Shigella amjibu sumaye tena

Kilichonichosha n baada ya hawa jamaa kukana matamshi yao wenyewe... bila hata aibu!
 
Waache wagombane wao kwa wao. Mwisho watasahau kuiba kura 2015, then CDM inachukua nchi.

SUMAYE ofcourse wote tunajua hafai kuwa Rais; lakini hata hao vijana kama kweli wanaitakia mema nchi hii, hivi ni kweli uporaji wa mashamba wa Sumaye na kukopa milioni 50 kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii, kunamfanya awe mbaya sana zaidi ya Kikwete, Lowassa na Rostam? Kweli?
Huwezi kuwasikia UVCCM wakizungumzia deep green, meremeta au hata epa ila sumaye..!
 
anamtuhumu sumaye kukwapua mil 50 kutoka ktk mfuko wa jamii na kumiliki ardhi kubwa huku amesahau, au hajui kuwa hao anaowatetea ni wale wale tulikuwa tunawalipa mil 152 kwa siku na bado wanatudai bil 94 jamani wanafight kwa huo urais utafkiri ni lazima rais atoke ccm wao walumbane mwisho wa siku with assistance ya katiba mpya Dola haitatuamulia rais.
Ushauri wangu kwa shigela na wahuni wenzake ni 'Toeni kwanza boriti katika macho yenu ndio mtaona vibanzi katika macho ya wenzenu'
 
<SOURCE> taarifa chanel ten

Asema wanamashaka na uwezo wake kuwa rais wa Tanzania 2015

mvurugano

nawasisha

FREDDY SUMAYE HEBU WAPELEKE NA HAWA HUKO ULIKOSOMA MAJUZI NAO WAPATE KUBADILIKA NDIPO URUDI TUKAJADILI WEWE KUTAMANI KUWA RAIS WANGU

Kwa watu makini, hata bila kumona uso kwa uso huyu aliyekua Fundi Mitrekta Freddy Sumaye aliyeishi siasa zetu chafu hapo kipindi cha nyuma na ukachukua wala dakika chache kumlinganisha na Mheshimiwa Fredrick Sumaye tuliemsoma moja kwa moja akiripotiwa na Invisible kwenye Press Conference aliyojiitishia pale Courtyard Hotel basi bila shaka utagundua kwamba kweli darasa bila DESA imetusaidia kwa kiasi kikubwa kupangusa uzuri kopo ambalo sie wengine tulishalitupa kwenye jalala la kule Vigunguti na sasa lafaa kuchotea tena maji ya kunywa kumpelekea mgeni rasmi (wapigakura) sebuleni!!

Kwa msingu huo nilitamani hata naye huyu Fisadi wa Kimaasai tukimpeleka tu shule huko ma-Ughaibuni mbona hizi siasa za fitina fitina na kutembeza senti tano mitaani ataziacha tu!!

Ila hili lingine ambalo akimuingiza mtu kwenye BLACK BOOK yake basi mpaki kifo ndicho kije kuwapatanisha nasema hata tungempeleka shule za kule nchi ya ya Mzee Shaaban Robert (Kusadikika) wala huo ukoko wa sias za Chuki, Visasi, Vinyongo, Umimi, Upwani, na mambo mengine kama hayo kamwe hayawezi kumtoka.

Shule hutakasha bwana usiombe; hebu muone yule Fundi Mekanika wa mitrekta aliyesome SUA, Freddy Sumaye, leo hii MBA ya ukweli ilivyompiga jiki kichwa na kuondoa yale mi-oili chafu yote ya mitrekta mbovu; hata anapozungumza siku hizi mtu unaweza ukapata cha kwenda kumsimulia mtu wa pili na wala hana tena ile LUGHA YA MAFUNDI tuliokua tumzoea nayo huko nyuma.

Mhe Sumaye, japo kwenye mahesabu yetu ya kuwa rais wa nchi hii na wewe wala haumo lakini hebu chonde mfanyie mpango huyu ndugu Eddu wa Monduli naye aende huko ulikoenda kula Kitabu walau akabadilike. Maana, kwa kusema ukweli, mtu ukimtazama kwa karibu Ndugu Lowasa, Mrema Augustino, Rostam Aziz, Seif Shariff Hamad, Nchimbi, Malisa, Ridhiwani Kikwete, Makamba Junior, Hussein Mwinyi, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe ... na wengine wengi tu hapa nchini na kweli kabisa utakuta ni watu wenye uwezo mkubwa sana tu ambao taifa letu limebahatika kuwapata isipokua tu wanakosa sana kati ya mambo haya matatu:

(1) PERSONAL ETHICS AND LEADERSHIP INTEGRITY

(2) SOUND EDUCATION BACKGROUND, VISIONARY & READINESS TO LEARN AT ALL TIMES, and

(3) EXPOSURE FAR BEYOND THEIR OWN NEIGHBOURHOODS

Hivyo nasema hapa kwamba laiti viongozi wetu wangelikua ni watu wa kukosolewa wakakosoleka, wasikivu na wenye kujitathmini wenye tu japo hata mara moja katika ngazi ya nafsi yake mwenyewe, basi ni kwamba mtu utagundua kuna mikasoro ya kufanyia kazi. Lakini pale ambapo mwanasiasa ni ni Mbumbumbu (hata kama kapata vijidarasa vichache tena kwa KUDESA TU OPEN UNIVERSITY pale Kinondoni) na kwamba hana habari kama kweli yeye ni mbumbumbu, na kwamba bado yuko tayari hata kutafuta umbumbumbu wake huo kwa kutumia VIJISENTI MITAANI ili umbumbumbu wake huo uonekane kwamba ina mng'ao sawa tu na Almasi zetu toka kule Mwadui, basi hadi hapo ndipo taifa zima mjue kwamba tunalo MZIGO MKUBWA SANA TENA GUNIA LA MISUMARI YA MOTO kuubeba wakati wote mgongoni.

