Shibuda: CCM ina uchakavu wa fikra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda: CCM ina uchakavu wa fikra

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mbeshere, Jun 8, 2011.

 1. m

  mbeshere Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wetu, Thehabari, Maswa
  MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amesema CCM ina uchakavu wa fikra na anguko la vitendo linalowatafuna viongozi wake hivyo kushindwa kutambua hisia za wananchi.
  [​IMG] Mbunge Shibuda akizungumza bungeni.

  Kwamba viongozi hao wamesahau na kuzitupa siasa za Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa kuwa na sera ya kutesa kwa zamu hali inayowanyima haki wananchi ya kufaidi matunda na rasilimali za nchi yao.
  Shibuda alitoa kauli hiyo Wilayani Maswa wakati akizungumza na wananchi na wazee wa Jimbo la Maswa Magharibi kuhusiana na changamoto zinazoikabili jamii ya Watanzania.
  Alisema viongozi wa CCM wameshindwa kuzibua masikio na kutambua hisia za Watanzania wanahitaji nini ili kuwaletea maendeleo badala yake wanajinadi kujivua gamba kumbe ni funika kombe mwanaharamu apite.
  “CCM inauchakavu wa fikra, ndiyo sababu CHADEMA tunawambia maovu yao ili watambue hisia za wananchi lakini hawataki kuzibua masikio na badala kupongeza wao wanakasirika.Siku zote ukweli unatabia ya kuudhi masikio” alisema Shibuda
  Mbunge wa Jimbo la Mawa Magharibi alibainisha kuwa Watanzania masikini wanateswa na viongozi waliopo madarakani kutokana na sera yao ya kutesa kwa zamu, huku uovu ukifanywa funika kombe mwana haramu apite wao wakidai wanajivua gamba.
  Alisema viongozi wa CCM na serikali yake ni wavivu na wana hila mbay na desturi mbovu na tabia ya ubinafsi na visasi hali ambayo ni hatari kwa mustakabali wa nchi ndiyo maana upizani umekuwa ukisema yaliyo katika ukweli na uwazi na kisasi cha CCM ndiyo kimeifikisha nchi mahali pabaya kuzaa matabaka.
  Alidai kuwa kwa miaka 20 sasa CCM imeshindwa kuandaa viongozi bora baada ya Mwalimu Nyererena katu haiezi kusimama kwa vile imekosa mbegu bora ya uongozi wa kuwatumikia wananchi.
  “Naomba niseme, CCM na dola ni wavivu wanatabia mbovu na chafu zisizojenga. Sheikh akiwa mwovu usikasirikie Msahafu na usichome Biblia kwa sababu ya padri mwovu. Hivyo CCM haiwei kusisima, watu wazima hovyo,” alisema Shibuda na kuhoji tangu lini kanzu jeupe likafuliwa kwa sabuni ya mkaa?
  Kuhuisu vyama vya upinzani alisema CCM ina deni ya kuvipenda kwa sababu vyote vina muenzi Baba wa Taifa na kueleza mzazi hawezi kumkataa mwanaye na masikini anapaswa kupendwa na tajiri.
  Alisema CCM inapaswa kutambua kuwa vyama vidogo vya upinzani vina faida ya maslahi ya Taifa sawa na mgongo wa tembo kumfukuza inzi hivyo vinapaswa kupewa ruzuku.
  “Nina mavuno ya utajiri wa kumbaua tulikotoka. Je, tutajikwaa na kuangukia wapi, nitatoa urithi gani kusaidia Watanzania. Siasa si kugombana wala hila na visa.Bima ya haki itapatikana penye haki sawa katika nchi,” alisema Shibuda.
  Mbunge huyo pia aliwaasa wazee wa jimbo hilo kutambua thamani yao ya kuitwa wazee bila kuona haya kwani baadhi yao wana matende ya kuwaharibia vijana kwa madai kuwa wamelelewa na CCM.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Heko Shibuda wanavibandika vya nta kwenye masikio yao CCM hawasikii wala hawana hata nia ya kuzibua vibandiko,huku wakitujidanganya kwamba eti ni chama Sikivu
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Haswaa hawa CCM fikra zao ni chakavu wakiongozwa na Chiligati, Mukama, na vidingi vingine kama Kingunge
  halafu na huyo dogoo NAPE yaani fikra zake zinachakaa kwa speed ya Rocket..
  Big up shibuda Maghale kwa kuchomoka gambani, piga mziigo ili ujenge imani kwa wananchi waliokuheshimu na kukupa dhamana ya kuwaongoza..
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Well said, ila duh umekuja na speed siyo ya kawaida mkuu - huogopi mashimo na kona kali kali?

  [​IMG] Junior Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]


  Join Date : 8th June 2011
  Posts : 3
  Thanks1Thanked 0 Times in 0 Posts

  Rep Power : 0
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shibuda anajaribu kujitafutia umaarafu tu huyo Mbunge nyie wana CDM mtambue ya kwamba mwaka 2015 atogombea ubunge kwa tiketi ya CCM
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  nyie ndio vijana nape aliesema amewatuma kwenye mitandao ya kijamii! Pole sana. Kuna mwenzio ameandika thread ya Mh. Shibuda anaitwa jeykey. Nawaombea Mungu muwepo tutakapoichukua nchi na kuishi maisha ya haki na neema!
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hapa sitachangia
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi sana Shibuda!fanya kazi yako ya upinzani!!
   
 9. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  "Kuna vijana tumewatuma kwenye mitandao ya kijamii....."
  by Nepi Mnauaye
   
 10. V

  Vonix JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Makupa hilo nalo neno!!!!!be very carefull before supporting Shibuda.kwa mtazamo wangu huyu mtu namwona kama ana sura mbili,kwenye kusapoti maazimio ya chama iwe ni kule bungeni au kwenye maandamano mikoani picha huwa zinatumwa humu jf lakini yeye huwa haonekani,cdm iwe makini nae.:A S 100:
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Duuuuh Shibuda naona kasoma alama za nyakati, kabadilika.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nimekugongea senksi ya kwanza kabisa
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kugawana ni kujali mkuu,
  Vipi ile mipango yetu ya Saccos
   
 14. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haijalishi ili mradi yuko kwenye mlengo sahihi wa kuhimiza na kuhunga mkono jitihada za mabadiliko ya kifkra kwa Watanzani, tunawahitaji wengi members wa fikra na mitazamo mipya kwa Tanzania ya kesho.

   
 15. g

  gambatoto Senior Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NAPE at work. 2000/= per day.
   
Loading...