Shikamoo akina mama

mcndomba maprosoo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2013
Posts
225
Reaction score
94
Akina mama wote popote mlipo duniani kupitia kwa mama yangu kipenzi Nyasaland ninawapeni SHIKAMOO yangu ya dhati. Natambua umuhimu wenu mkubwa na wajibu mlionao katika kutunza na kulea familia.

Nazidi kuwaombea kwa Mungu wangu ili aendelee kumjalia kila mmoja wenu afya njema, mafanikio tele, kuwatetea dhidi ya hatari mbaya na kuwalinda na majanga yote.

Mola pia awafanikishe binti zangu Cosy & Salome katika mema yote ili waje kuwa sehemu ya akina mama wema duniani.

Mbarikiwe sana akina mama! Ninawapenda nyote.
Nawatakieni sherehe njema

Ndimi mwanenu mumpendaye
Maprosoo!
 

The home of great thinkers!!!
 
lizinzi utalijua tu....eti shikamoo unataka papuchi ya bure nini?
 
Mleta mada ubarikiwe

Ni nani kama MAMA?

Hebu chukulia kama MAMA asingeweza kukutunza kwa muda wa miezi tisa nina uhakika hata hii mada tusingeiona hapa kutoka kwa mtu kama wewe

MAMA atabaki kuwa MAMA

Inabidi tuwashukuru sana wakina MAMA
 
lizinzi utalijua tu....eti shikamoo unataka papuchi ya bure nini?
pole sana mkuu! inaelekea kuwa ndiyo tabia yako, angalia sana usije ukaharibikiwa bado jamii inakuhitaji maana kwa dunia ya leo kuendekeza uzinzi ni kujiroga mwenyewe. Nakuombea kwa Mola ili akubadilishe na kuondokana na tabia hiyo
 
Mleta mada ubarikiwe

Ni nani kama MAMA?

Hebu chukulia kama MAMA asingeweza kukutunza kwa muda wa miezi tisa nina uhakika hata hii mada tusingeiona hapa kutoka kwa mtu kama wewe

MAMA atabaki kuwa MAMA

Inabidi tuwashukuru sana wakina MAMA

Hakika hakuna hakuna amzidiye mama. hata Suleman asema, "mwanamke mwema ni taji ya mumewe", Mith 12:4.
Muendelee kubarikiwa mama zangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…