Shirikia la Kijasusi la KGB HAD 1991

Mr.Black

Member
Jun 9, 2014
95
73
Habari wana jukwaa pendwa la JF intelligence Leo naomba kuwaletea uchambuz kuhusu shirika la KGB had lilipovunjwa mwaka 1991 tutaonana majukumu yake na utendaji kazi wake.

Mods naomba uzi huu msihamishee

UKWELI NA HISTORIA YA SHIRIKA LA KIJAJUSI LA KGB. HADI MWAKA 1991

TANGULIZI

The KGB, or Komitet Gosudarstvennoy Bezopasnosti (Committee for State
Security) lilifahamika zaid kama shirika la ukusanyaji wa taarifa za
siri ambalo lilikuwa linafanya kazi zake ndani la muungano wa nchi za
Kisoviet lilipata kuwepo katka karline ya 20 , shirika hilo
limebadilishwa majina tofaut tofaut na kufanyiwa maboresho zaidi tokea
kipindi cha mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 , jina la KGB lilikuwa
jina rasmi kuanzia mwaka 1954 hadi mwaka 1991 ,ila kiukweli shirika
hili lilikuwepo muda mrefu hasa katika muundo wa kisiasa wa Taifa la
Urusi, kazi za shirika ziliongezwa zaid kutoka katika mambo ya siasa
ambayo shirika lilitimiza wakati likiitwa Okhrana katika kipindi cha
utawala wa Tsar Nicholas II’s . mwaka 1917 Illich Vladimir Lenin
aliamua kuunda Cheka kwa kutumia mabaki ya shirika wakati linaitwa
Okhrana . shirika la KGB lilikuwa na majukumu hadi nje ya Urusi katika
kukusanya taarifa za kijasusi na pia kuwalinda siri za kisoviet na
pia kujitenga na kutumia vitu vya mataifa ya magharibi, taarifa zao,
na hata mawazo yao ya watu wa kimagharibi .

HISTORIA YA KGB

mwaka 1880 Tsar Alexander II aliunda idara ya polisi kwa ajili ya
taifa la urusi ambayo wananchi wengi wa Urusi ilitambulika kwa jina la
Okhrana., majukumu ya mwanzoni kama ya shirika hili ilikuwa ni
kuchunguza, kujipenyeza na kuzuia itikadi za siasa kali katika katika
taifa hilo la urusi katika kipindi cha karnee ya 19 na 20, kwa kuweka
watu wa Okhrana katika makundi mbali mbali ya kimapinduzi . tsar
aliendelea kujulishwa aina zozote za mipango ya hatari katika utawala
wake na kuweza kuzuia mipango hiyo kwa haraka zaidi. katika ya mwaka
1908 na 1909, wanachama wa 4 kati ya 5 wa kamati ya St. Petersburg ya
chama cha Bolshevik Party walikuwa ni maafisa wa Okhrana. Nicholas II
alikuwa na uhakika zaid wa kiusalama kwa jinsi alivyoweza kujipenyeza
katika makundi ya kimapinduzi na hili lilipelekea kupuuzia onyo la
mapinduzi ya karibuni ya mwezi 11 mwaka 1916 kutoka kwa baadhi ya
wanachama wa serikali yake ambayo ilikuwa inaelekea kuanguka

mwezi wa pili mwaka 1917 zaid wafanyakazi 400,000 wa viwandani wa jiji
la St. Petersburg walichoshwa na hali ya njaa na mazingira mabovu ya
kufanyia kazi,katika maandamano haya Tsar Nicholas alishindwa
kuyazuia kwa sababu katika makundi yote ya kimapinduzi ambayo Okhrana
walikuwa wanafuatilia mienendo na taarifa zao, makundi haya ya
kimapinduzi hayakuhusu katika maandamano haya ya wafanyakazi kupinga
Utawala wa Tsar Nicholas.Maandamano katika miji , Jeshi la Urusi
liliamua kusimama pamoja na wananchi kupinga Serikali,wakati serikali
inavunjika , bunge la Nchi hiyo (DUMA) lilishikilia madaraka katika
kipindi cha serikali ya mpito , pia Tsar alilazimika kung'atuka
madaraka

