SHIBUDA: CCM imejaa wachumia tumbo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SHIBUDA: CCM imejaa wachumia tumbo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Jan 2, 2012.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejaa viongozi ‘wachumia tumbo' ambao hawana muda tena wa kufanya kazi ya kutekeleza ahadi yao ya kuwatumia wananchi.

  Akihutubia wananchi juzi kwenye viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini hapa, Shibuda alisema kuwa CCM inaongozwa na wanyonyaji, hivyo akamtaka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nassoro Rufunga, kuacha tabia ya kutumia madaraka yake kuwatisha wananchi hasa wanaoshabikia vyama vya upinzani.

  Shibuda alisema tabia ya Rufunga ya kuweka mbele suala la ‘ukada' wake wa CCM wakati wa kutimiza wajibu wake ni la hatari, na kumtaka aelekeze fikra zake katika kuwatumikia wananchi wa mkoa wake sambamba na kuwaondolea kero zinazowakabili.

  Alielezea kusikitishwa kwake na taarifa alizopewa na wananchi kwamba pamoja na Rais Jakaya Kikwete, kuwapelekea mkuu mpya wa mkoa badala ya yule aliyestaafu, Brigedia Jenerali Dk. Yohana Balele, lakini mkuu huyo mpya ameonesha dalili za wazi za kukitumikia zaidi CCM badala ya wananchi.

  Shibuda aliongeza kuwa pamoja na kwamba wakuu wa mikoa ni wajumbe katika kamati za siasa za CCM lakini wanapaswa kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao vya siasa na kwamba kinyume chake itakuwa ni uvunjaji wa Katiba ya nchi na viapo walivyoapa.

  Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema mkuu wa mkoa hapaswi kutoa vitisho vya aina yoyote kwa wafuasi wa vyama vya upinzani kwa vile anapaswa kuwatumikia wote kama Watanzania na walipa kodi katika nchi hii.

  "Kwa kweli nimesikitishwa sana na taarifa kwamba mkuu wetu mpya wa mkoa amekuwa akijisifu kuwa yeye ni mmoja wa makada wazuri wa CCM, lakini mimi naamini kufanya hivyo anakosea na kama ni kweli basi anavunja kiapo chake pale alipoapishwa na Rais Jakaya Kikwete.

  "Sidhani kama anaielewa vema CCM, kama ni kweli aliyasema hayo niliyoelezwa ni vizuri basi akaitisha mdahalo kati yake na mimi ili tuweze kukaa na kuizungumzia CCM kwa undani kuliko anavyofanya hivi sasa, haielewi CCM kama mimi ninavyoielewa," alisema kuongeza:

  "Leo hii CCM halisi haipo bali imebaki CCM ya wachumia matumbo, si kwa ajili ya kuwatumika Watanzania. Aandae mdahalo awakusanye na makada wengine wote kuanzia makatibu kata, makatibu wa wilaya na kamati nzima ya siasa waje tuelezane, tuwape nafasi wananchi waweze kuelewa ni yupi kati yangu na yeye anayeielewa vema CCM," alijigamba.

  Mbunge huyo alisema kuwa muda wa Watanzania kutishwa hivi sasa haupo, bali kinachotakiwa ni utekelezaji wa ahadi walizoahidiwa wakati wa kampeni za uchaguzi si vinginevyo.


