Shilawadu hapa mlipofikia ni too much

Nilifikiri ni Mimi tu niliyeshituka baada ya kuona tukio lile,
Kiukweli walivuka mpaka wa umbea ukawa uzalilishaji...!!
Mmiliki wa hotel kama hakutoa ridhaa ya kuwaita shilawadu basi ahesabu hana wadanyakazi hapo....!!
 
Hebu na wewe usiegemee upande mmoja tu! Kuna watu wamefukuzwa kazi wawili kwa hilo deni, mmoja anakatwa mshahara na amelalamika anakokaa kodi anadaiwa. Kwa hiyo linex afanye kumhudumia mkewe wenzie wamefukuzwa kazina walibaki wanakatwa mshahara?
Isingekuwa wamefukuzwa watu kazi tungesema ila hao sasa atawaajiri? Halafu angelala hotel za chini kama alijua hana pesa.
Huyu linex kesi za madai nyingi kuliko Show anazofanya
 
ndio nasikia hii... Pole kwa linex, ila mchizi naye masongi yote haya mnashindwa kulipa hela lodge.. Ni aibu..
But kudhalilishana kiasi hicho mi nengeweza hata kufungua kesi mahakamani
 
Ndio mana makonda alitaka kuwakomesha... Kuna kipindi wamerusha habari Mbunge kingu kuwa anatoka na Vanesa bila kumuhoji Kingu, ila wanajifanya walikataa kurusha habari ya Gwajima kisa Gwajima hajaojiwa
 
Na huu nao ni uzalilishaji mwingine lau kama wewe usingeitoa hii post kile kipindi kilishapita na wapo ambao wala wasingejua kama kuna kitu kimepita ila baada ya wewe kutuma post yako hii kuna watu wengi wameanza kufuatilia huo ubuyu wako na kufika ktk upuyu wa akina sudi na kwisa hivyo wewe huna cha kumlaumu sudi kwa kuwa umefanya kilichofanywa na akina sudi

Sent from my SM-G930V using JamiiForums mobile app
Hahaha kweli bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sudi na huyo mbea mwezio wa kiume mmefikia hatua mbaya ya kushindwa kutunza heshima za watu.

Kipindi chenu cha tar 14th/07/2017 hakikuwa cha kistaarabu pale ambapo mlifika KIBONA HOTEL na kuanza kuonyesha hadi mavazi ya ndani za mwanamuziki LINEX kisa kashindwa kulipia bili na kuacha mali zake hapo. Hicho ni kitendo kibaya na sio cha kiubinaadamu.

Hata hivyo kudaiwa ni jambo la kawaida kwani hata serikali inadaiwa na jamaa kaeleza hali hiyo ilijitokeza kutokana na hali ya kujifungua ya mkewe.

My take kwenu Sudi na Kwisa fanyeni kazi lakini tambueni mipaka yenu msikiuke haki za binadamu. Ipo siku mtamfanyia muelewa hatowaacha salama.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Hao shilawadu nawaskia skia,Sema wanavofanya sio poa
kitendo cha kujiita mmbea ni kujidhalilisha.
 
Back
Top Bottom