Shilingi kushuka thamani na hali mbaya ya uchumi wetu: Sababu ni nini na nini kifanyike?

Zitto hata aweke michoro,ameshapoteza credibility kwa uongo wake
Zitto ni mkweli lkn ukiwa na ushabiki wa kijinga wa kisiasa lazima you'll lose touch with reality and you won't understand him.
 
Sidhani naona mwendo ni kinyume, dar leo naona parking fees wanakusanya TARURA, ukiangalia logic hamna zaidi yakuwa wameanzisha organisation mpya na pesa hawana, kwa hiyo halmashauri na wafanya biashara wamepigwa mswaki na zero, leo kuna mpango wa kuuwa clearing and forwarding companies zote na NASACO mpya inakuja(tangazo la gazeti limetoka) on and on siyo tunarudi tumerudi, tena only 3 years imeerase mafanikio ya karibu miaka 40 ya mageuzi, subiri utaona watanzania nao wanahama nchi kama zamani (ubaharia wa le mutuz) au kama waethiopia
 
Tweet ya Zitto hii:

Huu Ndio mwenendo wa shs ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani na kulinganisha na nchi zinazotuzunguka za Kenya, Rwanda na Uganda. Mnaona nini?





6:22 AM - 26 Feb 2019
Pole hutapata wachangiaji humu umekosea hukumtaja tundu lissu au mbowe
 
Hata huko Iran kuna afadhali, wao ni development country inakaribia third world, tz tuna a nini? Hata bei ya mafuta na gas inatoka huko huko USA, halafu unakuwa na mdomo mrefu kuwaita mabeberu, kwetu pemba Beberu maana yake kidume, kwa hio watanzania mtakuwa nani nyie,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatutakiwi kusubiri kuona, inabidi tupinge. Tukiwaachia hawa watu wafanye wanavyoona wao tutasahau kama kuna nchi inaitwa Tanzania.
 
Ninakumbuka enzi za US$1 kuwa sawa na Tsh5. Huu ndiyo mwanzo was jina Daladala yaani nauli ni 1US$.

Kweli? Siamini! Sio $=Tsh 7? Iliwahi kuwa Tsh5? Hapana.

Hiyo Dalla ilipachikwa tu kama jina kwa hiyo sarafu ya Tsh5; lakini kihalisi haukuwa $1=Tsh 5

. Tunaweza kwenda 'archive' kutafuta usahihi wa hili!
 
Hatutakiwi kusubiri kuona, inabidi tupinge. Tukiwaachia hawa watu wafanye wanavyoona wao tutasahau kama kuna nchi inaitwa Tanzania.

Sasa tumekuwa kichekesho: Ili shillingi yetu isionekane inadhoofika, dawa ni kufungia gazeti linalochochea wananchi wasiipende serikali yao kwa sababu ya pesa kushuka thamani!

Wakati mwingine unaweza ukadhani hawa watu kichwani hazimo kabisa!

Na ukimsoma 'Bepari la Bariadi hapo #7, ndipo utakapoelewa tunakoelekea kama nchi!
 
Ndugu zangu kwa kweli inasikitisha sana kuona shillingi ya Kitanzania inavyoporomoka dhidi ya dollar ya kamarekani na sarafu ya nchi zingine. Kwa kweli ni aibu sana na sijui kuna nini hali kutokea hivi. Athari zake zinajulikana sana kwa sababu kila kitu kinachoagizwa kutoka nje kitapanda na hatimaye kumletea mwananchi mzigo asioutegemea. Mfano halisi ni bei ya mafuta ikipanda basi ujue kila kitu kitapanda. Hivi ndugu zangu kuna tatizo gani?. Mbona shillingi ya Kenya 103= $1 na hii imekuwa hivi karibu miaka miwili?. Serikali, sisi ni Wananchi na mnatuongoza, kwa kweli tunasononeka sana kwa hali hii. Chukueni hatua za haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…