Shinyanga Mjini Vs Tabora Mjini

Wewe nawe unaota

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee sasa huu ni ubishani wa kwenye Gahawa, kama tatizo ni traffic lights hata Kahama zipo tena ni wilaya tu.

Let's argue kuhusu vitu vya maana, kama mademu wa bila kutongoza Ipuli na madem wa kuhonga wanaume wa Ngokolo A na B
Kahama siyo shai mkuu sema shai wapi taa za barabarani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa miaka ya ambayo Tumbaku ilikuwa sawa sawa siwezi kukukatalia hizi wilaya zilikuwa na mapato makubwa sana.

Ila kwa sasa ziko hali mbaya sana bahati nzuri tu ni kwamba wilaya hizi huwa hazina historia ya kusumbuliwa njaa kwa sababu zinazalisha chakula cha kutosha.

Pia ndiyo wilaya zenye mifugo wengi sana mkoani Tabora ukilinganisha na igunga na nzega.
Rudi kwenye kudesa upya mkuu,Wilaya zenye mzunguko mkubwa wa Pesa Tabora ni Urambo na Kaliua hizo nyingine zinafuatia,pitia tu takwimu za halmashauri husika uone makusanyo ya Ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahama haizalishi chakula kwa kiwango unachotaka kusema hapa.

80% ya karanga zinazopatikana Kahama zinazalishwa Tabora na soko kubwa la Karanga za Tabora ni kahama.

Zao kubwa kahama inalozalisha ni Mpunga tu sasa utasemaje kuwa wanategemewa na Shinyanga ?

Mahindi unayoyaona sokoni hapo kahama yanatoka Tabora katika wilaya za Uyui, Kaliua na Urambo.

Kimsingi bila Tabora Shinyanga inaweza kuteketea kwa njaa.
Shy inategemea kahama siyo tbr acha uwongo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakazia Hapo,wafabiashara mazao wa kahama wanatoa tabora kasoro labda mpunga .
Kinachonishangaza kuhusu shy,Kuna viwanda,lakini ukipita hata hizo area,hakunaga mishemishe kabisa hata msimu wa pamba,pametulia Kama hawapo,
Ukija khm,msimu viwanda vinaoperate yaani mishemishe kibao,sio mamantilie,bodaboda,magari ya mizigo,maduka,bars,Gest etc
 
Naona kila mdau anapapamba alikozaliwa,kukulia au kuishi huku hisia zikitawala,nilitarajia kukutana na takwimu za kufa mtu.

BTW: Mjadala ni mzuri!

Kuna mdau amegusia suala la uislamu na uswahili au kudumaa kwa miji,hii conspiracy nimeisikia sana kwenye miji iliyokaliwa na waarabu mf Tinde na Bukene kwamba eti wapo conservative na hostile sana kwa wageni kuwekeza (majungu&fitina etc)

Itakuwa conspiracy tu.
 
Soma vizuri comment yangu, mm mwenyewe muislamu, ninachosema tabora kuna umwinyi sana na hii ni kwa sababu ilikuwa kituo na route ya slave trade na umwinyi ndio unachangia uswahili hapo tabora mjini.

Tabora ni nyumbni mm, na nimesoma hapo A level, so maisha ya Tabora mjini, na uswahili uliopo naufahamu sana, lakini ukiondoa Tabora mjini, urambo mjini na kaliua miini, sehemu zingine za tabora watu ni wachapa kazi na ni hazina umwinyi, na ndio maana wafanyabiashara wengi wa tabora ni waha
Unataka kuharibu uzi wa mwenzio,,,hapo tiari ushaingizi udini. Inamaana waislamu ndio tatizo?? Natamani nikutukane but namuogopa Allah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kahama ni habari nyingine, kwa mzunguko wa hela na per capital ni pakubwa kuliko wilaya nyinginza tanzania na pengine baadhi ya mikoa kama singida, rukwa, lindi na shintanga nyenyewe.

Ukiondoa Kahama, kwa ukanda huo, bariadi panaweza kufuatia, napo ni sabahu pamekuwa makao makuu ya mkoa, then Igunga, igunga inakua kwa kasi sana.

Ukuaji wa Nzega ni mdogo sana,
Maswa na Meatu wako nyuma sana, na kunakua taratibu sana,labda lami ya maswa bariadi ikiisha itaweka chachu ya maswa kukua, lakini hata hivyo panahitaji miaka mingi sana, kwa sababu Bariadi itaendelea kuimeza Maswa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabora is nore populated kuliko shibyanga, ukaribu wa ahintanga na mwanza ndio unaoipa shinyanga viwanda, kama pwani inavyopata viwada kwa kuwa karibu na dar

Pop ya tabora mjini ni around 230,000 wakati shinyanga mjinj ni around 160,000
Kwanza utambue kuwa Tabora ni mji mkubwa sana kuulinganisha na Shinyanga tu hivyo population ya mjini ni automatically itakuwa kubwa kulinganisha na Shinyanga.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachanganya madesa sana mkuu.

Tunapoongelea shinyanga na Tabora tunaongelea miji siyo mikoa.

Kahama ipo mkoa wa shinyanga lakini hakuna mtu wa kahama anayeweza kukubalia kuishi shinyanga.Shinyanga mjini ni hovyo kweli.

Ukizungumzia almasi na dhahabu,hizo almasi hazina faida yoyote kwa shinyanga mjini.Kwanza ziko wilaya ya Kishapu.

Dhahabu pia haiifaidishi shinyanga mjini.Dhahabu ipo kahama.

Pia huwezi kulinganisha kahama na Tabora.Kahama ni wilaya,Tabora ni mkoani.
Miundo mbinu Tabora ipo vizuri sana,wala hili sidhani kama tutabishana.Kwa biashara kidogo kahama imechangamka na ina mwingiliano mkubwa kidogo.Sehemu zenye hela kahama sio zenye dhahabu Bali zenye mazao hasa tumbaku,mpunga,na asali.

Shinyanga imani za kichawi ni kubwa pia.Matukio ya jinsi hiyo ni mengi na huenda ni moja ya mikoa hatari katika fani hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…