katika kipindi cha miezi 9 ya kutokuwa na demokrasia ya kueleweka
iliwapa uhakika Illich Vladimir Lenin na chama chake cha Bolshevik
ambapo kwa siri waliweza kuunganisha nguvu zao.Baada ya mapinduzi ya
mwezi wa saba mwaka 1918 kushindwa kufanikiwa, chama cha Bolshevik
waliweza kupata ushawishi mkubwa katika kamati la jeshi la mapinduzi
ambapo mwaka waliweza kuvamia WinterPalace(jumba la utawala wa
kifalme enzi hizo) na jeshi la mapinduzi hakuwapata upinzani sana
kuweza kudhibiti winterpalace na hivyo Lenin akawa kiongozi wa
serikali mpya ya Urusi

Lenin alikuwa ana amini zaidi katika mabavu/utemi na hii ni kutoka na
kuvutiwa zaid na kikundi cha The jacobs(kilianzishwa huko paris mwaka
1789 hiki kilikuwa ni chama cha kisiasa chenye ushawishi mkubwa
kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa na kilikuwa ni chama chenye itikadi
kali na kilikuwa chama ambacho hawana huruma ) . lenin alimteua Feliks
Dzerzhinsky kama mwenyekiti wa baraza la People’s Commissariat katika
mambo ya ndani (NKVD) . Shirika hili majukumu yake ilikuwa ni
kuhakikisha wanazuia na kuzima harakati zozote za mapinduzi ndani ya
Taifa hilo.kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango bora zaidi ,
The Vecheka ilianzishwa kama mbadala ya NKVD , jina la CHEKA
lilifupishwa na watu tu wakati wa kutamka., shirika hili lilikuja kuwa
misingi ya KGB . lenin alimteua .Dzerzhinsky kuwa mwenyekiti wa
shirika hilo ( bwana .Dzerzhinsky ambaye alikuwa mchoraji ambaye
alifungwa jela miaka 11 kwa tuhuma za kujihusisha na njama za
mapinduzi kipindi cha utawala wa Tsar )hili lilikuwa ni chagua la
kwanza kabisa la lenin la kumteua kuwa mwenyekiti wa shirika la CHEKA

baada ya Bwana Dzerzhinsky kuwa mzoefu kwenye nafasi yake hiyo alianza
kufanya mabadiliko ya kiutendaji na kimuundo ndani ya shirika la CHEKA
ambapo aliamua kuhamisha makao makuu ya shirika la CHEKA kutoka St.
Petersburg kwenda jiji la Moscow ambapo shirika hilo la CHEKA
walihamia kwenye za zamani za kampuni ya Bima ya All Russian Insurance
.Shirika liliongezewa nguvu kutoka kuwa chombo cha kuchunguza hadi
kuwa na uwezo wa kumata, kufungulia kesi na kuwa na uwezo wa kufunga
watuhumiwa wote ,pia CHEKA walipewa uwezo wa kuongeza makambi kwa
ajili ya kuwafunga wafungwa wote wa kisiasa na wengine

kabla ya kubadilishwa jina shirika la CHEKA walihusishwa na mauaji ya
wananchi wa Urusi 500,000 tokea shirika hilo lianzishwe , kwa ajili ya
kuboresha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi na mataifa ya magharibi
na hivyo shirika la GPU lilianzishwa ambapo kimamlaka lilikuwa chini
ya NKVD na halikuwa na nguvu sana kama CHEKA lakin baadaye kwa
shinikizo la Lenin bwana Dzerzhinsky aliweza kubakia kuwa mwenyekiti
wa GPU na aliweza kufanya shirika la GPU kuwa na nguvu sana kama
kipindi cha CHEKA . na baaada ya kupatikana kwa katiba mpya ya
muungano wa kisoviet mwezi wa saba mwaka 1923 GPU lilibadilishwa jina
na kuitwa OGPU likiwa na lengo la mshikamano ambapo Lenin alikuwa
anataka kutimiza ndani ya Taifa hilo la Kijamaa kuwa wenye mshikamano

