Shirikisha jamii yale ambayo MBUNGE wako ameyafanikisha JIMBONI……. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shirikisha jamii yale ambayo MBUNGE wako ameyafanikisha JIMBONI…….

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Meitinyiku L. Robinson, Apr 26, 2012.

 1. Meitinyiku L. Robinson

  Meitinyiku L. Robinson JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni imani yangu kuwa wengi wetu humu ndani kwa namna moja ama nyingine tumetoka katika majimbo tofauti ya Uchaguzi, jambo ambalo linatufanya tuwe na wawakilishi Bungeni.

  Wawakilishi ambao kwa juhudi zetu sisi wananchi na kwa juhudi zao binafsi kama Wawakilishi na vile vile kwa juhudi za Serikali (kama zipo) wanajitahidi kuhakikisha kuwa matatizo na shida walizo nazo Wapiga kura wao kama si zinatatuliwa zote basi sehemu flani ya matatizo hayo yanatatuliwa.

  Tumekuwa tukiona na kusikia juhudi za Wabunge wengi katika kulitetea Taifa letu kwa ujumla hili ni jambo la heri sana lakini binafsi ningependa vile vile kufahamu;

  1. Je huko watokako wananchi wanawachukulia vipi??
  2. Je wananchi wanaridhika na utendaji wao wa kazi??
  3. Je wananchi wanapata fursa ya kuzungumza na kushauriana na Wabunge wao??
  4. Je yale waliyoyategemea Wananchi yanatia moyo ama ni ubatili mtupu.

  Sikatai kwamba mpaka sasa ni miaka miwili imepita toka tutoke kwenye Chaguzi sasa isije ikatumika kama ni kigezo cha kusema kuwa muda bado upo hivyo Mbunge atafanya tu la hasha! Wakati tulionao ni sasa kama Biblia isemavyo siku moja kwa Mungu ni sawa na Miaka elfu na Miaka elfu ni sawa na siku moja hivyo nasi muda tulio nao ni sasa.

  Natambua kuwa yawezekana kwa namna moja ama nyingine Mbunge kama Binadamu mwingine ameshindwa kutimiza ahadi flani lakini je hata ahadi moja kweli?? Kati ya zile ahadi tatu, tano, kumi ama hamsini alizoahidi hata moja hajatimiza??

  Taja jina la Mbunge wako, Jimbo lako, kile ambacho unaona kinafaa kutushirikisha ambacho kakifanya na je unafikiri anafaa kurudi kukuwakilisha??

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki JF

  MEITINYIKU L. Robinson
   
Loading...