Shibuda awashangaa wanaoogopa urais
Thursday, 09 April 2009 16:30
Na Peter Masangwa
Majira
MBUNGE wa Maswa (CCM), Bw. John Shibuda ameshangazwa na kitendo cha Kamati Kuu ya Mkoa wa Shinyanga kutoa tamko katika Jimbo lake kuwa Rais Jakaya Kikwete ndiye mgombea pekee katika uchaguzi wa mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Bw. Shibuda alisema kitendo hicho kinafanywa na wanasiasa wenye mawazo mgando na maoni yaliyopauka kwani mwana demokrasia hawezi kuthubutu kukandamiza katiba kwa kiasi hicho.
.
Kwi kwi kwi...mbavu zinauma kwa kicheko...

"Inasikitisha sana kwa mtu kama Shibuda niliyeonesha nia ya kugombea urais kuwachanganya watu namna hii na kuanza kujihami kwa kutoa matamko na kufanya maandamano kushinikiza kuwa mgombea abaki kuwa Rais Kikwete," alisema Bw. Shibuda.
Alisema kuwa demokrasia bila utii ni wendawazimu kwani kitendo cha kumtisha kwa jinsi hiyo haitabadili utashi wake wa kugombea urais kwani anaamini kile anachokisimamia.
Bw. Shibuda alisema tamko la CCM linasema milango iko wazi kwa mwanachama mwenye sifa kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho lakini tamko la Mkoa wa Shinyanga linasema mtu akijitokeza atafukuzwa.
"Viongozi ndani ya chama na nje ya chama wanahitaji kufundishwa haki elimu za kiraia ili wajue na kuisemea demokrasia na si kukurupuka kwa kujikosha kwa kiasi hicho," alisisitiza.
Alifafanua kuwa kitendo chake cha kuonesha nia ya kugombea si kuwa Rais Kikwete hafai na wala hajafanya kazi ila anatambua kazi yake, hivyo kugombea kwake ni jambo la kikatiba na kidemokrasia na kuwaonya wanaojaribu kuvunja katiba kwa kiasi hicho.
Je, kama Rais Kikwete angekuwa na huruka kama Bw. Idd Amin wananchi wangekubali kumpa vipindi vyote viwili?" Alihoji Bw. Shibuda.
Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Shinyanga juzi ilitoa tamko kuwa mgombea urais wa chama hicho atakuwa Rais Kikwete kwani ndiyo utamaduni waliojiwekea.
Pia Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam imeunga mkono Rais Kikwete kuwa mgombea pekee kwa tiketi ya chama hicho.
sawa,hawakuwa sahihi mheshmiwa Shibuda...but sio wewe unaefaa kugombea kwa tiketi ya CCM pia bado...neeeeeeeext!
sawa,hawakuwa sahihi mheshmiwa Shibuda...but sio wewe unaefaa kugombea kwa tiketi ya CCM pia bado...neeeeeeeext!
nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..
nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..
haaa haaa haa! unajua niliposoma hii mada mwanzo nilifikiria huyu Shibuda kajitokeza kugombea, kumbe naye anapendekeza JK against Kivuli..,Ndiyo.
Kwa kumbu kumbu zangu nakumbuka Mwinyi alikuwa na upinzani kwa term la pili na mpinzani wake alikuwa kivuri.
semilong,
inaonyesha wazi kuwa unachanganya mchuzi hapa.. Nachouliza mimi ni candidates vipindi vya pili kati ya mwinyi na mkapa kulingana na katiba ya chama ccm.. Wewe unazungumza kwa mapana ya taifa na kutofikira kwamba katiba ya chama ni ile ile toka wakubali maximum ya uongozi ni vipindi viwili..pamoja na kuundwa vyama vingi bado utaratibu ni ule ule ndani ya chama hicho..
nauliza, hivi Mwinyi na Mkapa walikuwa na Upinzani kipindi cha Pili?..
MkamaP,
haaa haaa haa! unajua niliposoma hii mada mwanzo nilifikiria huyu Shibuda kajitokeza kugombea, kumbe naye anapendekeza JK against Kivuli..,
semilong,
inaonyesha wazi kuwa unachanganya mchuzi hapa.. Nachouliza mimi ni candidates vipindi vya pili kati ya mwinyi na mkapa kulingana na katiba ya chama ccm.. Wewe unazungumza kwa mapana ya taifa na kutofikira kwamba katiba ya chama ni ile ile toka wakubali maximum ya uongozi ni vipindi viwili..pamoja na kuundwa vyama vingi bado utaratibu ni ule ule ndani ya chama hicho..
Sasa kama kulikuwepo na mpinzani aasimama pamoja na mapendekezo ya nyerere kwa mwinyi au mkapa nambie.. Ikiwa kila mmoja wao alipitishwa bila kupingwa ktk kipindi cha pili, naomba kuelemishwa kwa nini leo kwa jk iwe issue..
huyo mdogo wako hata kama kazaliwa 1985 ame graduates na kadhalika bado ni mdogo wako, wewe mkubwa kwake utaendelea kuwa mkubwa kwake hadi kaburini kwani ndiyo katiba ya mwenyezi mungu..