Shinikizo la juu la damu (High blood Pressure) Fahamu chanzo, kinga na tiba ya tatizo hili

Asanteni wakuu kwa michango hii,nadhani anahitaji kupata ushauri wa daktari wake juu ya kubadilishiwa dawa na si kuacha.
Binafsi nilitaka nijiunge na kampuni moja wanauza tiba mbadala na walikuwa wakituaminisha kuwa wateja wetu wanaweza kuondokana na matumizi ya dawa zunazowaletea madhara.
 
Nimeulizwa swali hili na mtu anayetumia dawa za pressure na lakini zinamfanya awe na upungufu wa nguvu za kiume.
Je kuna tiba mbadala isiyoleta madhara hayo?
Tafadhali tufafanulie kwanza.

Upungufu nguvu za kiume ni nini hasa?

1. Je, ni kukosa hamu ya kujamiana?
2. Je ni kuwa na hamu ya kujamiana lkn husimamishi hata iweje?
3. Je ni kuwa na hamu ya kufanya, jnasimamisha na una weza kufanya lkn kwa muda mfupi tu umemaliza?
4. Je ni kuwa na hamu, kusimamisha vizuri lakini ukafanya kwa muda mrefu bila kufika mwisho?
5. Au ni kufanya yote hayo lkn unakojoa kijiko hakijai?

Tuanzie hapa kwanza, maana hii dhana siielewi kabisa.
 
Nimeulizwa swali hili na mtu anayetumia dawa za pressure na lakini zinamfanya awe na upungufu wa nguvu za kiume.
Je kuna tiba mbadala isiyoleta madhara hayo?
Usijaribu Usijaribu Usijaribu.
Tukumbuke ya Loliondo na tuangalie watu wanavyteseka.Kuna watu wanajidai wanaunga mifupa mwisho watu wanaishia kukatwa miguu.
Hizi tiba mbadala tuwaachie kina mama wenye mashetani
 
Punguza chumvi Kwa asilimia80,punguza wanga sana,Fanya mazoezi hata ya kutembea asubuhi na jioni,tafuna vitunguu saumu sana asubuhi kabla hujaamka tafuna hata punje kumi na maji pia jion fanya hivyo hivyo kwa miezi mitatu ,achana na nyama nyekundu !!! Nimefanya hayo nimeona nafuu kubwa sana
hapo kwenye kutafuna kabla ya kuamka vpi mkuu (i mean unaweza kufanya hivo ukiwa usingizini)
 
Dawa za pressure haitakiwi kuacha bila kumuona mtaalamu. Inaweza sababisha pressure kupanda kupita kiasi na kifo. Pia dawa za mitishamba nyingi ni utapeli. Sishauri aache na kuhamia huko.

Ila akizingatia mazoezi na ulaji mzuri inaweza msaidia kupunguza dawa.
 
Aache ujinga.Tiba mbadala ni kama kikombe cha babu Loliondo.

Kama uume hausimami basi amtaarifu daktari wake ambadilishie dawa za pressure.Pia afanye mazoezi na kupunguza uzito.Kama anafikiria kuacha dawa za presha anunue mashine ya kupima presha awe anajipima nyumbani aone mwenendo wa presha yake.
 
Asanteni wakuu kwa michango hii,nadhani anahitaji kupata ushauri wa daktari wake juu ya kubadilishiwa dawa na si kuacha.
Binafsi nilitaka nijiunge na kampuni moja wanauza tiba mbadala na walikuwa wakituaminisha kuwa wateja wetu wanaweza kuondokana na matumizi ya dawa zunazowaletea madhara.
tiba mbadala atumie kama suppliiments kwa uzoefu wangu sioni kama zitamfaa sana kuna dawa nzuri za prssure zisizo na shida hiyo ni kuongea tu na daktari atambadirishia dose.
 
Wasalaam,

Mama yangu ni mgonjwa anasumbuliwa na pressure, lakini pia anatatizo la macho, yaani wakati mwingine kichwa humuuma.

Hivi karibuni amekuwa akiumwa kichwa sana usiku wa manane akiwa amelala, kichwa humuuma sana mpk hukosa usingizi na kuamka na kukaa.

Anatumia mara moja moja dawa za pressure si kila siku.

Sasa tunashindwa kuelewa kuuma huku kwa kichwa ni kwa sababu ya tatizo la pressure au macho?

