Shinikizo ladamu na kupoteza uono(vission) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shinikizo ladamu na kupoteza uono(vission)

Discussion in 'JF Doctor' started by eedoh05, Oct 25, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana kwa ushauri wenu juu ya tatizo la macho. Leo swali langu ni hili: Je ni kweli kwamba Hbp inaweza kusababisha mtu akapoteza uwezo wa kuona(vission)? Je, kama jibu ni ndiyo, nini cha kufanya ili ku-recover?
   
 2. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  naenda waita wahusika nakuja!
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Shinikizo la damu (High Blood Pressure) inaweza sababisha kupoteza uono (vision). Kwa kifupi katika HBP mishipa ya damu mwilini hujibana (vasoconstriction) na hivyo kuhitaji moyo kufanya kazi ya ziada kuweza kusukuma damu kupita katika mishipa hiyo. Na hilo linaweza kupelekea mishipa hiyo kupasuka (kwenye ubongo kusababisha kiharusi au stroke) sehemu fulani fulani za mwili.

  HBP inaweza kusababisha upotevu wa uono kwa njia zifuatazo:

  - Kubana kwa mishipa ya damu ndani ya jicho (retina) hivyo kusababisha kukua kwa presha kwenye retinal blood vessels na hivyo kusababisha kupungua uono. Pia mishipa hiyo inaweza kupasuka pasuka (cumulative effect) na hivyo kupoteza uono taratibu mpaka kupofuka. Hili tatizo linaitwa Hypertensive Retinopathy.
  - Kutokana na mabadiliko ya kimishipa ndani ya jicho, hii inaweza kusababisha optic nerve kuvimba na hivyo kushindwa kutuma message kwenye ubongo na kusababisha kutoona.

  Matibabu/kinga kubwa ya Hypertensive retinopathy ni kucontrol tu HBP kwa njia mbali mbali ie. kutumia dawa, diet, na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu HBP. Pia kufanya check up ya macho mara kwa mara unapoenda clinic ya HBP kwa kutumia kifaa kinaitwa (Retinoscope). Daktari akikuangalia jicho kwa hiki kifaa anaona hayo mabadiliko na kukushauri jinsi ya kuyakabili.

  NB: Tafadhali omba daktari akucheki kwa Retinoscope kila unapoenda kwenye clinic ya HBP au Kisukari. Ni haki yako.
   
 4. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ahsante sana dr Riwa. Nitazingatia ushauri wako. Kwa ufupi nilianza kuvaa miwani ya macho 1985; ingawa tatizo la kutoona mbali nililihisi mwaka 1982. Nimekuwa nikibadilisha lensi kila baada ya miaka 5 au 6 hivi. Na mwaka 2006 nikagunduliwa kuwa na hbp. Mwaka 205 nikapewa miwani ambayo ni double focus. Iliharibu uwezo wa kuona karibu, ilinibidi kuivua nisomapo. Kabla ya kupata miwwani ya aina hii nilikuwa nasoma tu pasipokuvua miwani.

  Mwaka huu 2011 kuanzia mwezi wa 8 nimeona uono wangu umepungua ghafla. Naona vitu kama vina ugiza giza fulani iwe mbali ama ni somapo.
   
Loading...