Shikamoo Mapenzi

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Haya kumekucha amka, amka sasa utume sms nyingine ya "Morning my love" juu ya sms nyingi za jana za "umeshindaje" "nakupenda" "uwe na usiku mwema" ambazo hazikujibiwa tangu mchana na mtu alikuwa online.

Endelea kukomaa kulimwagilia penzi lililokufa, utapigwa blue tick mpaka unuke wino. Wewe unasema ni juhudi, mwenzio anaona ni kiherehere . Wewe unasema unajali, yeye anaona ni usumbufu.

Komaa we si una nguvu kuliko Samsoni, au Juma wa tandale aliyesumbuliwa na mapenzi mpaka akamwambia mama yake 'kua uyaone'.

Anyway mwenzenu Side Kijogoo yalimshinda na ndio maana usiku mmoja kabla ya ndoa aliamua kutumia kadi zile zile za harusi ila alikata kwa peni jina la muolewaji. Akakata Ashura akaandika kwa juu Mwajuma.

Hili tunaita ni tatizo la kiufundi, yaani siku ya ndoa ni ile ile, mahali ni pale pale, ila mwali kabadilika si yule tena mliyekuwa mnamfahamu kwa hiyo hizo zawadi zenu mlizobeba kama mmeandika jina la bi harusi basi chukueni maker pen haraka mbadilishe, la sivyo mtazua balaa kwa Mwajei

Shikamoo Mapenzi .
 
Babe wangu ni Lazima akiamka asubuh Atume Salamu kabla hajaingia kazini, Ni jambo ambalo Tulikubaliana Yeye kama mwanamke ni lazima alifanye .
Screenshot_20230829_111608_WhatsApp.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom