PreGE2025 Shinyanga: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

PreGE2025 Shinyanga: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975

WanaJF,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Shinyanga. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

shinyanga.jpg

Mkoa wa Shinyanga uko Kanda ya Ziwa katika Tanzania na ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji, pamoja na madini, hasa almasi. Mkoa huu una historia ya utajiri wa madini, hususan kupitia mgodi maarufu wa almasi wa Mwadui.

Idadi ya Watu​

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Shinyanga ni 2,241,299; wanaume 1,102,879 na wanawake 1,138,420, na ina wilaya 5 ambazo ni Shinyanga Manispaa, Shinyanga Vijijini, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Ushetu

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi​

Mkoa wa Shinyanga una jumla ya majimbo 6 ya uchaguzi:
  • Jimbo la Shinyanga Mjini
  • Jimbo la Solwa
  • Jimbo la Kahama Mjini
  • Jimbo la Msalala
  • Jimbo la Kishapu
  • Jimbo la Ushetu
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Mkoa wa Shinyanga ulishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa katika maeneo mengi ya mkoa huo.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi zaidi kulinganisha na wapinzani wake.

Katika uchaguzi wa Ubunge, wagombea wengi wa CCM walipita bila kupingwa na wengine kushinda kwa kura nyingi dhidi ya wapinzani wao huku wakiwa na ushindi wa 100%.

Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kata nyingi. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu kutokuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi.

Updates

December, 2024

January
February
March
May
June
July
August
September
October

Kamati Kuu CCM yatangaza rasmi majina ya watia nia Ubunge 2025​

  • MKOA WA SHINYANGA

    Jimbo la Shinyanga Mjini

    1) Stephen Julius MASELE
    2) Patrobas Paschal KATAMBI
    3) Abubakar Gulamhafiz MUKADAM
    4) Eustard Athanace NGATALE
    5) Hassan Athuman FATIU
    6) Hosea Muza KARUME
    7) Paul Joseph BLANDY

    Jimbo la Kishapu
    1) Lucy Thomas MAYENGA
    2) Boniphace Nyangindu BUTONDO
    3) Bonda William NKINGA
    4) Dotto Salum KWIGEMA
    5) George Martine JIMISHA
    6) Madaha Mayega CHABBA
    7) John Ngano NHYAMAH

    Jimbo la Solwa
    1) Ahmed Ally SALUM
    2) Sosthenes Julius KATWALE
    3) Selemani Emmanuel CHOKALA
    4) Zinguji Mayala MACHWELE
    5) Leonard Nduta LUKANYA
    6) Alphistone Michael BUSHI
    7) Constantine Joseph BUDAGA

    Jimbo la Itwangi
    1) Azza Hillal HAMAD
    2) Chrispine Myeke SIMONI
    3) Sebastian Pastory MALUNDE
    4) Fred Romanus SANGA
    5) John Elias NTALIMBO
    6) Christian Misobi BUDOYA
    7) Helena Daudi MBULI
    8) Anna James NG’WAGI

    Jimbo la Kahama Mjini
    1) Sweetbert Charles NKUBA
    2) Francis Fikili MIHAYO
    3) Jumanne Kibela KISHIMBA
    4) James Daudi LEMBELI
    5) David Anyandwile KILALA
    6) Juliana Kajala PALLANGYO
    7) Benjamini Lukubha NGAYIWA

    Jimbo la Ushetu
    1) Emmanuel Peter CHEREHANI
    2) Valelia Wilson MWAMPASHE
    3) Mussa Shilanga MISUNGWI
    4) Machibya Mwambilija DOFU

    Jimbo la Msalala
    1)Mabula J. MAGANGILA
    2) Ezekiel MAIGE
    3) Ambrose N. NAKALE
    4) Ramadhani SHIGANZA
    5) Edson Simba MASONDOLE
    6) Simon James LUFEGA
 
WanaJF,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Shinyanga. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Shinyanga uko Kanda ya Ziwa katika Tanzania na ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji, pamoja na madini, hasa almasi. Mkoa huu una historia ya utajiri wa madini, hususan kupitia mgodi maarufu wa almasi wa Mwadui.

Idadi ya Watu​

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Shinyanga ni 2,241,299; wanaume 1,102,879 na wanawake 1,138,420, na ina wilaya 5 ambazo ni Shinyanga Manispaa, Shinyanga Vijijini, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, Ushetu

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi​

Mkoa wa Shinyanga una jumla ya majimbo 6 ya uchaguzi:
  • Jimbo la Shinyanga Mjini
  • Jimbo la Solwa
  • Jimbo la Kahama Mjini
  • Jimbo la Msalala
  • Jimbo la Kishapu
  • Jimbo la Ushetu
HALI YA UCHAGUZI MKUU 2020

Mkoa wa Shinyanga ulishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa katika maeneo mengi ya mkoa huo.

Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi zaidi kulinganisha na wapinzani wake.

Katika uchaguzi wa Ubunge, wagombea wengi wa CCM walipita bila kupingwa na wengine kushinda kwa kura nyingi dhidi ya wapinzani wao huku wakiwa na ushindi wa 100%.

Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kata nyingi. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu kutokuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi.

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
Sasa mod nini maana ya huu uzi kama huweki habari za mkoa husika???? Kwa mfano hapo Shinyanga mwenyekiti wa Chadema kafukuzwa mbona hujaaupdate??
 
Back
Top Bottom