   
 2. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA), amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kimejaa viongozi ‘wachumia tumbo’ ambao hawana muda tena wa kufanya kazi ya kutekeleza ahadi yao ya kuwatumia wananchi.
  Akihutubia wananchi juzi kwenye viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini hapa, Shibuda alisema kuwa CCM inaongozwa na wanyonyaji, hivyo akamtaka Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nassoro Rufunga, kuacha tabia ya kutumia madaraka yake kuwatisha wananchi hasa wanaoshabikia vyama vya upinzani.
  Shibuda alisema tabia ya Rufunga ya kuweka mbele suala la ‘ukada’ wake wa CCM wakati wa kutimiza wajibu wake ni la hatari, na kumtaka aelekeze fikra zake katika kuwatumikia wananchi wa mkoa wake sambamba na kuwaondolea kero zinazowakabili.
  Alielezea kusikitishwa kwake na taarifa alizopewa na wananchi kwamba pamoja na Rais Jakaya Kikwete, kuwapelekea mkuu mpya wa mkoa badala ya yule aliyestaafu, Brigedia Jenerali Dk. Yohana Balele, lakini mkuu huyo mpya ameonesha dalili za wazi za kukitumikia zaidi CCM badala ya wananchi.
  Shibuda aliongeza kuwa pamoja na kwamba wakuu wa mikoa ni wajumbe katika kamati za siasa za CCM lakini wanapaswa kuwajibika moja kwa moja kwa wananchi bila kuwabagua kwa itikadi za vyama vyao vya siasa na kwamba kinyume chake itakuwa ni uvunjaji wa Katiba ya nchi na viapo walivyoapa.
  Kutokana na hali hiyo, Shibuda alisema mkuu wa mkoa hapaswi kutoa vitisho vya aina yoyote kwa wafuasi wa vyama vya upinzani kwa vile anapaswa kuwatumikia wote kama Watanzania na walipa kodi katika nchi hii.
  “Kwa kweli nimesikitishwa sana na taarifa kwamba mkuu wetu mpya wa mkoa amekuwa akijisifu kuwa yeye ni mmoja wa makada wazuri wa CCM, lakini mimi naamini kufanya hivyo anakosea na kama ni kweli basi anavunja kiapo chake pale alipoapishwa na Rais Jakaya Kikwete.
  “Sidhani kama anaielewa vema CCM, kama ni kweli aliyasema hayo niliyoelezwa ni vizuri basi akaitisha mdahalo kati yake na mimi ili tuweze kukaa na kuizungumzia CCM kwa undani kuliko anavyofanya hivi sasa, haielewi CCM kama mimi ninavyoielewa,” alisema kuongeza:
  “Leo hii CCM halisi haipo bali imebaki CCM ya wachumia matumbo, si kwa ajili ya kuwatumika Watanzania. Aandae mdahalo awakusanye na makada wengine wote kuanzia makatibu kata, makatibu wa wilaya na kamati nzima ya siasa waje tuelezane, tuwape nafasi wananchi waweze kuelewa ni yupi kati yangu na yeye anayeielewa vema CCM,” alijigamba.
  Mbunge huyo alisema kuwa muda wa Watanzania kutishwa hivi sasa haupo, bali kinachotakiwa ni utekelezaji wa ahadi walizoahidiwa wakati wa kampeni za uchaguzi si vinginevyo.

  Source: gazeti la Tanzania Daima, 02/01/2012

  HONGERA SHIBUDA KWA KUWEKA MAMBO HADHARANI
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana hata huwa simwelewi, anaamka au analala?
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  SHIBUDA alihamia CHADEMA baada ya kumwagwa na CCM aliyokuwa akihubiri siku zote kuwa anaipenda na hata kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Hakuna asiyejua kwamba alipokosa kuteuliwa kuwa mgombea Ubunge kwa CCM ndipo akaona tumbo lake litakosa chochote kitu na akaamua kwenda CHADEMA... Yeye ndiye mchumia tumbo huyu.
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  sijui lolote..! labda..
   
 6. t

  tweve JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 696
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Shibuda huku chadema upo uhamishoni muda ukifika utarudishwa kwenu ccm.hata hivyo hongera umeongea points kwa mara ya kwanza
   
 7. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Popo,siyo popo!kinyonga,siyo kinyonga,yaani simwelewi kabisa!hivi Shibuda ni mpinzani?
   
 8. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  pamoja na kutoeleweka kwake mara nyingi,ila kwa hili kasema real! yuko sahihi kabisa mzee Magale
   
 9. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Shibuda anajua anachokifanya, kumbukeni ni toka akiwa ccm. Leo hii anajipya gani? sijui wanaomshangaa leo. Utakapofika utimilifu wa wakati tutajua.
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kigeugeu!
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kweli mwaka mpya na mambo mapya ya muda
   
 12. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Katika vita mbinu huwa hazifanani, na maisha ni vita (Tafakari) kwani maisha ni lazima yaendelee.
   
 13. K

  Konya JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ni kweli,sijua anasimamia upande gani,,
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,860
  Trophy Points: 280

  [​IMG]
   
 15. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huyu bwana si sisiemu huyu au naota ninachokiona hapa? kahama lini tena toka CCM?
   
 16. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu ni kigeugeu but kwa hili atakuwa kaona mwezi.ameongea ukweli
   
 17. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  walau hapa kaongea kiupinzani upinzani kuliko kauli zake za hapo awali
   
 18. M

  Molemo JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  tapeli wa kisiasa
   
 19. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,467
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Yule kasema kweli lakini kwanini iwe leo?labda mwaka mpya na mambo mapya ,yawezekana kwenye payroll ya CCM wameikatisha.
   
 20. m

  matawi JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii picha nzuri sana inafanana sana na shibuda
   
Loading...