mwaka 1924 baada ya Lenin kufariki dunia , Joseph Stalin alikuwa
kiongozi wa taifa hilo na hivyo Dzerzhinsky ambaye alikuwa anamuunga
mkono Joseph Stalin kipind cha harakati za kupata uongozi, kupitia
hilo Joseph Stalin aliamua kumwacha abakie katika nafasi ya kuwa
mwenyekiti wa shirika la OGPU na baada ya Dzerzhinsky kufariki mwaka
1926 nafasi yake ilichukuliwa na Vyacheslav Menzhinsky. moja ya
majukumu ya OGPU ilikuwa ni kuhakikisha wananchi wote wa taifa la
Kisoviet wana utii , ambapo joseph stalin alianzishwa mashamba ya
ujamaa kwa wanananchi wote.kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya nje OGPU
walitoa ngano na mikate kutoka mashambani kitu kilichopelekea vifo vya
watu zaidi million 5

baada ya kifo 1934 cha Vyacheslav Menzhinsky ambacho kilikuwa ni kifo
chenye utata sana, nafasi yake ilikuja kujazwa na Genrikh Yagoda
ambaye kitaalum alikuwa ni mfamasia , chini ya utawala wake OGPU
waliweza kupanua maabara zake na walianzisha tafiti za kisayansi
katika tafiti za kibailojia na kemikali za kuangamizi, ambapo Yagoda
mwenyewe alipenda zaid kufanya tafiti za binadamu akiwatumia wafungwa
wa makosa mbali mbali , baaaye Yagoda alikuja kuliwa baada ya kukili
kosa la kufanya mauaji ya Menzhinsky ili aweze kushika nafasi ya
uenyekiti wa shirika la OGPU

Nikolai Yezhov alichaguliwa mwenyekiti mpya wa OGPU,katika kipindi
hiki matukio ya kigaidi ndani ya Taifa la kisoviet yalikuwa yamefikia
kilele , katika kipind hiki vijana 3000 wa Yagoda waliuliwa kati ya
mwaka 1936 na 1938 , na baadaye kwa Stalin kwa hofu ya kuja kushindwa
kumdhibiti Yezhov wakiwa pamoja Stalin alimpiga risasi Yezhov ilikuwa
ni mwaka 1938
baada ya hapo aliteuliwa Lavrenti Beria kuwa mwenyekiti wa KGB
aliongoza kwa miaka 15 ambapo Beria alikuwa ni kiongozi mwenye Akili
sana ambapo aliweza kutanua NKVD ikiwa chini ya OGPU na mwaka 1941
mashirika yalitenganishwa ambapo shirika jipya la NKGB wao walikuwa na
wajibu wa usalama wa nani wa taifa hilo la usoviet na kuzuia aina
yoyote ya kazi/mipango ya majasusi kutoka nchi zingine ,wapiganaji wa
kwanza, kusimamia makambi ya kukusanya na kusimamia vibarua,vita ya
msituni na kazi mbalimbali kipindi cha vita na mjeruman wakat wa vita
kuu ya pili ya dunia. mkuu wa NKGB alikuwa anaitwa Vseveolod Merkulov
ambaye alikuwa ni mtiifu sana kwa Beria na hivyo kugeuza NKGB kama
chombo cha Beria ili kumdhibiti Beria ndani ya NKGB mwaka1950,
Merkulov alibadilishwa na Viktor Abakumov akwa boss wa NKGB ambaye
hakuwa na mahusiano ya karibu na Beria lakin baadaye beria aliweza
kumshawishi Stalin kuwa Viktor Abakumov alikuwa anataka kumpindua
hivyo mwaka 1951 aliuliwa

baada ya kifo cha stalin 1953 beria alijaribu kushika nafasi ya stalin
kama dikteta wa taifa hilo lakin alidhibitiwa na kuuliwa mwaka 1953 ,
baada ya Nikita Khrushchev kuwa kiongozi wa Taifa hilo la kisoviet
aliweza kufanya mabadiliko ya jina la mwisho mwaka 1954 na kuunda KGB
ambapo shirika lilikuwa na wajibu wa kudhibiti jeshi la polisi,
kuendesha oparesheni mbali mbali, kulinda mipaka ya nchi na
kuhakikisha usalama wa ndani wa taifa hilo



HISTORIA YA KGB(1954-1991)

