Shibuda kufanya ya Mpendazoe

Shibuda hawezi kupambana na chadema, washikaji wakiweka kambi mambo yanakwenda vizuri. Shibuda ni mzigo, hafai kabisa huyu bwana!
 
ni afadhali jimbo lipotee lakini shibu-mbu afukuzwe kwa gharama yoyote.
 
atufaiiiiii uwiiiiii simttaki na misemo yake ya kinafiki sijui msukuma gani ana mambo ya mipasho kiasi kile
 
Katika kile kilichotegemewa na wataalam wa mambo kesho yule mbunge kipenzi cha wengi John Shibuda atatoa upande wake wa stori kwa yale yanayoendelea katika chama chake. Ametoa msisitizo kwa vijana wamsikilize kwa kuwa anaujumbe maalum kwao na pia uchambuzi wa aina ya vyama vya siasa vilivyopo nchini, kuanzia vile vyenye mlengo wa SACOS, kikanda, familia na kimaslahi binafsi.

source: mtanzania

Watch out:
Viongozi wa CDM waliokutana na Rostam kufanya naye mazungumzo na kuweka makubaliano kaeni chonjo kwani jamaa ana taarifa na ushahidi wa kutosha.
 

Duh ! kazi ipo kumbe CDM wameisha anza mazungumzo na Rostam , kweli hiki ni chama cha mafisadi
 
Hili la Shibuda mbona cha mtoto:

Magamba mawili yaliyobakia yameshindikana KUKOBOKA -- yakitaka kutoka yanatoka na ngozi -- kazi ipo mwaka huu.
 
Sasa huu ni mkorogo kwanza chama cha wachaga, mara hoo chama cha kaskazini mara hoo chama cha familia ya mtei, mara hoo chama cha wakatoriki, mara hoo chama cha wakristo, mara hoo chama cha wamarekani, mara hoo chama cha kihuni malengo yake kuvuruga amani, sasa ETI CHAMA CHA MAFISADI.. DUHH KAZI KWELI KWELI.. Yaleyale ya cuf. mi yangu mimacho na mimasikio..
 
Shibuda anajulikana na tabia zake na kuwa ametumwa na ccm na sishangai na wala sioni kama hii ni habari mpya na suala la Chadema kuwa na mazungumzo na Rostam ni kitu cha kawaida kumtumia mtu mdhaifu ili upande juu steping stone! Na haimaanishi kuwa CDM ni mafisadi anatumika na watu wanachapa mwendo mbele na kujichukulia Jimbo la nyongeza bila jasho
 
Mkuu sio rahisi unavyodhania, na hata kama wakimfukuza kwa kosa gani hasa? hapo ndipo mahakama itakapo amua kama kafanya kosa linastahiki kutimuliwa na kuwaondolea wana maswa mwakilishi wao
Hivi mahakama inaangalia ni kosa gani au inathibitisha kosa kwa sababu linaweza kuwa kosa kwa CCM lisiwe kosa kwa CDM inategemea katiba zao.
 
Tabora na Shinyanga wote si wasukuma? Kuna shida gani msukumu mmoja kuwa campaign manager wa msukuma mwenziwe?

Nasikia harufu ya ukabila hapa. Unapotafuta Candidates kwa sifa ya ukabila ndipo ninapoanza kupata shaka. Yaleyale ya Chadema Chama cha Wachaga. Sasa hivi Chadema kitakuwa Chama cha Wasukuma.

Nadhani John Mrema au Marando anafaa zaidi kuwa Kampeni meneja.
 

Acha ujinga, kipenzi cha wengi...... Unamaanisha nini unaposema wengi? Mbona mnapenda kushabikia upumbavu? Eleweni ujinga wenu ndio mtaji wa wengine.

Usiwakilishe mawazo yetu katika huu ujinga, kama Shibuda ni kipenzi chako kivyako. Ndio yale yale ya JK 2005....kipenzi cha wengi, tumaini lililopotea nk... kumbe hewa. Sasa unatuletea ya Shibuda... halafu ni magazeti yaleyale ... Mtanzania
 
Acha ujinga, kipenzi cha wengi...... Unamaanisha nini unaposema wengi? Mbona mnapenda kushabikia upumbavu? Eleweni ujinga wenu ndio mtaji wa wengine.

Kipenzi cha wengi waliomchagua, hivi huwezi kuchangia hadi utoe maneno mabaya?
 
Kipenzi cha wengi waliomchagua, hivi huwezi kuchangia hadi utoe maneno mabaya?

Kuna neno baya hapo, ama ni mmoja wapo wa wale ninaowataja, Ujinga ni kwa wajinga na upumbavu ni kwa wapumbavu, hatuwezi kubadilisha lugha.

Na ushabiki wa kijinga ndio unaolitafuna taifa hadi leo....Hebu anaglia yanayotokea bungeni sasa.... ni ujinga mtupu, halafu nakatwa kodi kugharamia ujinga huo.
 

Nashindwa kuona ujinga hapo, niliposema kipenzi cha wengi nilimaanisha wapo wanaompenda tena kwa ushahidi, Mbowe na viongozi wa CDM walipoenda shinyanga waliambiwa wazi kwenye mkutano kuwa watu washinyanga wanampenda Shibuda naye Mbowe alisema pia katika chama nao wanampenda. Sio sababu za kutumia maneno mjinga, mpumbavu, mpuuzi kwa mwana jamvi mwenzako eti kwa sababu tu mnatofautiana mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…