Shibuda ni mbunge wa chama gani?

Shibuda ni mbunge wa chama gani?

Shibuda ni Mbunge wa CCM kupitia Chadema!

Mbunge hawezi kuwa Wa chama, Anakuwa Mbunge wa Jimbo Kupitia Chama Fulani. Sasa Shibuda ni Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia CHADEMA
 
Najua wapo watakao shtushwa na kichwa cha habari na kudhani mm ni kilaza kwa kuuliza swali ambalo lipo wazi. Nimeuliza maana nimeshindwa kumuelewa John Shibuda aliyekuwa kada wa CCM na baada ya kuchakachuliwa na kura za maoni akakimbilia CDM. Kinachonishangaza ni mwenendo wake kama mwanachama na mbunge kwa tiketi ya CDM amekuwa akipingana na sera na kanuni za chama hicho. Tumeshuhudia akikiuka msimamo wa pamoja uliowekwa na chama chake bungeni kwa kutohudhuria kikao kilichopangwa kugomea na kutoka nje wakati Mhe. Kikwete akilihutubia bunge. Kilichonishtua zaidi ni kwamba jana chama chake kilifanya maandamano katika wilaya ya Maswa Mashariki ambako yeye ndie mwakilishi wa jimbo hilo lakini hakushiriki. Tokea kuanza kwa maandamano na mikutano ya kanda ya ziwa JOHN SHIBUDA hajaonekana kwenye mkutano wala maandamano yoyote. Kulikoni hapa?


shibuda ni mwanachama wa CDM.ila inaonekana yupo liberal zaidi ya wenzake.yeye na zito wanafanana
 
Back
Top Bottom