SHIEE: Unampenda mtundu wa kupika msosi na fundi kitandani tena?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,103
34,063
UJUMBE: HUJAOA/ HUOI MALAIKA, UNAOA BINADAMU.

Habarini wadau,

Kama unaoa binadamu basi lazima atakuwa na mapungufu flaniflani.

Unakuta boya akija maskani au akiwepo popote anamsifia mwanamke mwingine kuwa anajua kupika sana au anazungusha kiuno balaa awapo kitandani, bora hata umsifie usafi, wakati huo anamponda mke wake mbele za washkaji au hatari zaidi kwa mwanamke mwingine.

Ni umbwira huo.

Kama wife wako sio fundi kitandani, basi atakuwa anajua kukujali kwa msosi mzuri, kama vyote hivyo havijui basi atakuwa anajua na anapenda kukufulia nguo zako unazochafua.

Kama hawezi hayo basi atakuwa anaweza kusimamia majukumu mengine home na kumwongoza binti wa kazi au shamba boy kutimiza majukumu.

Hawezi yote hayo utakuta analima sana au ni msimamizi mzuri wa biashara kama Wachaga wengi.

Huwezi pata manzi / wife ambaye ni kama malaika jomba.

Sasa ukienda kumtangaza kwa washkaji au wenzake ndio ili iwaje au wafanyaje. Ni uboya.

Kuna muda hata sisi tunazingua sana ila wanatuvumilia.

''Wanaume'' waliooa watanielewa fresh kasoro wavulana.

Hujaoa malaika, umeoa binadamu mwenye jinsia ya kike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama mke hawezi majukumu ya kitandani itabidi beki 3 a-take place.
 
hamna kitu kinakera kama mwanaume kwenda kujadili mapungufu ya mkewe kwa mchepuko...
 
Udhaifu namba moja ni kwenda kumponda mke wako kwa washkaji zako/kwa mchepuko.

Bora useme mke wangu ananipiga, kuliko kusema weakness za mke wako. Acha mke hata girlfriend wako tu haipendezi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi zetu hayo yalikuwa yakiongelewa na wanawake saluni, mmechoka kujadili siasa na mpira kwenye kahawa au mmechukua nafasi yao..?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom