Shija: Siwezi kupona lazima nitakufa!

Shija: Siwezi kupona lazima nitakufa!

Wapinzani wa kweli bado hawajazaliwa tz,siyo hawa wachumia tumbo,bora CCM itawale miaka bilioni ijayo,wapinzani akina mbowe,lowassa,sumaye,mbatia au zitto? Bora tuongozwe na ngiri na siyo hawa watu
Umevuta bange ya malawi eeh
 
Mkuu Tinde Nsalala, kwanza pole kumpoteza rafikiyo kipenzi John, pili ni very touching story. RIP John.

Hapa duniani hakuna kimya, there is nothing new under the sun, uhai umeumbwa na kifo pia kimeundwa, mtoa uhai ndio Huuchukua .

Ile siku John anaumbwa kila kitu kuhusu maisha yake kilikuwa kimeisha andikwa hadi atakufaje na lini, saa, dakika, sekunde hadi nukta.

Malaika mtoa roho, Israel, anaipitia kila nafsi kwa saba mara 70 kila siku ili saa yako ikifika, asipitishe hata nukta moja.

Hivyo saa ya John ikifika, saa yako inakuja, usisahau kuuacha ujumbe wa maandishi kuhusu hiyo "AIWA" ili iwekwe pembeni yako uende nayo kumpelekea kama ulivyo muahidi.

Hapa duniani ni mapito tuu, makao yetu ni kule aliko John.

Muda mfupi Kabla ya Kukata roho: NINI HUTOKEA?

Life after Death: What Happens after Death?

Paskali
Umenena vyema ndg.Kuhusu AIWA hakika nitafanya km ulivyoniasa.
 
Shija,SIWEZI KUPONA!

Ni kauli ya mwisho ya RAFIKI yangu kipenzi,JOHN aliyoitoa akiwa amelalia mapaja yangu jioni ya J'pili moja huko Zanzibar.

Nathubutu kutamka-JOHN aliuawa!Muuaji wa JOHN ni VURUGU za ki-SIASA zilizopata kutoka huko visiwani mapema mwa miaka ya 2000.

Mapema siku hiyo (niliyoitaja hapo juu)rafiki yangu aliniaga "Akinitaja jina .... naelekea kwenye mkutano wa MAALIM" alimaanisha Maalim Seif."Poa.."nilimwitikia.Haikuwa desturi.Desturi ya rafiki yangu huyo kuchelewa kurudi hata eti baada ya saa moja usiku!Siku hiyo,na kwa mara ya kwanza John sikuwa nimemwona ndani ya mda zoea.Hata baada ya saa zingine 2 kupita,rafiki yangu Huyo sikumwona.NILIPATWA na MASHAKA!Mashaka hayo ni kwa sababu haikuwa kawaida ya JOHN!


NILITAHARUKI!Taharuki hiyo ikanipelekea kuvuta kumbuku ya wapi John aliniaga akielekea.Nilijisemea moyoni "ktk mkutano wa Maali...". Hamad,hata kabla sijamalizia kujisemea sauti ya mtangazaji 'mwanamke' ktk kituo cha redio niliyokuwa naisikiliza kwa wakati huo,alitamka " VURUGU kubwa zimejitokeza jioni ya leo ktk mkutano usio kuwa umepatiwa kibali na polisi wa wanachama wa CUF" alisema.Hakika,akili ilinituma moja kwa moja ktk ushiriki wa rafiki yangu.Niliamini alikuwa MHANGA wa habari tajwa na kituo kile cha redio.Kwani,hata mda wa yeye kupitiliza kurejea nyumbani,kulinipa uhakika huo.Ikawa MTIHANI mkubwa kwangu!


Mosi,MTIHANI wa kipi John kimemsibu?!

Pili,MTIHANI wa je,yu wapi 'kwa wakati huo' mgeni mwenza wa huko visiwani?!

Sikupata majibu kwa wakati huo zaidi ya kutahayaruki tu!Km mwanaume,niliendelea kuwaza na kuwazua kuhusu VURUGU zile tajwa na hatima ya rafiki John.


Saa 5 usiku nikiwa na hangaikia usingizi sauti ya mtangazaji,kijana ilihabarisha..."Majeruhi wa VURUGU zile walikuwa wapo ktk Hosp fulani huko visiwani".Nilijisemea 'mara moja acha nielekee huko.Nilienda.

Mamia ya majeruhi ktk kituo hicho cha afya waliniogopesha!Roho iliniamisha John yu mmoja wa wale.Nilimtafuta na kumpata.Hakika alikuwa ni mmoja wa majeruhi waliojeruhika VIBAYA!


Damu ilimtoka sehemu mbalimbali ya mwilini mwake John wangu!Mbavu nne zilikuwa tayari zimeshavunjika!Mkono wa kulia nao ulikuwa imevunjika mara tatu!Jicho la kulia pia lilivuja damu nyingi!HAKIKA,hapakuwa na sehemu iliyo salama.."Nilijisemea".


JOHN "nilimwita"?Shija,SIWEZI KUPONA na lazima nitakufa "alisema"!Siasa inaniua!Nimeteleza kutoka juu ya mnazi na kuumia vibaya!Sijui hata km nitamuona MAMA yangu tena!"ALIKATA ROHO!

Nililia na kuhudhunika sana!Mapaja yangu yalikuwa yamejaa damu ya John!NILIMPOTEZA JOHN wangu!

Nilijiuliza;

Je,mkutano wa SIASA ulikuwa na sababu ipi ya kuutoa uhai wa John?!

Ni kweli John aliuawa na kuteleza kwake toka mnazini?!

Na kwa nini alipanda mnazi?!

Nilipata jibu,John alipanda mnazi kwa kuogopa mabomu ya machozi!La isingekuwa mabomu ya machozi hata leo John angekuwa hai.Sisemi vyombo vya ulinzi vilitamatisha uhai wa John la hasha!Bali uoga wa John wakupigwa mabomu ya machozi ndiyo hasa kilichompelekea yeye kupanda na kudondoka juu ya mnazi.

NATAKA KUSEMA NINI KTK HILO:

Ndg zangu,SIASA za chuki tuachaneni nazo.SIASA za mlengo huo zitawaangamiza kina John wengi sana!Tuweni na malidhiano ktk yote. Sisi sote ni waTz na nchi hii yetu wote.Tusihukumiane kwa KISASI bali kwa KUVUMILIANA.

Tuheshimiane,tujaliane,tusaidiane na TUPENDANE.Tuwe na wepesi na TAMAA ya KUSAHIHISHANA hata pale tulipopishana ama kwa lugha au kwa matendo.

MAISHA tuishiyo hapa duniani ni mafupi mno!Sote tu WAJA WAKE.


Kwako John, TAMBUA nakukumbuka sana rafiki yangu.REDIO yako 'AIWA' Bado ninayo!NAAHIDI nitakuja nayo siku tukikutana huko ulipo mola akipenda.AMIN!
Pole kw yaliyokukuta ndg, ila hili la radio ndio.......... Kw mungu au!
 
So what!!!wamaanisha bora tuendelee nao hawahawa!!!umerogwa na nani weye mtu.kakojoe ukalale nyambafuuuu
Matusi ya nini nimejaribu tu kukupa mfano wa ANC wewe unatoa matusi,kuna watu wamepoteza damu zao kuwasaidia tu viongozi kupata nafasi ya kupata madaraka,ukisoma vizuri hata John anafuga kufa kwa ajili ya siasa
 
Huwezi amini lakini nakuhakikishia hata CUF wakiongoza watakuwa hivyo hivyo mfano chukua toka ANC ya Zuma anavyowatandika waandamanaji
Wewe hata ukiwatetea hao wauwaji wenzako CCM, huna pa kutokea, damu za raia wasio na hatia zimewaganda katika mikono yenu, na iko siku Mungu atawalipa mmoja baada ya mwengine.
 
Wewe hata ukiwatetea hao wauwaji wenzako CCM, huna pa kutokea, damu za raia wasio na hatia zimewaganda katika mikono yenu, na iko siku Mungu atawalipa mmoja baada ya mwengine.
Sijawatetea popote nachokushauri fanya kazi upate pesa au jiweke karibu na uongozi ili siku mkitawala nawe uwe miongoni mwa wapigaji la sivyo utaendelea kulaumu mpaka umauti ukufike
 
Sijawatetea popote nachokushauri fanya kazi upate pesa au jiweke karibu na uongozi ili siku mkitawala nawe uwe miongoni mwa wapigaji la sivyo utaendelea kulaumu mpaka umauti ukufike
Mm sina shida ya kuwa karibu na uongozi, wala mm si mtu wakutegemea utawala, na wala mm sio kazi yangu kulaumu ila nakufahamisheni, uongozi ni dhamana musijisahau, mm naishi vizuri sana na nasomesha watoto wangu vizuri sana na nnapata rizki yangu bila kumdhulumu mtu, ya halal kabisa, ila nnawakumbusha tena nyinyi ma opportunist duniani tunapita tu kila mtu atalipwa kwa alioyafanya.
 
Huu ni 'mtego' wa ibilisi ambao umenasa wengi mno;ni uwanja wa maslahi,uwanja wa hadaa na uongo,maficho ya madhalimu dhidi ya umma,uwanja wa kuwindana kama mahayawani,uwanja wa visasi na ni uwanja wa kuchafuana.Zote hizo ni shughuli zinazoratibiwa kiustadi na ibilisi na kutekelezwa na wafuasi wake watiifu.
 
Wewe hata ukiwatetea hao wauwaji wenzako CCM, huna pa kutokea, damu za raia wasio na hatia zimewaganda katika mikono yenu, na iko siku Mungu atawalipa mmoja baada ya mwengine.
Mwambie huyo killer
 
Maneno kuntu!Malidhiano hakika ndilo jambo pekee litalo leta suluhu ya kisiasa.Shime wafanya SIASA pendaneni.

Siyo wanasiasa tu watanzania kwa ujumla wetu.Nilitegemea hii ingekuwa motto hata kwa sisi JF members kuacha siasa za chuki na ku-advocate for peace
 
Mm sina shida ya kuwa karibu na uongozi, wala mm si mtu wakutegemea utawala, na wala mm sio kazi yangu kulaumu ila nakufahamisheni, uongozi ni dhamana musijisahau, mm naishi vizuri sana na nasomesha watoto wangu vizuri sana na nnapata rizki yangu bila kumdhulumu mtu, ya halal kabisa, ila nnawakumbusha tena nyinyi ma opportunist duniani tunapita tu kila mtu atalipwa kwa alioyafanya.
Good mkuu
 
Back
Top Bottom