Shilole atamani kuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, aja na mikakati

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Muimbaji Shilole amezungumza na Ayo TV pamoja na millardayo.com ambapo amesema kuwa anatamani sana siku moja kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Igunga mahali ambapo ndipo alipotokea, Shishi amesema kuwa anatamani kuiongoza Igunga hata kama kwa nafasi ya Udiwani ili aisaidie na kuiendeleza kwenye mambo mengi.

Shilole amekiri kwamba yeye ndiye mtu aliyeifanya Igunga ikajulikana hivyo ataweza pia kuifanya Igunga ikaendelea kiuchumi na hata kuitangaza zaidi kupitia jina lake.
 
Ajiandae 2020 agombee udiwani.... anajisemesha ili ateuliwe tu from nowhere.

Mwenzie alipambana hakupata bure.
 
Muimbaji Shilole amezungumza na Ayo TV pamoja na millardayo.com ambapo amesema kuwa anatamani sana siku moja kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Igunga mahali ambapo ndipo alipotokea, Shishi amesema kuwa anatamani kuiongoza Igunga hata kama kwa nafasi ya Udiwani ili aisaidie na kuiendeleza kwenye mambo mengi.

Shilole amekiri kwamba yeye ndiye mtu aliyeifanya Igunga ikajulikana hivyo ataweza pia kuifanya Igunga ikaendelea kiuchumi na hata kuitangaza zaidi kupitia jina lake.
Ilo jambo ni la heri ,raisi wetu askie klio chako akupe uongoz ,ww unafaa sana,ni mtu mtulivu,usiye na makuu ,mpenda watu,mpenda amani,mtu wa watu,unaye jiheshmu sana kwa kutokua na kashfa mtaan,wala kutojiusisha na ujinga wa kutembea na wanaume kla kona,ww ni msanii wa kuigwa na jamii .............
 
Kwani hawezi kuisaidia hiyo Igunga ikaendelea kiuchumi (kama anavyodai) bila ya yeye kua mkuu wa hiyo wilaya?

Nauliza tu!
 
Viongozi wanapaswa kuwa ni wetu wenye hekima,busara,maono maadili na elimu ya kutosha..... lakini pia ni lazima wawe na background nzuri....sio mtu aliyewahi kuwa muhuni au kuishi maisha ya kihuni
 
mwambieni ajirahisi na amchekeee chekeee jiwe tuu, mambo yatakwenda!!
 
Naona tangu mamdogo apate kile cheo,wasanii wanawehuka tu.
Akamuulize mwenzie alifikaje pale ajifunze na yeye
 
Muimbaji Shilole amezungumza na Ayo TV pamoja na millardayo.com ambapo amesema kuwa anatamani sana siku moja kuteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Igunga mahali ambapo ndipo alipotokea, Shishi amesema kuwa anatamani kuiongoza Igunga hata kama kwa nafasi ya Udiwani ili aisaidie na kuiendeleza kwenye mambo mengi.

Shilole amekiri kwamba yeye ndiye mtu aliyeifanya Igunga ikajulikana hivyo ataweza pia kuifanya Igunga ikaendelea kiuchumi na hata kuitangaza zaidi kupitia jina lake.

Kujiamini ni suala muhimu sana katika maisha. Kama anaona anaweza arudi Igunga kuonesha uwezo na dhamira yake katika kuhudumia WanaIgunga. Wao ndio watambeba.
 
Back
Top Bottom