Kwa watu wengi tumezoea kuita KGB ila kirefu chake ni Komitet
Gosudarstvennoi Bezopanosti of the Soviet Union shirika hili
lilianzishwa mwaka 1954 huko moscow, shirika hili awali lilianzishwa
kama kamati ya ulinzi ya Taifa la Usoviet na lilijumuishwa kwenye
baraza la mawaziri , ila KGB walifanya kazi zao kwa uhuru na kwa
kujitegemea kuliko taasisi yoyote ya serikali ya Taifa hilo la
Usoviet.KGB lilikuwa ni shirika kubwa zaidi la kipelelezi duniani na
chombo cha ulinzi cha Taifa hilo , pia KGB ilijihusisha kwenye kila
idara na kila kitu katika maisha ya wa watu ya kila siku katika Taifa
hilo la muungano wa Usoviet. KGB ilikuwa ni siri na ni shirika ambalo
lilijitenga zaid, na inasemekana kuwa ilikuwa ni vigumu sana
kufahamika kwa wananchi , hawakujua nini kinaendelea au kinafanywa na
shirika hilo, pia KGB ilikuwa imegawanyika katika idara mbali mbali na
kila idara ilikuwa inaongozwa na mwakilishi ambaye lengo kuu ni
kusimamia kanuni za usalama wa Taifa hilo la usoviet, zaidi ya watu
500,000 wamefanya kazi ndani ya shirika la KGB na maelfu ya wapelelezi
KGB walikuwa katika kila kona katika mataifa mbali mbali ulimwenguni
kwa malengo ya kutimiza majukumu mbali mbali yenye manufaa kwa taifa
hilo .Mwaka 1977 katiba ya Usoviet ilitamka kuwa baraza la mawaziri
lita ratibu na kuongoza kazi za mawaziri pamoja na kamati za kitaifa
ikiwemo KGB. Tarehe 5 mwezi wa saba mwaka 1978 mabadiliko mapya ya
kisheria yalipitishwa ambapo yalibadili hadhi ya KGB , na kuwa
Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri wa Taifa hilo la kisoviet

Jukumu la msingi kabisa la KGB ilikuwa ni kukusanya taarifa za
kijasusi kutoka mataifa mengine duniani, kulinda na kuzuia mataifa
mengine kuweza kupata taarifa za kijasusi kutoka katika taifa hilo la
Kisoviet,kuhakikisha na kulinda usiri katika polisi, Askari wa KGB,
kuzuia migomo na maandamano katika Taifa hilo, kuhakikisha kuna usiri
kwa walinzi wote wa Boda za Taifa hilo,na walikuwa na jukumu la
kukusanya taarifa za kijajusi(electronic espionage) kupitia kutegesha
simu kwa ajili ya kupeleleza, kutumia tap recorder,keywatchers, n.k
lakin pia KGB walisimamia maadili ya kisoviet yanafuatwa na pia
walisambaza itikadi za kisovieti kwa propaganda . Majasusi katika
kitengo hiki walihakikisha wananchi wanapata taarifa ambazo
zimeruhusiwa tu na serikali ndiyo ambazo wananchi wapata

Kama ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya kisoviet, KGB lilianza
kuanguka baada tu ya aliyekuwa Raisi wa Taifa hilo Mikhail Gorbachev
aliposhika tu madaraka alianza kufanya mabadiliko katika shirika hilo
ambapo maofisa wengi wa KGB walianza kutambulika wenye vyombo vya
habari na hakukuwa na usiri tena wa maofisa wanao fanya kazi kwenye
shirika hilo na pia maofisa wengi wa KGB waliweza kuruhusiwa kufanya
mahojiano na vyombo vya habari, muda huo huo majukumu mengi ya KGB
yalianza kupoteza mwelekeo tofaut na malengo yao ya awali. na baadaye
KGB walibadilisha jina na kuitwa RFIS (Russian Foreign Intelligence
Service) na liliendelea kufanya upelelezi nje ya Taifa hilo



