Shirika la Nyumba kung'arisha nchi. Laanza kujenga nyumba 1000 Dodoma

Dodoma Demand

Senior Member
Oct 6, 2021
130
74
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza mradi mkuwa wa ujenzi wa nyumba 1,000 mkoani Dodoma ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2023.

Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dkt. Maulidi Banyani, kwenye ziara ya kukagua na kutembelea maeneo zinapojengwa nyumba hizo Chamwino na Iyumbu, amesema mradi huu unajengwa katika awamu tatu, awamu ya kwanza zinajengwa nyumba 400 ambapo nyumba 300 zitakuwa Iyumbu na Chamwino nyumba 100, awamu ya pili itahusisha nyumba 325 na awamu ya tatu nyumba 275.

Adha, Dkt. Banyani amesema nyumba 100 zinajengwa kwa mtindo wa ghorofa wilayani Chamwino na zitapangishwa kwa wananchi na taasisi mbalimbali huku 300 zinazojengwa Iyumbu ni kwa ajili ya kuuzwa.

Akifafanua zaidi Dkt. Banyani amesema mradi huu unajengwa kwa msaada wa Serikali ambayo ililikopesha Shirika mkopo nafuu wa Sh. Bilioni 20 na Shirika likatoa Sh. Bilioni 1.4 na kufanya jumla ya gharama ya mradi huo kufikia Sh. Bilioni 21.4.

Amesema mradi wa nyumba za Chamwino umefikia zaidi ya asilimia 35 na mradi wa Iyumbu wa nyumba 300 umefikia asilimia 40, miradi hii inatarajiwa kufikia mwezi Juni shirika litaanza mchakato wa mauzo.

Akizungumzia bei, amesema kuwa nyumba 300 za Iyumbu zitauzwa bei fedha taslimu ama kwa makubaliano na mabenki kwa gharama ya kati ya Sh Milioni 50 - 99 kutegemeana na ukubwa wa nyumba na eneo huku pia kukiwa na maeneo ya mapumziko, biashara, viwanja vya michezo, maduka, shule na makao makuu ya shiriko hilo. Lengo ikiwa ni kuanza kutumia ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio amesema kuwa kampuni imejiongeza katika maeneo yote mawili Chamwino na Iyumbu kwa kununua mashine 17 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 60 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 20,000 kwa siku, kitendo hicho kimeimarisha ubora wa matofali wanayotumia na kupunguza gharama ununuzi kutoka kwa watu binafsi.

thumb_2602_800x420_0_0_auto.jpg
 
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeanza mradi mkuwa wa ujenzi wa nyumba 1,000 mkoani Dodoma ambazo zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2023.

View attachment 1971681
Juzi kwenye hotuba yake Rais pia alisema wamewadhamini mkopo wa zaidi ya bil.70 Ili kumalizia mradi wa Kawe, Morocco na Regency..

Shirika linafudi kwenye ufanisi wake kabla ya kuingia huyu hapa 👇

2952061_JamiiForums569115795.jpg
 
Tatizo ni lile lile ukishaona miradi ina awamu ujue kukamilika kwake ni 65%. Miradi mingi ya nhc ni mfu mfano pale morocco. Hapo wamejinadi kutakua na viwanja vya michezo shule nk. Ila subiri mradi uishe ni tofauti kabisa.
 
Mwendazake ndio alisababisha yote,hujamsikia mama juzi kwamba wawewadhamini Mabilioni wamalizie hiyo miradi ya Moroccan,Kawe na Regency?
 
Back
Top Bottom