Shibuda ni mbunge wa chama gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda ni mbunge wa chama gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanakwetu, Mar 3, 2011.

 1. mwanakwetu

  mwanakwetu Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Najua wapo watakao shtushwa na kichwa cha habari na kudhani mm ni kilaza kwa kuuliza swali ambalo lipo wazi. Nimeuliza maana nimeshindwa kumuelewa John Shibuda aliyekuwa kada wa CCM na baada ya kuchakachuliwa na kura za maoni akakimbilia CDM. Kinachonishangaza ni mwenendo wake kama mwanachama na mbunge kwa tiketi ya CDM amekuwa akipingana na sera na kanuni za chama hicho. Tumeshuhudia akikiuka msimamo wa pamoja uliowekwa na chama chake bungeni kwa kutohudhuria kikao kilichopangwa kugomea na kutoka nje wakati Mhe. Kikwete akilihutubia bunge. Kilichonishtua zaidi ni kwamba jana chama chake kilifanya maandamano katika wilaya ya Maswa Mashariki ambako yeye ndie mwakilishi wa jimbo hilo lakini hakushiriki. Tokea kuanza kwa maandamano na mikutano ya kanda ya ziwa JOHN SHIBUDA hajaonekana kwenye mkutano wala maandamano yoyote. Kulikoni hapa?
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shibuda ni kiongozi jasiri sana anayefanya mambo yake kwa umakini mkubwa na sio kwa kufata mkumbo . Wengi wa wanachama wa Chadema hivi sasa wanafata mkumbo. Hata jana jioni nilikutana na kijana mmoja Chadema damu nikamuuliza kwanini Chadema wanafanya mikutano na maandamano hivi sasa. hakua na hoja mahsusi ya kunipa mimi zaidi ya kusema wanapinga malipo ya dowans. Nilimuuliza mnapinga kwa maandamano au kwa kwenda mahakamani. Hakuwa na jibu.

  hata hoja ya maisha magumu sioni kama Chadema wakipata maamlaka kisheria kuongoza nchi atakuwa na jipya.

  Hongera sana Shibuda kusoma alama za nyakati , Jipumzikie tuli hapo Upanga.
   
 3. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyo yuko CDM kimwili lakini kiakili yuko CCM! Unajua kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, hata Mheshimiwa mmoja wa zamani alisema "...yaacheni magugu na ngano vikue pamoja...iko siku ya mavuno inakuja mwenye shamba atavuna ngano na kuiweka ghalani, na magugu atayatupa motoni..!"

  Shibuda alikuwa anataka ubunge tu kama alivyosema, sasa hivi anaogopa kujitokeza hadharani mbele ya wananchi (wenye shamba), mwacheni aongeze ruzuku na wabunge wa viti maalumu kwenye chama. Siku ya uchaguzi ujao (mavuno) ndo atakapo tupwa mbali!
   
 4. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  shibuda hana dira ,ni kigeugeu na trouble make.siku zake zinahesabika km na wenzake wengine.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Akiwa CCM basi ana UCUF pia maana hivyo vyama ni chanda na pete
   
 6. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280

  ...watch your quote!!!! hata kama wafuasi wa huyo aliyenena hayo maneno ni wastaarab lakini isiwe sababu ya kuwachokoza!!
   
 7. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #7
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  good!...
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,809
  Likes Received: 2,293
  Trophy Points: 280
  Shibuda asipewe uongozi ndani ya CHADEMA, abakie na ubunge wake na vijembe vyake visivyo na maana huku akishangiliwa na wabunge wa CCM.

  Yeye na hao wenzake wanaojidanganya kwamba siku moja wataweza kuja kuiongoza CHADEMA wafute mawazo hayo, chama kitampa uongozi mtu ambaye hanunuliki na ambaye msimamo wake unaonekana.

  Tena ndugu yangu usiumize kichwa, wenyewe mmoja baada ya mwingine wataondoka bila kufukuzwa.
   
 9. Z

  Zempugwa Member

  #9
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sorry naomba nimtete mh shibuda hata kiduchu japo nahisi anataka kuwa kilaza.ni kwamba mim niko maswa na ni mbunge anayekubalika sana ila hakushiliki maandamano ha ya coz kafiwa na mama yake mkubwa hapa maswa.siku Dr slaa anafanya mkutano mjini maswa pia siku hiyo ndio yalikuwa mazish ya mama yake
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  SHIBUDA NI NJAA KALI ANAITAMANI CCM LAKINI CCM HAIMTAKI,CHADEMA IMEMKARIBISHA LAKINI HAIMUAMINI KWA HIYO AMEBAKI KAMA WALE DADA ZETU WA OHIO

  ccm cdm
   
 11. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mmh! huyo Bwana POPO kabisa, kwa sasa yupo CDM nje ndani!
   
