Shinyanga: Fisi wafukua maiti zilizozikwa kizembe na Manispaa, wananchi wang'aka...

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Wakazi wa manispaa ya Shinyanga wamepeleka malalamiko yao kwa serikali baada ya manispaa hiyo kushindwa kuzika vizuri miili ya marehemu kwenye makaburi yanayomilikiwa na manispaa hiyo ambayo uzikwa watu waliokosa ndugu.

Hali hiyo usababisha eneo hilo la makaburi kunuka na kutapakaa kwa viungo vya binadamu jambo ambalo ni hatari kwa afya za wakazi wa eneo hilo.

Kwa kawaida kaburi inabidi liwe refu ili hata mwili ukifukiwa isiwe rahisi kwa wanyama kuufikia,lakini makaburi hayo huwa mafupi kiasi kwamba hata mijibwa koko inaweza kufukua.

Picha;

fisi2.jpg

fisi1.jpg

Baadhi ya mifupa ya maiti iliyokusanywa eneo la makaburi
fisi.jpg

Mkono wa maiti uliokutwa kwenye uso wa ardhi eneo la makaburi
 
View attachment 354113

View attachment 354114
Baadhi ya mifupa ya maiti iliyokusanywa eneo la makaburi
View attachment 354115
Mkono wa maiti uliokutwa kwenye uso wa ardhi eneo la makaburi

Hatari.
 
Jamani sijui tukoje, kila sehemu ni uzembe tu mweeee, hapo utaambiwa kuwazika watu watano zimetumika milioni kumi
 
Nako wanasubiri hadi Mh. Rais atolee tamko, daah Baba Magufuli una kazi sana.
 
Maiti ina thamani sana kwa ndugu,jamaa na marafiki, tofauti na hapo kuzikwa vizuri nadra sana. Sasa halmashauri inashindwaje kuzika miili iliyokosa ndugu vyema? Hii ni dharau kubwa sana kwa binadamu.
 
Nako wanasubiri hadi Mh. Rais atolee tamko, daah Baba Magufuli una kazi sana.
Hahahaah, mkuu sasa kila kitu sio lazima Rais, ngazi ya mkoa,wilaya,kata mtaa,kijiji,kitongoji kuna viongozi kibao wanakula mshahara wa bure, hawa ndio wa kuwaadabisha.
 
Shinyanga bana, na hii ipo hata mikoa mingine tofauti ni kwamba mikoa mingine ina uchache wa fisi au hamna kabisa.
 
Mengine muwe mnayaacha yapite, mengine mazindiko,

Wamezika kizembe LOL
 
Shinyanga bana, na hii ipo hata mikoa mingine tofauti ni kwamba mikoa mingine ina uchache wa fisi au hamna kabisa.
Mkuu, mkoa wetu hakuna fisi kabisa labda kama wale wa kichawi ila nako sijawahi kusikia. Ila hawa wa Shinyanga ni kiboko sana sio kwa njaa hiyo.
 
Back
Top Bottom