rwanda,Burundi hawana cha maana kuchangia zaidi ya kutegemea kufaidi fursa na rasilimali za watanzania. Nawapongeza Serikali ya Tanzania kwa kutokukurupukia Shirikisho la "kichovu" na badala yake mkakati uelekezwe SADC kwenye mataifa yenye "akili" na nia ya dhati kuwaondoa wanachama katika umaskini. Fikiria mfano ambapo EAC mnaondoa vikwazo vya usafiri na makazi: Watutsi wote, wakenya, warundi na waganda watalundikana Tanzania kuliko nchi yeyote katk umoja huu wa kinafiki. Mfanö rahisi ni utitiri wa wahamiaji haramu kutoka mataifa hayo ambao hawataki kurudi katika nchizao za halali. Kama vikwazo havijaondølewa hali ndio hii, je pasina vikwazo wakaachiwa waingie tu hali itakuwaje? Je, mtanzania anaweza anaweza kupata ardhi Kenya, Rwanda, burundi kirahisi, ilhali raia husika familia yake haijawahi kumiliki ardhi? Angalia mfumo/aina ya utawala/serikali ya Kigali na Kampala(dictatorship form of governments) kisha linganisha na Kenya na Tanzania hapo utaona ni sawa na kufuga kuku,kunguru na bundi kwenye tundu moja kitu kisichøwezekana. Wacha "waungane" japo muungano wao hautadumu maana ni mungano unao weza kufananishwa na sherehe ya fisi, wageni watarajiwa wamo mbuzi, swala, simba na nyka. "URAFIKI WA MASHAKA"
kENYA IANGALIE VIZURI UAMUZI WAKE WA KUUNDA SHILIKISHO. nCHI KAMA RWANDA, uGANDA NA bURUNDI HAZINA UTAWALA WA KIDEMOKRASIA, HIVYO HUENDA KENYA IKAPATA MATATIZO YALE YALE YALIYOMPATA MKONGOMAN KABILA NA BANYAMULENGE.

hata kama tutaadhilika kama nchi, lakini ni bora tukakaa na msimamo wetu wa kukataa kata kata kuunda shilikisho la kisiasa kuliko kwenda kichwa kichwa na kukaa pamoja na nchi kama Uganda,rwanda na burundi. halafu ni kweli kabisaa, tukiunganisha nchi hizi tuu, wakenya, waganda na wanyarwanda watahamia huku kwa wingi kuliko kwa sisi kwenda kwao.

Museveni na Kagame watoke kwanza ktk viti vya uraisi halafu ndipo tuunde shilikisho , la sivyo hiyo itakuwa united snake of east africa.
 
EAC ya sasa hivi imekaa kimaslahi zaidi especially kwa nchi ambazo hazina ardhi ya kutosha i.e. Kenya, Rwanda na Burundi. Kama wakiendelea na mpango wao huu haram itabidi serikali iwawekee visa kuingia Tanzania ndio njia ya kuwakomesha.
 
Ukijitambua mwenyewe ni rahisi kumtambua adui yako theni ushindi. Taka ustake, hakuna shirikisho pale bila ya Tz. Hawa jamaa imewaudhi sana Tz kukataa kujiunga nao so wanacho kifanya ni sawa na mtu anae jamba kwa hasira kumkomoa mbaya wake matokeo yake anajinyea kutokana na kutumia ngvu nyingi kujamba. Ona raia wao walivo jazana kwetu. Tutaendelea kuwathamini kama majirani zetu, tutapiga nao story barazani ila chumbani hawakaribishwi.

Nakupa big-up mkuu, hoja zako kimsingi zina mashiko. Naungana na wewe kuwa hapo hakuna shirikisho, zote hizo ni hasira kwa Tz kutokuwa wepesi kudanganyika kwa mambo wanayoona yatawaletea matatizo tuendako. Mfano suala la ardhi. Mimi nasema waache waungane, ila ninawasikitikia wakenya na rais wao mpya anayeburzwa na hawa jamaa mawili. Wakenya wanashindwa kujua sisi ndiyo rafiki na ndg zao wa kweli kuliko Rwanda, wanadanganywa wanadanganyika kirahisi. Wasije wakajuta baadaye
 
