Shija: Siwezi kupona lazima nitakufa!

Shija: Siwezi kupona lazima nitakufa!

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
248
Reaction score
253
Shija,SIWEZI KUPONA!

Ni kauli ya mwisho ya RAFIKI yangu kipenzi,JOHN aliyoitoa akiwa amelalia mapaja yangu jioni ya J'pili moja huko Zanzibar.

Nathubutu kutamka-JOHN aliuawa!Muuaji wa JOHN ni VURUGU za ki-SIASA zilizopata kutoka huko visiwani mapema mwa miaka ya 2000.

Mapema siku hiyo (niliyoitaja hapo juu)rafiki yangu aliniaga "Akinitaja jina .... naelekea kwenye mkutano wa MAALIM" alimaanisha Maalim Seif."Poa.."nilimwitikia.Haikuwa desturi.Desturi ya rafiki yangu huyo kuchelewa kurudi hata eti baada ya saa moja usiku!Siku hiyo,na kwa mara ya kwanza John sikuwa nimemwona ndani ya mda zoea.Hata baada ya saa zingine 2 kupita,rafiki yangu Huyo sikumwona.NILIPATWA na MASHAKA!Mashaka hayo ni kwa sababu haikuwa kawaida ya JOHN!


NILITAHARUKI!Taharuki hiyo ikanipelekea kuvuta kumbuku ya wapi John aliniaga akielekea.Nilijisemea moyoni "ktk mkutano wa Maali...". Hamad,hata kabla sijamalizia kujisemea sauti ya mtangazaji 'mwanamke' ktk kituo cha redio niliyokuwa naisikiliza kwa wakati huo,alitamka " VURUGU kubwa zimejitokeza jioni ya leo ktk mkutano usio kuwa umepatiwa kibali na polisi wa wanachama wa CUF" alisema.Hakika,akili ilinituma moja kwa moja ktk ushiriki wa rafiki yangu.Niliamini alikuwa MHANGA wa habari tajwa na kituo kile cha redio.Kwani,hata mda wa yeye kupitiliza kurejea nyumbani,kulinipa uhakika huo.Ikawa MTIHANI mkubwa kwangu!


Mosi,MTIHANI wa kipi John kimemsibu?!

Pili,MTIHANI wa je,yu wapi 'kwa wakati huo' mgeni mwenza wa huko visiwani?!

Sikupata majibu kwa wakati huo zaidi ya kutahayaruki tu!Km mwanaume,niliendelea kuwaza na kuwazua kuhusu VURUGU zile tajwa na hatima ya rafiki John.


Saa 5 usiku nikiwa na hangaikia usingizi sauti ya mtangazaji,kijana ilihabarisha..."Majeruhi wa VURUGU zile walikuwa wapo ktk Hosp fulani huko visiwani".Nilijisemea 'mara moja acha nielekee huko.Nilienda.

Mamia ya majeruhi ktk kituo hicho cha afya waliniogopesha!Roho iliniamisha John yu mmoja wa wale.Nilimtafuta na kumpata.Hakika alikuwa ni mmoja wa majeruhi waliojeruhika VIBAYA!


Damu ilimtoka sehemu mbalimbali ya mwilini mwake John wangu!Mbavu nne zilikuwa tayari zimeshavunjika!Mkono wa kulia nao ulikuwa imevunjika mara tatu!Jicho la kulia pia lilivuja damu nyingi!HAKIKA,hapakuwa na sehemu iliyo salama.."Nilijisemea".


JOHN "nilimwita"?Shija,SIWEZI KUPONA na lazima nitakufa "alisema"!Siasa inaniua!Nimeteleza kutoka juu ya mnazi na kuumia vibaya!Sijui hata km nitamuona MAMA yangu tena!"ALIKATA ROHO!

Nililia na kuhudhunika sana!Mapaja yangu yalikuwa yamejaa damu ya John!NILIMPOTEZA JOHN wangu!

Nilijiuliza;

Je,mkutano wa SIASA ulikuwa na sababu ipi ya kuutoa uhai wa John?!

Ni kweli John aliuawa na kuteleza kwake toka mnazini?!

Na kwa nini alipanda mnazi?!

Nilipata jibu,John alipanda mnazi kwa kuogopa mabomu ya machozi!La isingekuwa mabomu ya machozi hata leo John angekuwa hai.Sisemi vyombo vya ulinzi vilitamatisha uhai wa John la hasha!Bali uoga wa John wakupigwa mabomu ya machozi ndiyo hasa kilichompelekea yeye kupanda na kudondoka juu ya mnazi.

NATAKA KUSEMA NINI KTK HILO:

Ndg zangu,SIASA za chuki tuachaneni nazo.SIASA za mlengo huo zitawaangamiza kina John wengi sana!Tuweni na malidhiano ktk yote. Sisi sote ni waTz na nchi hii yetu wote.Tusihukumiane kwa KISASI bali kwa KUVUMILIANA.

Tuheshimiane,tujaliane,tusaidiane na TUPENDANE.Tuwe na wepesi na TAMAA ya KUSAHIHISHANA hata pale tulipopishana ama kwa lugha au kwa matendo.

MAISHA tuishiyo hapa duniani ni mafupi mno!Sote tu WAJA WAKE.


Kwako John, TAMBUA nakukumbuka sana rafiki yangu.REDIO yako 'AIWA' Bado ninayo!NAAHIDI nitakuja nayo siku tukikutana huko ulipo mola akipenda.AMIN!
 
Tujifunze kuvumiliana.

Ni rahisi sana kwa Wapinzani kuwavumilia wanachama wa CCM lakini si rahisi wanachama na Viongozi wa CCM kuwavumilia Wapinzani.

Umefika wakati Viongozi wa CCM waanze wao kuwaonyesha wanachama wao kwamba Upinzani si.uadui.Tunaona Rais akisadiana.na wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na polisi kutesa na kunyanyasa Wapinzani ifike mahali tuseme imetosha Taifa letu sote.Na.sote tuna haki ya kuishi na kuwa Viongozi ndani ya Taifa letu.

Viongozi waastaafu ni wakati wa kuamka mliko lala Tanzania yetu sote Mpinzani si RAIA wa kigeni ni Mtanzania mwenye haki zote za kiraia.Elimisheni wanachama wenu itoshe kusema sasa ubaguzi,chuki na visasi basi.

Tukae meza moja tushirikiane kujenga Tanzania
 
Back
Top Bottom