Shida ya maji mchana wilaya ya Moshi

myoyambendi

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
157,903
687,138
Jamani wahusika naomba mtujibu, siku hizi kwenye mji wa Moshi maji mchana imekuwa bidhaa adimu majumbani kwa watu, ila cha kushangaza seheme za kuoshea magari mpaka wanamwaga ovyo! hata kama ni biashara muwe 'mnabalansi' na watu majumbani wapate, he!!
 
Mdau huko moshi hasa msimu wa kiangazi huwa ni kawaida kwa mgao wa maji, kuna wanaopata mchana jioni yanakatwa na wengine mchana hamna hadi jioni. Cha muhimu uwe na reserve tank kuna mikoa mingine maji yanaonekana mara moja kwa wiki au mwezi.
 
duh. litangazwe janga, kwani tuna ukame kama sudan? hiku wangewaelimisha waoshaji wa magari wajenge uwezo wa 'kurisaiko' maji baada ya kuyatumia, wayapate tena hata nusu yake. yooote yanapotelea chini!!
 
Hilo uanze kuliweka akilini, mji unapanuka na wakazi wanazidi kuongezeka, idadi ya taasisi hasa za kielimu nazo zinaongezeka hivyo tegemea matumizi ya maji nayo yanazidi hasa huu msimu wa kiangazi. Andaa tank yako ya lita 2000 mapema kabla hali haijawa mbaya zaidi
 
maji ni tatizo Tanzania, au Africa nzima kabisa, moshi mna bahati sana mnayaona angalau hiyo mchana unayoilalamikia, kwingine wanajatiwa wanahesabu wiki
suluhisho ni kununua tank la kuhifadhia maji, maana mabadiliko ya hali ya hewa yanavyotokea mito mingi ya maji fresh inakauka
 
Wewe unayelalama unaishi moshi ama porini?Sisi huku njoro ya dobi,kwa bibi Angu mandaka tuna maji 24/7 ,Si ajabu umevamia sehemu za wazi ama hifadhi ndo maana idara ya maji hawajakuketea hudumu!Tafakari chukua hatua!
 
karibu na kiwanda cha bia cha serengeti, kama unaeda TPC
Mie najua kilipo kiwanda cha TBL na kingine kilikuwa kinatengeza kimea cha bia, Tanzania Bag. Ila kilipo kiwanda cha Serengeti sijui ni sehemu gani? enewei Moshi nina siku nyingi sijatembea huko mwaya myoyambendi
 
tembelea uone pamebadilika sana, kuna kiwanda kipya cha bia barabara ya kwenda tpc karibu na 'geti fonga' maeneo ya matindigani ndio mji mpya, zamani tukilima mpunga
 
tembelea uone pamebadilika sana, kuna kiwanda kipya cha bia barabara ya kwenda tpc karibu na 'geti fonga' maeneo ya matindigani ndio mji mpya, zamani tukilima mpunga
Haya, siku nikifanikiwa kukanyaga ardhi ya nyumbani Kilimanjaro nitakuja kutembea hapo Moshi mjini kwa masaa kadhaa
 
Back
Top Bottom