MFUMO NA UTENDAJI KAZI WA KGB
KGB ilikuwa inaongozwa na mwenyekiti ambaye alikuwa ana
ithinishwa/kupitishwa na bunge la nchi hiyo lakin mwenyekiti huyu wa
KGB alikuwa anateuliwa na chombo cha watungaji sela , chini ya
mwenyeti wa KGB kulikuwa na wasaidizi wa awali walikuwa wanakuwa mmoja
au wawil na kulikuwa na wasaidizi wa pili wa mwenyekiti wa KGB
walikuwa wanakuwa 4 au 6 hawa pamoja na wakurugenzi wakuu wa KGB kwa
pamoja waliunda baraza la KGB ambalo lilikuwa na wajibu wa kusimamia
utekelezaji wa mambo mbali mbali ndani ya KGB

majukumu ya KGB yaligawanywa katika mafungu 4 ; 1. kulinda Taifa la
usoviet dhidi ya majasusi kutoka nje 2, kufichua na kuchunguza makosa
ya kisiasa na kiuchumi ambayo yanafanywa na wananchi wa Taifa hilo, 3,
kulinda mipaka ya Taifa hilo , 4 na kulinda siri za Taifa hilo . ili
kuweza kutimiza majukumu yote haya kati ya wa soviet 390,000 na
700,000 walifanya kazi katika bodi sita za wa wakurugenzi wa KGB

MKURUGENZI MKUU WA KWANZA;Alikuwa anawajibika kwa utendaji kazi na
kazi zote za kijasusi nje ya mipaka ya taifa hilo .ndani kurugenzi hii
kulikuwa na idara zingine chini yake ambazo ziligawanywa kiutendaji
kazi (mafunzo ya kijasusi, ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za
kijasusi) na kujua jiografia ya dunia nzima ili kuweza kufanya
utendaji kazi wao kwa ufanisi, kwa kuzingatia aina kazi katika
kurugenzi hii walikuwa wanateua mkurugenzi aliyefanya vizuri zaidi
kuliko wakurugenzi wengine na mwenye historia nzuri ya Kitaalum na
mwenye uwezo wa lugha za ya moja na mwenye imani kali zaidi ya kijamaa

MKURUGENZI MKUU WA PILI;Alikuwa anawajibika kuhakikisha udhibiti wa
mambo yote ya kisiasa na kuzuia ushawishi kutoka mataifa ya nje ndani
ya Taifa hilo, walikuwa na wajibu wa kuchunguza makosa ya kisiasa,
kiuchumi, kuzuia mabalozi au maofisa wa balozi kuweza kujichanganya
na wananchi wa kawaida wa kisoviet, walikuwa na wajibu wa kudhibiti na
kuangalia watalii wanaokuja kwenye taifa hilo na pia kuanglia na
kufuatilia wananchi wote wa kigeni waliokuwa wanasoma nchini humo

MKURUGENZI MKUU WA TATU; Kurugenzi hii wao walihusika na kuzuia
ujasusi katika majeshi yao, na walizuia na kuchunguza shughuli zote za
kisiasa ndani ya jeshi la kisoviet,ndani ya kurugenzi hii
ziligawanyika idara 12 ambazo walikuwa na wajibu wa kuangalia na
kuchunguza majeshi mbali mbali ya taifa hilo, pamoja na kazi zote za
bunge

MKURUGENZI MKUU WA NNE; hawa walikuwa na wajibu wa kuangalia usalama
wa ndani wa taifa hilo kwa kushirikiana na kurugenzi namba 2. iliundwa
1969 kudhibiti wapinzani wa mawazo ya kisiasa mbali na ujamaa na hawa
walikuwa na kazi ya kuzuia na kuvunjwa upinzani katika jamii za
kidini na hata wasomi ambao walikuwa wanapinga serikali ya kisoviet
walidhibitiwa au kupotezwa maisha

MKURUGENZI MKUU WA TANO;hawa walikuwa wanawajibika katika suala zima
la mawasiliano ndani ya taifa hilo, pia walihusika kuangalia mifumo ya
mawasiliano katika mataifa mengine ya nje,kulinda mawasiliano katika
kiwango cha hali ya juu ili maadui wasiweze kujua, walihusika kufanya
mawasiliano idara zingine za KGB walio nje ya taifa hilo pia
walihusika katika kubuni na kutengeneza vifaa vya kisasa vya
mawasiliano

