Kwa wasiomjua Shibuda!
Haya aliikandia CCM. Sasa kahamia kuikandia CDM.
1. Namkumbuka kama mtu aliyekuwa karibu sana na Waziri Kiongozi wa Zanzibar, marehemu Dr Omar Ali Juma.
2. Wengine tulidhani ni kiongozi ktk serikali ya ZNZ
3. Akageuka msemaji wa ZNZ
4. Alifanana sana na Raza wakati wa Dr Salmin, Komandoo.
5. Baadaye serikali ya ZNZ na Dr Omar akamstukia. Alichokipata huko anajua mwenyewe, na sikumbuki kama siku hizi anaenda ZNZ.
6. Wakati kuna fununu kuwa JK angegombe Urais, Shibuda alimtukana sana Jk usiku kukiwa na muziki ukumbi wa hotel ya Dodoma. Akiwa amelewa vilivyo, alimrushia makombora ya matusi JK usiku huo huku akimwambia hawezi kuwa Rais.
7. Shibuda ambaye akilewa ni afadhali ukakumbana na nyati alimsumbua JK, huku akimwambia ****** hawezi kuwa Rais..
8. Tuliokuwepo, tuliona Shibuda kapitiliza ingawa ingedaiwa Msukuma na ****** ni watani. Alimfuata Jk kila kona mpaka Jk akakasirika. Ilifikia hatua ya kumshikilia Shibuda asiendelee kumsumbua JK. Ilitia aibu, na watu wengi walisononeka na kuondoka.
9. Haya Shibuda huyohuyo akiwa na ujumbe wa wajumbe wa CCM mkutano Mkuu (Mkoa wa Shinyanga) na kanda ya Ziwa, ilibidi ateremshwe kwenye treni kutokana na fujo kwenye treni. Walikuwa wakienda Dodoma.
10. Baadaye akapambana na Iddi Simba kwenye Uenyekiti wa Wazazi Taifa. Vurugu tupu. Akashindwa, akata rufaa, ukisoma ile rufaa ya Shibuda ambayo hata haikusikilizwa kutokana na maneno yaliyomo mle hutaamini kama jamaa ni mzima.
11. Hayo ni machache tu...........
CDM inyamaze. Wala hajatumwa, bali mwenzenu nahisi ana matatizo hasahasa na pombe! Uhusiano wake na pombe unapaswa kuvunjika