Wakati Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi wamo katika mazungumzo ya kuunda shirikisho la kisiasa na kuitema kando Tanzania, ni wazi kabisa hiyo ni ujanja wa kuitisha Tanzani ili ikurupuke na kujiunga kichwakichwa kwa hofu ya kutengwa. Haiwezi kuwa EAC pasipo Tanzania. Kinacho fanyika sasa ni hasira za mkizi za hawa viongozi masalia walafi wanao waburuza raia wao. Lazima ifahamike wazi kuwa mlengwa mkuu ktk kile kilicho tarajiwa kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki si mwingine bali Tanzania na rasilimali zake. Asilimia kubwa ya Wanachama wa EAC mathalan Rwanda,Burundi hawana cha maana kuchangia zaidi ya kutegemea kufaidi fursa na rasilimali za watanzania. Nawapongeza Serikali ya Tanzania kwa kutokukurupukia Shirikisho la "kichovu" na badala yake mkakati uelekezwe SADC kwenye mataifa yenye "akili" na nia ya dhati kuwaondoa wanachama katika umaskini. Fikiria mfano ambapo EAC mnaondoa vikwazo vya usafiri na makazi: Watutsi wote, wakenya, warundi na waganda watalundikana Tanzania kuliko nchi yeyote katk umoja huu wa kinafiki. Mfanö rahisi ni utitiri wa wahamiaji haramu kutoka mataifa hayo ambao hawataki kurudi katika nchizao za halali. Kama vikwazo havijaondølewa hali ndio hii, je pasina vikwazo wakaachiwa waingie tu hali itakuwaje? Je, mtanzania anaweza anaweza kupata ardhi Kenya, Rwanda, burundi kirahisi, ilhali raia husika familia yake haijawahi kumiliki ardhi? Angalia mfumo/aina ya utawala/serikali ya Kigali na Kampala(dictatorship form of governments) kisha linganisha na Kenya na Tanzania hapo utaona ni sawa na kufuga kuku,kunguru na bundi kwenye tundu moja kitu kisichøwezekana. Wacha "waungane" japo muungano wao hautadumu maana ni mungano unao weza kufananishwa na sherehe ya fisi, wageni watarajiwa wamo mbuzi, swala, simba na nyka. "URAFIKI WA MASHAKA"

Nimeupenda sana udadavuzi wako maana huu ndio ukweli wenyewe wa EAC hakuna la maana sana pale hata tukiachana nao. Ukiwaangalia vzuri hao jamaa wote almost wanafrustration ktk nchi zao so wanatafuta namna ya kujifariji na kutaka kutuingiza Kingi.
 
Wewe sio Mtanzania tumeshakujua siku nyingi. Tunakufanyia utaratibu tutakunasa tu na kukurudisha kwenu

hahahaah hauna uwezo huo ukifanikiwa nakupa 100 million tzsh.
yani unataka mtazamo tufanane wote.aliwezekani ilo
 
Too much talking kwa watanzania, too much doing kwa wenzetu. Mzee Sitta pale Yuko kwa maslahi binafsi anawaza urais 2015 badala ya kupeleka hizi ajenda mezani. Huyu mzee Samwel Sitta Ni janga la kitaifa. Ndo matatizo ya JK kuweka washkaji katika wizara muhimu wanashindwa kutimiza wajibu.
Anayewaza uraisi hujamuona Mkuu? Yupo anazunguka nchi nzima kashaanza kampeni mapema sana.
Sitta hana shughuli ya kufanya huko EAC.. Arudi home tuijenge nchi yetu. Hao walioamua kuanzisha shirikisho waendelee. Tunawatakia Heri na fanaka, sisi bado tupotupo kwanza!
 
Kama vip tujiunge na SADEC. wakubanana nae anakuwa 1 tu Malawi.
 
Rais wetu mpendwa, mambo mengine yote mabovu uliyotufanyia watanzania tumepuuza na kuvumilia. Lakini hili la EAC tunakuomba usituingize huko chondechonde.
Tunawasihi na viongozi wote na washauri wote wa rais, msituingize kwenye ndoa hiyo ya kina Kagame na M7
Waacheni na ndoa yao. Sisi tujenge nchi yetu na tuimarishe ndoa yetu na visiwa vya unguja na Pemba.
 
Ha! ha! ha! ha! UNITED SNAKES OF EAST AFRICA! ha! ha! ha!, wacha wararuane wenyewe kwa wenyewe ndipo akili zitawakaa sawa! ha! ha! ha! ha!
 
Back
Top Bottom