MKURUGENZI MKUU WA VIKOSI VYA KULINDA BODA;Hawa walikuwa na wajibu wa
kulinda mipaka ya soviet ardhini na majini na walikuwa na majukumu ya
kuhakikisha wanazuia aina yoyote ya mashambulizi au uhamiaji haramu
ndani ya taifa hilo wakiwa na siraha zozote, kuangalia meli zote za
kigeni eneo lote la taifa hilo

KUSAMBARATIKA KWA SHIRIKA LA KGB
Tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka 1991 kiongozi wa Taifa la kisoviet Mikhail
Gorbachev alikuwa amevamiwa na wana mapinduzi ambao walikuwa wanataka
kupindua utawala wake , hawa wapangaji njama za mapinduzi akiwemo
luteni jenerali Yuri Plekhanov , alikuwa ni mwenyekiti wa walinzi wa
Raisi,Gorbachev’s na wengine walikuwa wanaona kama ujamaa unaenda kufa
chini ya utawala wa Gorbachev walicho amua ilikuwa ni kumshinikiza
ajiuzuru uraisi au akabidhi mamlaka kwa makamu wa Raisi Gennadi
Yanayev. baada ya kukataa kufanya hivyo walinzi wa KGB walizingira
nyumba yake na kuweza kumzuia kufanya mawasiliano na mataifa mengine
duniani na walimzuia asiwezee kutoka
pia jiji moscow wakurugenz saba wa KGB waliokuwa wanfahamika kama
Alpha Group walipewa maagizo kudhibiti jengo la shirikisho la urusi ,
tofauti na walivyo tarajia wanamapinduzi hao , jengo halikudhibiti na
kiongozi wa kutokutii amri alikuwa Mikhail Golovatov baadala yake
walipanga kufanya hivyo siku inayofuata makundi ya upinzani
yakiongozwa na Boris Yeltsin waliweza kulinda jengo la shirikisho la
urusi na hivyo mpango wa kuteka jengo hilo haukufanikiwa

baada ya kutambua mipango yao ya mapinduzi imeshindikana waliopanga
njama walijaribu kufanya mazungumzo na Gorbachev akiwa bado
ameshikliwa na wao lakin Gorbachev alikataa kuonana na wana mapinduzi
na hata baada ya vikosi vitiifu kufika kumkomboa wengi walikamatwa na
mapinduzi yakawa yamezuiliwa

Vinara 8 wa muhimu wa mapinduzi walio itwa ''Gang eight'' waliojaribu
kumpindua Gorbachev walikuwa , Makamu wa Raisi, mwenyekiti wa
KGB,Waziri wa ulinzi, waziri mkuu,wawakilishi wa baraza la usalama la
soviet,president state enterprise,industrial construction, Transport
,communication,and waziri wa mambo ya ndani ,kati ya hao saba
walikamatwa na kuhukumiwa kwa makosa ya kutaka kupindunia nchi na
mmoja alijipiga risasi ya kichwa

baada ya hapo Gorbachev alifanya mabadiliko makubwa sana ikiwemo
kuvunja umoja wa mataifa ya kisoviet na huo ukawa mwisho wa ujamaa
kule urusi na dunian kote, kati ya watu waliokuja kuondolewa
madarakan/kubadilishwa alikuwa ni Vladimir Kryuchkov ambaye alikuwa
mwenyekiti wa KGB kwa miaka 3 na nafasi yake ilikuja kujazwa na Vadim
Bakatin kama mwenyekiti wa KGB ambaye baadaye alitoa maoni kuwa KGB
ifungwe tu, na huyu alikuwa ni moja kati ya watu ambao Gorbachev
alimpenda maana alikuwa ni mtiifu sana kwake. na hatimaye October 24,
1991 KGB ikafungwa rasmi kazi zake

JE INAWEZEKANA KGB IPO LEO (UWEPO WAKE KIPINDI HIKI)
KGB ilianzishwa Tarehe 13 mwezi wa 3 1954 na kufa rasmi tarehe 24
mwezi October 1991 chini ya utawala wa Vadim Bakatin na Mikhail
Gorbachev tofauti na vipindi vya nyuma kabla ya 1954 KGB haikufa ila
ilifanyiwa tu marekebisho kulingana na mahitaji ila 1991 KGB ilikufa
rasmi na kuharibiwa vibaya na kujikuta yanabakia mashirika madogo sana
baada ya kuvunjwa na hivyo kujikuta wanabanwa na kushindwa kujitanua
na kuwa wenye nguvu kama ilivyokuwa zamani enzi za KGB yenyewe.
yafuatayo ni mashirika madogo yanayofanya kazi kwa sasa

