shida hizi mpaka lini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

shida hizi mpaka lini??

Discussion in 'Jamii Photos' started by ngoshwe, May 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hospitali ya Ludewa (Jimbo la Prof. Raphael Mwalyosi) !!


  [​IMG]
  Akina mama ambao wanawauguza ndugu zao katika hosptali ya Wilaya ya Ludewe wakisonga Ugali nje ya wodi ya akina mama wanaosubiri kujifungua, kati ya akina mama 100,000.wajawaito 200 hupoteza maisha katika Wilaya hiyo kutokana na ukosekanaji wa miundombinu.
  [​IMG]
  Wanawake wajawazito toka katika vijiji 76 vinavyo zunguka Wilaya ya Ludewa wakiwa wamelala na wengine wakila chakula huku wakiwa wamesubilia siku zao za kujifungua katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Iringa kati ya akina mama 100,000 wajawazito 200 hufariki kutokana na ukosefu wa huduma.
  [​IMG]
  Inasikitisha: Baadhi ya akina mama wajawazito wakiwa nje ya wodi ya wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Ludewa ambapo jengo hilo lina vitanda 6 na kila kitanda hutumiwa na akina mama wajawazito wawili. Wengine hulazimika kulala chini.  SHULE ZA MSINGI:

  [​IMG]
  Wanaoonekana pichani ni wanafunzi wa shule ya Msingi Juhudi iliyopo katika Wilaya ya Kigoma Vijijini mkoani Kigoma nchini Tanzania (Shule ya Msingi Juhudi - Kigoma Vijijini, Tanzania - wavuti)

  [​IMG]
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Kinole, katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro, wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba mkubwa wa madawati unaoikabili shule hiyo

  [​IMG]

  Mwalimu, Albert Juakali wa shule ya msingi Iboma iliyopo kijiji cha Udinde Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya Mti wa Mbuyu.

  [​IMG]

  Maisha Bora kwa kila Mtanzania?.  [​IMG]
  Tunazungumzia "fly overs" sasa!!

  Transport_preview.jpg


  Mtazamo:

  Hivi shida za watanzania hawa wanasiasa hawazio kwa macho??. Hata lini wataendelea kutumia matatizo ya msingi ya wanachi kama kauli mbiu ya kutaka kushindia uchaguzi.? HILI ENEO LINA MBUGE NA WATENADJI WOTE WA SERIKALI NA SIO KUWA HAYA MAISHA HAWAYAONI WALA HAWAYAJUI. LAKINI BADO VIONGOZI HAWA WANADIRIKI KUTUNISHA VIFUA MBELE HUKU WAKITUMIA FEDHA ZA UMMA NA KUENDELA KUTAMBA HUKU NA KULE KUWA WATANZANIA TUNA MAISHA BORA!!

  INASIKITISHA NA KUTIA UCHUNGU SANAAAANA SANA!.  Ikiwa haya maeneo ambayo watu wamekuwa wakiishi kama hawapo tanzania yana viongozi ambao walichaguliwa kwa ahadi ya kuwaletea masisha bora, ni vyema sasa wakati tukielekwa uchaguzi mkuu, matatizo kama haya yabainishwe kama sehemu ya kuwawajibisha Wanasiasa na viongozi wa Serikali katika maeneo husika kwani nchi inaangamia.

  Tafadhali kama inawezekana kupata thread maalumu ya kuchangia maoni kwa mifano ya wazi ya picha za maeneo ambayo hali ni ngumu kuliko vile wanasiasa wanavyojigamba, itakuwa ni jambo jema ili ikibidi jamii ijue na kupima iwapo viongozi husika wanastaili kuendelea kujigamba majukwani kuhusu maisha bora kwa watanzania.
   

  Attached Files:

 2. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  its sooo sad jamani...
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,974
  Likes Received: 21,140
  Trophy Points: 280
  just imagine,kwa hela ya VX moja ya mbunge kungekuwa na mabadiliko gani hapo,vitu vingine havihitaji hata degree/phd just common sense.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,983
  Likes Received: 690
  Trophy Points: 280
  Mkuu, silaha tunayo.........CCM imetuchosha, ushawahi kusikia waziri au katin=bu mkuu au kamishina amekosa VX yenye mafuta full tank, au umeme umekatika kwa sababu luku haijalipwa na serikali on time? au posho za wabunge zimeshindwa kulipwa on time?

  kweli kuanzia uhuru tumeshindwa kujenga ward standard hapo? hata tukiachilia mbali vitanda........tujenge anagalau jengo moja refu kama bweni ili liwasitiri mama zetu!!

  lakini again hao hao watawapa CCm kura japokuwa wanalala nje na kwenye wodi chakavu!!
   
 5. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yaani hii inauma sana. jamani watz tuamke hii nchi inaliwa visivyo, hao wamama hivi kweli hapo wako hospitali kweli, daktari gani atakaa hapo kuzalisha hao wamama jamani, si wangebaki wajifungulie home tu kuna tofauti gani hapo. hapo na hela ya wembe wanalipia wenyewe, wembe yaan, wembe na vikorombwezo vingine. na hao ndo wanaoipa kura zaidi ccm, watu wa vijijini ndo wanatoa zaidi kura ccm. Mungu awasaidie jamani jamaniiiiiiiiiiiii, just imagine your wife anasubiri kujifungua kwenye mazingira kama hayo, na ana imani tosha kuwa yuko mahali salamaaaa. inauma sana.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  May 10, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  I'm just sayin'...I'm not sayin'...but you know what I'm sayin'.....
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Wakuu wanaohusika wapo wapi?Inaonyesha hakuna Serikali hapo mahali. EEhh WaTanzania hivi tutauondosha lini Umasikini? Inaonyesha Wakuu wanaohusika wamelifumbia macho Tatizo hilo la Donda Sugu wao kuwa na Magari ya kifahari wanyonge ndio tunaoumia ama kweli Waswahili husema mwenye Nguvu mpishe apite mungu atusaidie kuondosha huu umasikini na kutupatia Viongozi wenye huruma juu ya Wananchi wake ameen
   