Je watu wanaogua tatizo la pressure, ni namna gani ataweza kuihimili pressure?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wenye uelewa juu ya hili tatizo
 
pole sana kwa kuuguliwa, mpe pole pia mama . ningekushauri aende akaonane na Dr. Zipo baadhi ya dawa za pressure ambazo baadhi ya side effects zake ni maumivu ya kichwa so Dr ataona kama ipo haja ya kubadirisha dawa au kupunguza dose. lakini pia anaweza kufanya baadhi ya vipimo ili kujiridhisha baadhi ya maradhi yanayoweza kusababisha kichwa kuuma. Pamoja na kusubiri ushauri humu lakini chukua pia hatua za kwenda kwa Dr.
 
tiba nzuri ya pressure ni kubadilisha kabisa mfumo wa maisha....kuanzia vyakula hadi mazingira yanayomzunguka ktk shughuli zake za kila siku.

kuumwa macho pia kunaweza kusababisha kuumwa kwa kichwa....na pressure inaweza kuleta matatizo ktk macho vilevile.
 
pole sana kwa kuuguliwa, mpe pole pia mama . ningekushauri aende akaonane na Dr. Zipo baadhi ya dawa za pressure ambazo baadhi ya side effects zake ni maumivu ya kichwa so Dr ataona kama ipo haja ya kubadirisha dawa au kupunguza dose. lakini pia anaweza kufanya baadhi ya vipimo ili kujiridhisha baadhi ya maradhi yanayoweza kusababisha kichwa kuuma. Pamoja na kusubiri ushauri humu lakini chukua pia hatua za kwenda kwa Dr.

Ahsante sana mkuu
 
Mama yetu ana umri gani?Pressure ni ugonjwa unaohitaji dawa kila siku na kuwa monitored kila mara. Ni silent killer.
Ukianza dawa huwezi ukawa unatumia unaacha. Ni lazima utumie dawa maisha yako yote.
 
Ahsante sana mkuu
Mama aendelee kumeza dawa za presha na kichwa kitapona ninatatizo km hilo nibadilisha madr wa macho mpaka basi mmoja ndio akaniambia ni presha baada ya kumeza dawa nimepona kichwa vizuri akabadilisha mfumo wa maisha apunguze chumvi
 
Mama yetu ana umri gani?Pressure ni ugonjwa unaohitaji dawa kila siku na kuwa monitored kila mara. Ni silent killer.
Ukianza dawa huwezi ukawa unatumia unaacha. Ni lazima utumie dawa maisha yako yote.
Haana mimi ninayo bidhaa ukitumia miezi mitatu mfululizo basi pressure kwisha
 
Bidhaa?
Wacha utani kwenye masuala ya afya. Hamna dawa ambayo ni approved duniani kote inayoweza kutibu presha kwa miezi 3.
 
Natumia hii dose ila huwa nameza wakati wa usiku inasaidia sana kweli pressure inashuka kuelekea normal.
Mkuu hii dose ni ya kweli au??

Manake ss hv nina mwaka na kidogo natumia amlodipine lakin sioni chochote haishuki wala nini, natamani kweli kutotumia dawa za presha lakini sina jinsi
 
Mr Miller,
Duuh hii kweli au?? Manake ndizo ninazotumia kila siku ya Mungu ila sasa kweli naona pressure haishuki, natamani kweli kurudi maisha ya kutotumia dawa daah
 
Pole sana mkuu,hata mimi nilikuwa na hilo tatizo na nilichofanya ni kusimama kunywa pombe for 6 month,na kuanza mazoezi 1hr * 4/7 days ,pia nilikuwa nameza tembe 3 za vitunguu swaumu kila siku for 3 month,nikaacha matumizi ya chumvi nyingi,na vilevile nikapunguza wanga na sukari kwa asilimia 70%,sasa hivi preassure yangu ipo 122/85 many times ,nakunywa beer moderate at least 2 days a week during weekends.

Hongera mkuu, hapa ulikuwa bado hujaaanza kutumia dawa au ulianza dawa kisha ukaziacha??
 
Mkuu hii dose ni ya kweli au??

Manake ss hv nina mwaka na kidogo natumia amlodipine lakin sioni chochote haishuki wala nini, natamani kweli kutotumia dawa za presha lakini sina jinsi
amlodipine ni dawa nzuri sana kwa presha btw ushawahi andikiwa (nifidepine+clonidine) au carvedoril na dokta? jaribu vitunguu swaumu bila kuacha dawa za presha uone kama una mabadiliko zaidi kuacha dawa ghafla za presha sio uamzi mzuri.
 
Back
Top Bottom