1.THE FOREIGN INTELLIGENCE AGENCY;hili liliundwa baada ya kufa kwa KGB
na kwa sasa wanahusika zaid na utendaji kaz nje ya urusi, kukusanya
taarifa za kijasusi na kufanya uchambuzi wa taarifa za kijasusi.
zamani kaz hiz zilikuwa chini ya Mkurugenzi mkuu wa kwanza
2.The Federal Agency for Government Communications and Information;ni
muunganiko wa kurugenzi kuu 8 na kurugenzi 16 ambao kwa pamoja wana
wajibu wa kuhakikisha usalama wa mawasiliano na ujasus na maelfu ya
watu waliokuwa KGB wamejiunga na Federal Protective Service na the
Presidential Security Service.ambayo inawajibika katika kulinda
Kremlin pamoja na viongozi wengine wa serikali.
3. The Federal Security Service ; hii iliundwa mwaka 1993 baada
kufukuzwa aliyekuwa waziri wa ulinzi wa taifa hilo , shirika lina watu
zaidi ya 75000 ambao kwa pamoja wana wajibu wa kulinda usalama wa
ndani wa taifa hilo

MAJINA YA VIONGOZI WALIO WAHI KUONGOZA KGB

1.Felix Dzerzhinsky(Alizaliwa1877–alikufa1926)- Aliongoza
KGB(CHEKA)KUANZIA TAREHE 20 December 1917- HADI TAREHE 20 July 1926

2.Vyacheslav Menzhinsky(1874–1934)-Aliongoza KGB( GPU-OGPU) KUANZIA 30
July 1926 Hadi Tarehe 10 May 1934

3.Genrikh Yagoda(1891–1936)-Aliongoza KGB(NKVD) KUANZIA 10 July 1934
HADI 26 September 1936

4.Yakov Agranov(1893–1938)-Aliongoza KGB KUANZIA 29 December 1936 HADI
15 April 1937

5.Mikhail Frinovsky (1898–1940)-Aliongoza KGB KUANZIA 15 April 1937
HADI 28 March 1938

6.Lavrentiy Beriya (1899–1953)-Aliongoza KGB KUANZIA 29 September
1938 HADI 26 June 1953

7.Ivan Serov(1905–1990)-Alianza 13 March 1954 HADI 8 December 1958

8.Alexander Shelepin(1918–1994)ALIANZA 25 December 1958 HADI13 November 1961

9.Vladimir Semichastny (1924–2001)13 November 1961 HADI 18 May 1967

10.Yuri Andropov(1914–1984) ALIANZA 18 May 1967 HADI 26 May 1982

11.Vitaly Fedorchuk (1918–2008) ALIANZA 26 May 1982 HADI 17 December 1982

12 Viktor Chebrikov(1923–1999)ALIANZA 17 December 1982 HADI 1 October 1988

13.Vladimir Kryuchkov(1924–2007)ALIANZA 1 October 1988 HADI 22 August 1991

14.Leonid Shebarshin(interim)(1935–2012) ALIANZA 22 August 1991 HADI
23 August 1991

15.Vadim Bakatin (born 1937).ALIANZA 23 August 199122 October 1991


Imeandikwa na
Mr. Black
Jamii forum


Hekima ni jambo jema
 
Mbona wanasema Putin aliwahi kuwa mkurugenz hapo na sjamuona kwenye list??
 
KGB nawaelewa sana, sema hujuma na kuvunjika kwa USSR ndio kiliochoangusha KGB.

To me the KGB was far more better than any other Intelligence organization
Who lied to you ukiwa KGB unakuwa better? To be the most efficient intelligence apparatus kama KGB yenye kusambaa dunia nzima sio suala la kitoto.

Baadhi ya maofisa ya KGB iliwapasa kutelekeza familia zao kwa zaidi ya miaka 40 ili kufanikisha baadhi ya operations zenye risk kubwa sana.

