Shinyanga: Mgombea CHADEMA na wenzake 8 wakamatwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba amesema hadi sasa watu tisa wamekamatwa kwa tuhuma za kutaka kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi (CCM).

Magiligimba alisema jana kuwa miongoni mwa watuhumiwa ni aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Salome Makamba.

Alisema mwanasiasa huyo yupo nje kwa dhamana. Alisema watuhumiwa wengine wanane ni wanaume na kwamba Polisi wanaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika, watawafikisha mahakamani.

Kamanda Magiligimba alisema watuhumiwa hao, walikamatwa kila mmoja kwa wakati wake na katika mazingira yake na kwamba walikamatwa kama wahalifu na si wafuasi wa chama fulani.

Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo, liliwakuta watu wawili ndani ya gari lenye namba za usajili T 729 DFP aina ya Toyota Kluger rangi ya kijivu mali ya Salome.

Kamanda Magiligimba alisema wakati watuhumiwa wakitaka kuchoma nyumba a mbunge mteule huyo akiwa amelala kwenye jengo hilo na ndugu zake.

Alisema, Katambi na wenzake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje na wakaona moto ukiwaka huku pembeni yake kukiwa na dumu lenye mafuta ya petroli na kuanza kuzima moto huo.

Magiligimba alisema baada ya kuzima moto huo, waliona gari likipita barabara ya lami ya kutoka Shinyanga kwenda Mwanza na ndipo walipolifuatilia. Alisema watu hao walipogundua wanafuatiliwa, waliamua kuingia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na kuegesha gari hilo.

Alisema baada ya msako, ilibainika kuwa watu hao ndiyo waliokuwa eneo la tukio na baada ya mahojiano walikiri kuwa gari hilo mmiliki wake ni Salome, aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Chadema.

Magiligimba alisema dereva ambaye ni mdogo wake Salome, aliyefahamika kwa jina la Timoth Makamba alikimbia. Lakini msako uliofanywa na jeshi hilo nyumbani kwa Salome, ulifanikiwa kuwakamata watu wawili, Justine Owesiga (35) na Gibson Mkongwa (31).
 
Back
Top Bottom