 12. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Kweli huyu jamaa ni bonge la kilaza, na hata huyo CDM damu uliyekutana naye atakuwa ameamua kutokujibu kuepuka kubishana na mpumbavu. Umeamua wanapinga kwa maandamano, halafu unauliza wanapinga kwa maandamano.... Swali la kipumbavu kabisa. Kwa hiyo wewe unaunga mkono RA alipwe hela kwa niaba ya Dowans agawane na mmiliki mwenzie Mkwere? Lakini hata Shibuda aliposema anagombea urais na JK hamkumuelewa pia.
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Hizi ni fikra mfu!!
   
 14. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kweli CHADEMA hamna utu, mtu amefiwa na hamkwenda kuzika wala kumpa mkono wa pole , badala yake mmeamua kuendelea na mikutano. Je angekufa mama yake mkubwa na mbowe au slaa au wale wabunge wetu wa moshi na arusha mngefanya hivyo kweli ? ubaguzi utawamaliza CDM
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Usiniulize kwenye hiyo glass kuna nini!
   
 16. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Labda tusaidie pia kutufahamisha sababu ya Shibuda kutoshiriki hayo maandamano, inawezekana unajua kitu hadi ukapost thread. Na ukiwauliza wana Maswa watakwambia kuwa maandamano yalifurika watu haijapata kutokea. Walipita Malampaka wananchi wakalazimisha DR Slaa awahutubie bila kujali kuwa polisi hawajaarifiwa. Sasa ungeniambia watu hawakwenda mkutanoni kwa kuwa Shibuda hakuwepo ningekuelewa. Kwa taarifa yako 67% ya wabunge wa CCM wamekaa kimaslahi na hawakisaidii chama. afadhali hata ya Shibuda CDM.
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Umejuaje kama hawakuenda???? Kumbuka uongozi siku ya mazishi walikuwa pale Maswa.Huoni kwamba ni lazima walimuhani, ila kwa kuwa media Tanzania zimedhibitiwa dhidi ya CDM huwezi kupata coverage, ila kama angefiwa chiligati wangeenda hadi wamiliki wa vyombo vya habari.Mazingira tuliyonayo ni magumu sana ndiyo maana tunawaasa CDM WATUONDOLEE hili gonjwa CCM KUPITIA NGUVU YA UMMA
   
 18. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nilisha wahi sema kuwa mbunge yeyote wa CDM ambaye anania ya dhati katika kuendeleza taifa(yaani yupo kitaifa zaidi) huwezi kumkuta anashiriki mikutano kama ile. hata watu wanapokusanyika pale huwa wanaenda kuwashangaa jinsi wanavyolalama. Unajua mshindani wa kweli ni anayekubali matokeo. sasa cdm walichemka kwenye uchaguzi sasa wanaona kufanya fujo kwa kuzurula. Kuweni wakubwa. wewe unalalamika kuwa maisha magum ndio maisha magum lakini wewe umefanya juhudi gani? au unakalia kulalamika unataka JK akuletee hadi mdomoni kwako.
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Great Thinkers why tunahangaishwa na propaganda za CCM? Kila siku mara Zitto mara Shibuda mara sijui nani. Ukiangalia wanaonzisha hizo mada ni CCM damu na kuna wana CDM huku wanaingia kichwa kichwa kuchangia kila mada. Kuna watu humu are supposed to be ignored for the sake of the forum.

  Kama Zitto au Shibuka are not fit for our part, let the Nature Select jamani tuache kuyumbishwa! Nchi Inaliwa ninyi mmekaa kujadili nani hawakufika kwenye Maandamano tena watu wanajadili na kutoa Conclusion pasipokuwa na Fact

  Wana CDM we need to have our own way of thinking which is different from CCM, Chama kimejitahidi kuvuta vijana wengi ambao ni Mtaji mkubwa tuahakikishe tunawamaintain hawa Vijana

  Hao akina Shibuda tuwaache, ni Wabunge wetu wa CDM ila kama hawastahili kuwa ndani ya Chama acheni Natura iamue tu
   
 20. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Hapo sidhani km ni swala la kuwa na utu au laa!...Chadema ni taasisi,hivyo lazima kuna taratibu,,huwezi kuahirisha mkutano kwa sababu,mmoja wa wanachama kafiwa mama mdogo.Hata serikalini au taasisi,ukifiwa na mama mdogo hupewi ruhusa ya zaidi ya siku moja ya mazishi ambayo nayo ni kiubinadamu si kisheria. Pia kwa kuwa chadema ni taasisi,basi wenda iliwakilishwa kwenye mazishi na mkutano ukaendelea. Mkubwa mikutano hii ina vibali,ina gharama na mengine.Ukiahirisha tu inakuwa imekula kwako.
   
Loading...