Kazi za ujasusi ni kazi iliyojawa na uzalendo wa hali ya juu saana. Officers wanakuwa tayari kupoteza kila kitu kwa ajili ya usalama wa taifa husika.
 
Labda Putin alikua ktk hivi vishirika vidogo vidogo vilivyoanzishwa, baada ya kufa Hilo kubwa
Putin alikuwa ni jasusi mkazi (resident spy) wa KGB huko Dresden Ujerumani, and that's why Putin anafahamu kijerumani kwa ufasaha sana. Moja kati ya sifa ya jasusi mkazi ni kuwa na weledi wa kutosha katika lugha ya nchi lengwa (host country)

Wadadisi wa mambo wanasema kuwa mkuu wa idara ya ujasusi ni lazima uanzie cheo cha major genera kwenda juu. Putin alikuwa boss wa mwisho wa KGB akiwa na cheo cha colonel tu baaaas. Hii inatokana na makubwa aliyoyafanya akiwa Dresden Ujerumani. Alikuwa na CV kali saana plus kujuana na Micahel Gorbachev ndio akawa boss wa KGB.
 
Ni potential piece of information. Nitarudi kusoma baada ya kuamka.
Ngoja nilale kwanza.
 
Putin alikuwa ni jasusi mkazi (resident spy) wa KGB huko Dresden Ujerumani, and that's why Putin anafahamu kijerumani kwa ufasaha sana. Moja kati ya sifa ya jasusi mkazi ni kuwa na weledi wa kutosha katika lugha ya nchi lengwa (host country)

Wadadisi wa mambo wanasema kuwa mkuu wa idara ya ujasusi ni lazima uanzie cheo cha major genera kwenda juu. Putin alikuwa boss wa mwisho wa KGB akiwa na cheo cha colonel tu baaaas. Hii inatokana na makubwa aliyoyafanya akiwa Dresden Ujerumani. Alikuwa na CV kali saana plus kujuana na Micahel Gorbachev ndio akawa boss wa KGB.


Putin , ni kitu kingine kabisa anaelewa lugha zote za UN kwa ufasaha kwa ujumla anazungumza lugha 7 zitumikazo; na anazizungumza kwa ufasaha kama mzawa wa nchi au mabara yanayotumia lugha hizo.

Kwa kifupi, Putin is a genius and a smart thinker. Ndiyo maana unaona Obama alikojoa kwa Putin, Trump yeye hajui hata cha kufanya.
 
Kabla, sijalala,

Inaonekana jina la Vladimir lina nafasi tangia kitambo sana hapo Russia.
Wako 3 wakurugenzi mean that, Putin wa Leo ana undugu wa karibu kati ya hao Vladimir walioongoza shirika.

Kwa hiyo, ni kweli hii kazi wanapeana kazi kwa kufuata life trees chart.

Mean that, kama hauna ndugu huko hizi kazi utazisikilizia kwa majirani tu walio na ndugu zao huko .

Mmmmmh, Kweli JF haijawahi kuacha siri zozote zisiwekwa wazi. Heshima.nyingi sana, Kwa The bold Infantry Soldier, Beautiful Nkosazana , Poise Nifah . Girl Next-door @et al
 
Who lied to you ukiwa KGB unakuwa better? To be the most efficient intelligence apparatus kama KGB yenye kusambaa dunia nzima sio suala la kitoto.

Baadhi ya maofisa ya KGB iliwapasa kutelekeza familia zao kwa zaidi ya miaka 40 ili kufanikisha baadhi ya operations zenye risk kubwa sana.

Kazi za ujasusi ni kazi iliyojawa na uzalendo wa hali ya juu saana. Officers wanakuwa tayari kupoteza kila kitu kwa ajili ya usalama wa taifa husika.
Kwel kabisa ujasusi ni uzalendo kwanza
 
Kabla, sijalala,

Inaonekana jina la Vladimir lina nafasi tangia kitambo sana hapo Russia.
Wako 3 wakurugenzi mean that, Putin wa Leo ana undugu wa karibu kati ya hao Vladimir walioongoza shirika.
Vladimir (ruler of the world) ni kitambulishi cha jina kama unavosikia Kim huko korea!..
 
Back
Top Bottom