SHINDANO LA UBUNIFU WA NEMBO (LOGO)

Mar 22, 2016
3
1
Legal Services Facility (LSF) ni Kampuni inayotoa ruzuku kwa mashirika yanayotoa huduma za msaada wa kisheria Tanzania, ambayo inafadhiliwa na Serikali ya Denmark kupitia Shirika la Misaada la Danida na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la DFID. Ni Kampuni ambayo inakuza na kusadia mbinu za kibunifu katika kupata msaada wa kisheria. Maadili ya msingi ya LSF ni Haki za Binadamu, uwazi na uwajibikaji, ushirikiano na ubia, usawa na uendelevu. LSF inataka kutengeneza nembo (Logo) mpya ambayo itakwenda sambamba na muelekeo mpya wa Kampuni, wenye Kauli mbiu ya “Haki ni kila siku kwa matatizo ya kila siku."

LSF imeandaa Shindano la kutengeneza Logo yake mpya kwa watu wote wenye vipaji na uwezo wa ubunifu huo,

MOTO

Haki ni kila siku kwa matatizo ya kila siku “Everyday Justice for Everyday problems”

MAONO

Maono ya LSF ni kuhakikisha kuwa raia na jamii yote ya Tanzania inapata Haki

DHAMIRA

Kukuza na kulinda Haki za Binadamu kupitia uwezeshaji wa Kisheria, kuongeza upatikanaji wa huduma za Kisheria kwa masikini na wanajamii waishio katika hali hatarishi hususani wanawake

NANI ANAWEZA KUSHIRIKI

Mtu yeyote mbunifu bila kujali umri wake, elimu yake nk. anaweza kushiriki shindano hili, pia wanafunzi wanaombwa kushiriki.



NAMNA YA KUSHIRIKI

Mshiriki anatakiwa kutuma kazi yake ambayo ataambatanisha na maelezo (Maneno 200) kwa lugha ya Kiingereza yanayoeleza ubunifu, logo yake sambamba na Kauli Mbiu yetu “ Haki ni kila siku kwa matatizo ya kila siku”

VIGEZO VYA KUSHRIKI

· Kazi inatakiwa iwe na ubunifu wa Kipekee

· Kazi inatakiwa isiwe na uhusiano na kazi yeyeote iliyokwisha fanywa

· Kazi ya ubunifu inatakiwa kuwa ya mshiriki mwenyewe na siyo ya mtu mwingine

· Kazi (ubunifu) uwe katika fomati ya vekta

· Iwe rahisi kuitambua na kuikumbuka

· Ubunifu uwasilishe maono na dhamira ya LSF

ZAWADI KWA WASHINDI

Katika Shindano hili mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 5, mshindi wa pili milioni 3 na mshindi wa tatu milioni 1. Logo itakayoshinda itakuwa mali ya LSF na itatumiwa katika machapisho na shughuli zote za LSF.

JINSI YA KUTUMA KAZI

Ubunifu/ Kazi ihifadhiwe kwenye CD na kuwekwa katika Bahasha, na iletwe kwa njia ya mkono au itumwe kwa Barua pepe; logo@lsftz.org na kwa njia ya Posta katika anuani ifuatayo

Chief Executive Officer

Legal Services Facility

Bima Street, Nyati Rd, Mikocheni B

P.O.Box 31480

Dar es Salaam, Tanzania

Tel: 0222 781061


Mwisho wa kupokea ubunifu huo ni Jumanne, 29 Machi, 2016, saa 10:00 Jioni
 

Attachments

  • SHINDANO LA UBUNIFU WA NEMBO.pdf
    468.1 KB · Views: 120
Back
Top Bottom