 8. MANI

  MANI Platinum Member

  #8
  May 10, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,413
  Likes Received: 1,873
  Trophy Points: 280
  Hayo ndio maisha bora kwa kila Mtanzania aliyohubiri Mkulu.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  MUNGU kisha tusaidia, tumepewa haki ya kuchagua viongozi na chama cha kutuletea maendeleo kila baada ya miaka mitano. Lakini sisi hatutaki kutumia fursa hii. CCM nenda rudi matatizo tunayaona kura hatutaki kupiga hatutaki kushawishi wananchi vijijini kuwa kama miaka 50 ya uhuru mambo yako hivi hakuna kinachoweza kubadilika miaka kumi ijayo. Ni uwongo, ni afadhali kuleta watu tofauti wenye mawazo tofauti ili watuongoze.
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sidhani kwanza kama kuna daktari at most utakuta kuna Rural Medical Aid( RMA ) yeye ndo dokta. Tuwaambie watu wa vijijini kuwa juhudi zao watu wa mjini hatuzithamini hata kidogo, ndo maana hizo ndo hospitali zao. Tukukaa kimya hakutakuwa na mabadiliko hata siku moja.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  hakika yake hii inauma, karne hii bado selikali haioni aibu tu, na tatizo sio kwamba hakuna hela, tatizo ni matumizi mabaya ya pesa, ndo maana wanasema hazitoshi, ni kweli kwamba pesa za selikali hazitoshi kufanya hayo mambo kwasababu zilizopo zina matumizi mengine ya anasa na kujilimbikizia kwa viongozi wetu, zitatoshaje sasa wakati wao hawajajilimbikizia nakununua magari ya kifahari na kula anasa kwa kutaliii nchi za nje na mahela ya kodi zetu? this is too much wajameni. sasa hapo hao wamama wameenda kufanya nini? manake hakuna msaada watakaoupata hapo, utakuta hapo kuna panado tu za kutuliza maumivu na sijui rangi mbili na vidawa vidogo vya kusafisha vidonda sijui, docta naye hapo lazima awe mfalme, ili mtu ahudumiwe vizuri lazima alete kuku/jogoo ale supu....ufisadi kuanzia mkiani hadi kichwani.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  May 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  shida hao wadau ukienda kule Vijijini kuhubiri serikali mbadala kwa faida yao, hawakuelewi kabisa, maana akija Mzee wa CCM akiwaambia kuchagua serikali mbadala mtaleta vita nchini, na wao wanaamini.
  Nakumbuka pia , hawa watu duni n a masikini ndio diraha kubwa ya CCM, inawatumia hawa kupata kura kirahisi, maana wakiwaninilia Tshirt, wakipewa chumvi na mafuta ya kupikia wanakua wamekidhi njaa yao ya siku moja.....kisha wanaamikia kwenye sanduku la kura kuchagua wawakilishi wa Umma.
  mpaka leo najiuliza wale wakazi wa kwenye jimbo la kapt.John Komba, waliwaza nini kumchagua huyo mtu, kuna mtu alinambia sauti yake ya kwaya na maspika makubwa yalimpa ulaji, hayo ndiyo mambo watu wetu wanayoyatafakari katika chaguzi.
  kataaa CCM kwa maendeleo ya Taifa lako.
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2010
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nanii amesema hakuna hela za kuwalipa wafanyakazi maana zinakuja huku!!!!!!!!!
   
 14. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  twaelekea uchaguzi mkuu..yapo ya kuwaza na kuwazua kuona na kuamu iwapo wanastaili tena kuwapa.

  At last huko Ludewa ni good news, kuwa wananchi wameyaona na kuamua. Nguvu ya Wananchi itumike kuondoa madarakani wote wanaoipelea nchi yetu pabaya!!

  "Jimbo la Ludewa Profesa Mwalyosi, ameangushwa na Deo Filikunjombe. Matokeo yanaonyesha Filikunjombe amepata kura 6,000 dhidi ya 4000 za Profesa Mwalyosi."
   
 15. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #15
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Its so sad to see this kind of world still existing in 21st century.Mimi ningeomba wapinzani during this campain wapige picha na kutengeneza movie between our leaders how they enjoy their life,what they eat,what they drive and than make a movie of what they are,eg taking these photos of their hospital and schools,than show them live the dicrepencies between the two walk of life.
   
 16. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  natamani nisiyaone haya.
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Ooh god inasikitisha sana
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Aug 3, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Unamwamini mungu wewe?
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,686
  Likes Received: 21,951
  Trophy Points: 280
  Halafu serikali hiyohiyo inayoshindwa kuwapa maisha bora watu wake inawaachia wageni na baadhi ya viongozi serikalini wanakwiba rasilimali zetu na kuzipeleka nje. Tuwaondoe this October.
   
 20. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We are now playing our last card for the coming five years. jamani tuwe serious safari hii tusikosee tena, ila nashukuru mambo yameanza kuwa safi kwani hivi vizee ving'ang'anizi vinachomolewa taratibu.
   
Loading...