Ningeendelea sana kuomba Shule alikoenda yule Fundi Sumaye na lugha / fikra za kwenye mi-gereji tu kichwani hadi leo hii karudi nyumbali mtu ambaye si lazima akutangazie kama kaongeza darasa bali kwa nidhamu tu ya lugha yake, direction thabiti kwenye maelezo yake (japo mie sijayanunua bado) na kwenda kwa stepu bila uswahili na fitina mingi ni dalili tosha kwamba kweli mwenzetu huyu kapata shule BILA KU-DESA na kwamba shule hiyo hakika imemkomboa hivi sasa!!

Jamani kiongozi wa ngazi yoyote akiwa na walau sifa hizo tatu hapo juu basi kazi huwa ni nyepesi mno lakini the vice versa ni kiama. Ndio maana wataalam wetu wote wanaofanya kazi chini ya madiwani katika jiji, manispaa na halmashauri mbalimbali nchini KIKUKWELI NAWAHESHIMU MNO maana mazingira yao ya kazi ni ngumu kupita kiasi kwa sababu mabosi wao ambao ni madiwani waliowengi ni watu ambao ni MBUMBUMBUMBU WA KUDUMU KWA KUJICHAGULIA!!!

Na wala usiniulize kwa nini Mambumbumbu wa jiji la Dar es Salaam nao waliona kero sana baada ya CCM nacho kuligundua tatizo hili ninalolizungumzia na kuamua kuwaletea diwani PhD Masaburi na watu tukasikia in a chorus mambumbumbu wa jiji wakigoma kabisa kumkaribisha huyu mtu aliyeona mwanga, kusafiri sana ila kama anayo personal ethics na leadership integrity bado nasubiri kwa hamu kuona PRACTICAL RESULTS jijini na wala si mi-ripoti mizuri mizuri na takwimu yasio na maana yalioandaliwa kwa utaalam mkuba.

Mhe Sumaye, wahimize wanasiasa waende shule zisizoendekeza KUDESA, WACHANJE MBUGA MBALI NA VIJIJI WALIKOZALIWA ILI WAJUE KWAMBA KUMBE KWINGINEKO KUNA MPISHI MZURI ZAIDI AMBAYE WAZAZI WETU WANGEENDA NAO KUJIFUNZA. Chonde wasaidie maana katika hizo points tatu hapo juu viongozi wetu wamegawanyika katika mix ambazo ni so interesting.

Kwa mfano, na ninasema kwa nia njema kabisa, Zitto Kabwe anayo good education background bila DESA ila hana personal ethics wala leadership integrity.

Mheshimiwa Lowassa anayo very UNIQUE IN-BORN TALENT of both Social and Business Enterpreneurial Mind lakini hajaruhusu ikapigwa msasa hii talanta imekua naexcesses nyingi mno katika jamii. Jambo ambalo linatushawishi ku-question his genuine education background so far, na his personal ethics and leadership integrity is REALY WANTING.

Mheshimiwa Mrema ni mtu mmoja ambaye otherwise ni LULU KWA TAIFA LETU. Watu wa aina yake huwa hawazaliwi wengi sana ndani ya kipindi kifupi. Watu wa aina yake ambao nao ni lulu ni akina Mwalimu Nyerere, Dr Ali Mohamed Shein, Salim Ahmed Salim, Everist Kaigaruki, Magufuli, Moringe Sokoine, Mama Nkya ... lakini a mark of an UNTRACEABLE SOUND EDUCATION background inamuangusha sana ila Personal Ethics ni Average na Leadership Integrity imesimama mpake arudi kwa muumba wake.

Julius Mtatiro anayo personal ethics and leadership integrity ya hali ya juu (hata kama bado hajajaliwa fedha wala haonyesha uharaka wa kuzikimbilia), huyu bwana kwa UDSM pale wenzake waliosoma naye wanamheshimu kitaaluma ila dosari yake kubwa ni kwamba hajui lolote zaidi ya mipaka ya Tanzania basi!!

Mhe Sumaye wasaidie wenzio waenda NDANI YA DARASA ulikoenda wewe (japo swala la wewe kuwa rais wangu tutaujadili siku nyingine) ili wakome kuwa miziko yetu kifikra na matendo yao!!!

quote_icon.png
Originally Posted by Ntemi Kazwile
Dah kumbe shule nzuri bwana, tangu amalize MBA yake siku hizi Sumaye anaongea point, nimeshitushwa kidogo maana nilizoea kumsikia akitoa point zilizokuwa tata sana enzi za uwaziri mkuu wake.

Hongera Sumaye
 
Back
Top Bottom