Shilawadu hapa mlipofikia ni too much

heavyload

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
900
497
Sudi na huyo mbea mwezio wa kiume mmefikia hatua mbaya ya kushindwa kutunza heshima za watu.

Kipindi chenu cha tar 14th/07/2017 hakikuwa cha kistaarabu pale ambapo mlifika KIBONA HOTEL na kuanza kuonyesha hadi mavazi ya ndani za mwanamuziki LINEX kisa kashindwa kulipia bili na kuacha mali zake hapo. Hicho ni kitendo kibaya na sio cha kiubinaadamu.

Hata hivyo kudaiwa ni jambo la kawaida kwani hata serikali inadaiwa na jamaa kaeleza hali hiyo ilijitokeza kutokana na hali ya kujifungua ya mkewe.

My take kwenu Sudi na Kwisa fanyeni kazi lakini tambueni mipaka yenu msikiuke haki za binadamu. Ipo siku mtamfanyia muelewa hatowaacha salama.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Linex juz katumiwa pesa na DJ khaleed
Mkuu Linex kaeleza kuwa pesa alizotumiwa kaenda kumhudumia mkewe aliyejifungua na dj Khaleed kathibitisha hilo na Linex hakukataa kuwa anadaiwa

Sheria ipi inayowaruhusu kina Kwisa kuingia hadi chumbani ampapo jamaaa ameacha mavazi yake na vitu vingine kama passport na boxer. Hata tu mwenye hotel hiyo achunguze athari zitakazotokana na tukio hilo kwani inaonyesha wahudumu wake ni watu wasiofahamu maadili ya kazi yao na watamfukuzia wateja

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom