Shinyanga: Mfanyabiashara aidai Vodacom Tsh. Bilioni 10 kwa madai ya kuvujisha Taarifa zake Binafsi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Mfanyabiashara kutoka Shinyanga amefungua kesi dhidi ya Vodacom Tanzania Plc na kudai Shilingi bilioni 10, akidai kwamba kampuni hiyo ilitoa taarifa zake binafsi kwa chatbot ya akili bandia (AI) bila idhini.

Katika kesi ya kihistoria iliyowasilishwa Mahakama Kuu ya Shinyanga, Sayida Masanja anataka kampuni hiyo ilipe kiasi hicho kutokana na "kupoteza faragha kwa kiwango kikubwa" kilichosababishwa na madai ya kutokuwa na ulinzi wa data yake binafsi.

Amedai kuwa Vodacom iliruhusu na kurahisisha ufikiaji usioidhinishwa wa watu wa tatu(Third part). Masanja amesema mwezi wa Februari na Machi mwaka 2023, aligundua taarifa zake binafsi kwenye ChatGPT.

Taarifa inayodaiwa kushirikishwa ni pamoja na simu za kuingia na kutoka, IMEI, IMSI, kitambulisho chake cha SIM, na Taarifa Zinazoweza Kutambulika (PIIs). Pia anawalaumu kampuni hiyo kwa kushirikisha maeneo mbalimbali aliyopatikana.

Amekusanya nakala za taarifa inayodaiwa kushirikishwa kama sehemu ya ushahidi wake mahakamani.

Vodacom yakanusha madai
Vodacom imepuuza madai hayo. Kampuni hiyo imeeleza pingamizi la awali na kuomba mahakama kuitupa kesi hiyo na kuamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi kwa kosa la kufunguliwa Mahakama Kuu badala ya mahakama ya mkazi au mahakama za wilaya, kinyume na Kifungu cha 13 cha Sheria ya Taratibu za Kiraia.

Kifungu hicho cha sheria kinaelekeza kuwa kesi yoyote inapaswa kufunguliwa katika mahakama ya kiwango cha chini kinachostahili kuishughulikia, ikiripoti mahakama ya mkazi au mahakama ya wilaya.

Kupitia Huduma za Sheria za Afrika Mashariki wa Dentons EALC, Vodacom ilisisitiza kuwa haikuwajibika kwa kuruhusu ufikiaji wa mtu wa tatu au mtu yeyote asiyeidhinishwa kwenye taarifa za mlalamikaji.

Pia imekanusha kuwa inahusika na ChatGPT au kuisaidia Akili Bandia kwa njia yoyote.
 
Nani anawapaga namba zetu hawa kina Tamisemi, Tatu mzuka nasijui Mchezo Blaaa blaaa... wanasheria rukeni na hizo tu maana hii mitando ya simu inatuona sisi kama ma zwazwaa na ndio maana unashangaa mtu umeongea nae kwamba akutumie namba umtumie hela apo apo inaingia meseji ya tapeli kuwa iyo hela itume kwenye namba Hii... kajulia wapi natuma hela kama si wizi mtupu.
 
Nani anawapaga namba zetu hawa kina Tamisemi, Tatu mzuka nasijui Mchezo Blaaa blaaa... wanasheria rukeni na hizo tu maana hii mitando ya simu inatuona sisi kama ma zwazwaa na ndio maana unashangaa mtu umeongea nae kwamba akutumie namba umtumie hela apo apo inaingia meseji ya iyo hela itume kwenye namba Hii... wizi mtupu.
yani bongoo hii mitandao ikiamua kushtakiwa ile serious AISEE ITAFILISIKA..!! jamaa wanazingua sanaa haya makampuni ya kamari yanauziwa sana namba zetu
 
yani bongoo hii mitandao ikiamua kushtakiwa ile serious AISEE ITAFILISIKA..!! jamaa wanazingua sanaa haya makampuni ya kamari yanauziwa sana namba zetu
Daah yaani imekuwa kero kila baada ya mda meseji ya kamari,mimi siku hizi meseji zimepungua baada ya kuanza kuziblock.
 
mimi kuna siku nikapigiwa simu kwenye namba ya Till ya M Pesa na kutaka kupigwa hela.

sasa nikajiuliza namba yangu imepatikanaje wakati unapomurushia hela mtu inaenda code peke yake na sio namba ya laini husika ?

nikawatafuta Voda ila stories zikawa nyingi ohh mtafute Manager wa eneo husika,mara sijui hili na lile …

niliwambia kitu kimoja tu kwamba nikipigwa hata mia mtanieleza system yenu inaingiliwa vipi mpaka mtu anapata namba ya Till ya M Pesa na taarifa zangu zote kwa ujumla la sivyo tutakula sahani moja.

sijawahi kuona namba yoyote inaingia kwenye hii simu tokea kipindi hicho.

Vodacom wana michezo michafu sana halafu ni kama tuko uchi yaani.

unajua hata Polisi akitaka taarifa zako anatumiwa bila hata kufuata utaratibu wowote ?

Voda mimi nilishaacha kuwafanya kua laini yangu official kwa sababu usalama ni 0
 
nasema voda wana afadhalii kuna hawa AIRTEL NA HALOTEL aisee ni weziii wa kutupwaaa... ukimtumia tu mtu hel au mkiwasiliana kuhusiana na masuala ya helaa bhasi tegemea msg ya MATAPELI ITAINGIA au utapigiwaaa yani wanashirikiana sana na matapeli.
 
Back
Top Bottom