Shirika la Makumbusho ya Taifa Posta mnatia aibu Wizara ya Maliasili na Utalii

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,055
8,672
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi ni mdau wa sekta ya utalii na tunaleta wageni wengi tu hapo Makumbusho ila kutokana na aibu na fedheha kutoka kwa wageni tunaowaleta imebidi niliseme hili.

Choo kinachoonekana pichani kinatumika na wageni pamoja na wafanyakazi wa shirika la Makumbusho na ni siku ya 4 sasa hali yake ni mbaya, uozo wa harufu mithili ya mzoga,Mh Kigwangallah hii ndio kaulimbiu ya TANZANIA UNFORGETABLE unayohamasisha? Basi kweli imekuwa aibu unforgettable kwani miongoni mwa wageni wetu wamegoma kuja kutembelea hapa baada ya wenzao kuwajuza fedheha hii inayotia aibu kama Wizara nzima sasa.

Katibu Mkuu Prof Mkenda, ofisi tajwa hapo lift mbovu mwa miaka dahali sasa, huduma hovyo ikiambatana na vitendea kazi kama vionyeshwa hafifu, kweli ofisi kama hii ambayo ipo puani mwa Ikulu na usoni mwa ofisi na makazi ya Mh Raisi mnaienzi kwa aibu hii?

Wahusika mnasubiri hadi Rais awatembelee?

Mnanajisi kauli mbiu ya #Tanzania Unforgettable, sasa nafikiri mnataka mnajisi na kauli mbiu ya Mh Rais isomeke kama awamu ya V-WONDERS!!

Mdau anayewakilisha fedheha za wageni kwa Taifa letu
IMG-20191122-WA0079.jpg
IMG-20191122-WA0078.jpg
 
Mkuu kwanini usingeenda kununua soda aina ya koka kola ukaja ukapamwagia pakawa safi?,maana nasikiaga koka kola huwa ni nzuri kwa kusafishia kwenye vigae na masinki!ni vema pia ukayapeleka malalamiko yako pale ofisi ya mali asili na utalii ili walifanyie kazi
 
Labda ndio unforgettable yenyewe hio

Hivi hata hao wenye ofisi nao wanaingia na kutoka ina maana huo uchafu hawauoni.?
 
Hawa jamaa si ndo bodi yao ilivunjwa na Waziri Kigwangalla au sio hawa? Na Mkurugenzi Mkuu wao alipewa mwezi mmoja ajitetee ili asiondolewe pamoja na bodi. Kama yule mkurugenzi alibaki na uongozi wake unashindwa kusimamia mambo madogo kama haya basi HAWATOSHI kabisa kwenye nafasi zao. Mi nilishaenda siku moja nikakosa hata tour guide wa kunitembeza ikabidi nizurure tu mwenyewe mle ndani nikashangaa natokea ofisini kwa watu, bure kabisa hii makumbusho.
 
Back
Top Bottom