Shilole na ubalozi wa Condom

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,962
Habari zenu wakuu.

Tasnia ya muziki inakuwa TZ na namna ya wasanii wetu kuingiza kipato inapanuka zaidi, kwani kwa sasa makampuni yameweza kuwaamini wasanii kuwa wanaweza wakawa ni njia mojawapo ya kuwatangazia bidhaa zao.

Leo katika pitapita zangu mitandaoni nimekutana na Shilole akiwa na ubalozi wa Kondom.

Hii pia inaonyesha kuwa makampuni hayamng'ang'anii msanii mmoja kuwa balozi kama baadhi ya watu walivyokuwa wanasema.
 
kwa hiyo itabidi na yeye atangazie uma kuwa natumia?

ila njia thabit ya kuzuia maambukizi ni kuachana na ngono sio matumizi ya hizo kinga.

matangazo yenyewe ya hizo kinga yanashawishi ngono kuliko kukataza ngono.
 
Sio km ubalozi wa bia/ soda mpk aonekane anakunywa ili wajue msisimko la ladha yake

au
mitindo ya mavazi mpaka avae,
Tuone kama kweli mavazi ni mazuri

au ubalozi wa king'amuzi mpk uwe nacho nyumbani uonekane unakitumia watu wajue ubora na faida zake

Au kama ubalozi wa pempaz amvalishe mtoto kuona ubora na jinsi inavyovaliwa.

Au ubalozi wa pikipiki watu waone unavyoipanda na kuiendesha.

Matangazo katika ubalozi wake huu anaweza kuishika tu mkononi na kuwahamasisha watu watumie km vile matangazo ya vazi la wanawake analovaa ndani siku zake za mwezi.
Ni simple tu, yani anashika mkononi na kusifia ubora wake yani zimethibitishwa na tbs

NB:
Ubalozi/ matangazo mengine yatangazwe kuzingatia jinsia, sababu inaweza kuleta picha mbaya kwa jamii
Ingependeza zaidi balozi wa sekta hiyo ikawa ni mwanaume kwa utamaduni wetu
 
kwa hiyo itabidi na yeye atangazie uma kuwa natumia?

ila njia thabit ya kuzuia maambukizi ni kuachana na ngono sio matumizi ya hizo kinga.

matangazo yenyewe ya hizo kinga yanashawishi ngono kuliko kukataza ngono.
Sasa utaachana aje na ngono uchukue kadi ya chaputa au
 
Hongera yake maana hadi wameamua kumpa ubalozi wa Condom maana yake yeye mwenyewe hayumo kwenye list mkonga wa taifa.
 
Back
Top Bottom