Shibuda amtikisa Waziri Profesa Mwandosya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shibuda amtikisa Waziri Profesa Mwandosya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 7, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi
  10/7/2009

  MBUNGE wa Maswa, John Shibuda (CCM), ameendelea kuwa mwiba kwa Baraza la Mawaziri, baada ya kuhoji mantiki ya rasimu ya itifaki ya matumizi ya Mto Zambezi, iliyowasilishwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwondosya kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

  Awali Shibuda aliwahi kuhoji bungeni tafsiri ya uzalendo kwa Baraza la Mawaziri ambalo mwenyekiti wake ni Rais; kutokana na nchi kuingia katika mikataba mingi mikubwa ya kifisadi ambayo hupita kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi.

  Jana, Shibuda aliendeleza msimamo huo baada ya kumbana Mwandosya kwa kuhoji mantiki ya rasimu ya itifaki hiyo kwa nchi alipoiwasilisha kwenye kamati hiyo kujadiliwa, akitaka maelezo ya kina ikiwemo athari na manufaa yake.

  Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya kikao hicho cha kamati, Shibuda ambaye alichelewa kuingia ukumbini, alitaka ufafanuzi na kutishia kuwa ikipita bila ufafanuzi huo, ataipinga bungeni.

  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Musa Azzan Zungu, alipoulizwa kuhusu hilo, kwanza alishtuka na kuhoji kwa kusema: "Ehee... we nani kakwambia hivyo?"

  Zungu alifafanua akisema: "Taarifa ninayoweza kukwambia ni kwamba, kweli waziri aliwasilisha rasimu hiyo na kesho (leo) kikao kinaendelea njoo".

  Awali, Waziri Mwandosya alipoulizwa alitaka mwandishi awasiliane na Zungu ambaye ni Makamu Mwenyekiti kwani yeye alikwishaiwasilisha kwenye kamati.

  Lakini vyanzo hivyo huru, vilifahamisha kuwa Shibuda alichelewa kuingia, alipoingia alipitia rasimu hiyo ya matumizi ya Mto Zambezi inayohusu bonde lake, lakini akataka kile alichokiita mchanganuo wa mambo muhimu.

  Vyanzo hivyo huru viliongeza kwamba, Profesa Mwandosya alisema tayari suala hilo limejadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri; lakini Shibuda, akasisitiza chombo hicho cha maamuzi ni mhimili tofauti na bunge.


  Kwa mujibu wa duru hizo, Shibuda alitaka waziri aandae mchanganuo wa rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuona maeneo makuu ambayo nchi itanufaika.

  "Alichosema ni kwamba, anataka mantiki ya kilichoandikwa, si maandishi akidai kuwa nchi hii ni tajiri wa mikataba mibovu, hivyo alitaka kujua faida na hasara," kilifafanua chanzo hicho.

  Vyanzo hivyo vilidai zaidi kwamba, alitaka kuona uchambuzi huo wa kina ili kuachana na dhana ya kupitisha rasimu za kimataifa kwa sababu mbalimbali, ama kwa urafiki wa viongozi waliopo madarakani.

  "Anachokisema ni kwamba, itifaki za kimataifa hazipaswi kupitishwa kwa sababu, labda ya urafiki wa viongozi waliopo madarakani; kwani kama akija kiongozi mwingine na mikataba hiyo ikawa na utata, inaweza kuwa na athari kwa nchi yetu," kilifafanua chanzo kingine.

  Alipoulizwa kuhusu hilo, Shibuda, alisema: "Mimi sina mamlaka ya kuzungumzia mambo ya ndani ya kamati, muulize Zungu," alisema na kukata simu.

  Mto Zambezi ambao ni wa nne kwa urefu barani Afrika, unatumika kama chanzo kikuu cha kuzalisha umeme katika nchi za kusini mwa Afrika.

  Mpaka sasa mto huo una mabwawa makubwa na miradi midogo ya kuzalisha umeme, ambao unatumika kwa nchi za Zambia, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Afrika Kusini.

  Mabwawa makubwa ya kuzalisha umeme ambayo ni Cabbora lililoko Msumbiji na Kariba lililoko mpakani mwa Zambia na Zimbabwe na miradi midogo ya kuzalisha umeme ipo kwenye mto huo katika maporomoko ya Victoria mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.

  Kumekuwepo mikakati ya umeme unaozalishwa katika mto huo kutaka utumike katika nchi zote za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) ambayo Tanzania ni mwanachama. Mara kadhaa Rais Jakaya Kikwete amezungumzia kuwepo kwa uwezekano wa nchi yetu kupata umeme kutoka Zambia ambao kwa asilimia kubwa unazalishwa katika Mto Zambezi.
   
 2. p

  p53 JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Shibuda ni mzuri sana wa kujenga hoja na wala haogopi.Simjui in person lakini nilivyomuona kwenye picha,tv nikagundua kwamba hana personality ya kushika nyadhifa za juu serikalini.
   
 3. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Pointless kabisa hasa kwa kumjaji mtu kwa sababu ya "haiba"na muonekano wake akiongea na waandishi wa habari na hiki ndicho kilichotuponza watz kwa JK!Moja ya sifa yake kubwa JK mwaka 2005 ilikuwa "anamuonekana mzuri sana wa umbile"na hata akapata kura nyingi kwa sifa hiyo!

  Hao uliowagundua kuwa wana personalities nzuri za kushika nafasi nono serikalini wamefanya nini zaidi ya kuboronga?Bythewa,ni akina nani waliokukosha kwa personality zao nzuri na wakafanya kazi njema?

  Indeed is another valueless point which has been inserted vividly for 2010's political propaganda!

  Shame on them!
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  sitegemei Prof alishindwa kujibu maswali rahisi kama hayo..............ni vitu ambavyo viko wazi kwenye rasimu kama hizo......lazima kulikuwepo na ufafanuzi (ikiwemo faida na hasara) wakati wa uandaaji wa rasimu husika..........
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I don't know about the merit of the specific objection from Shibuda. Lakini alivyo shoot down hii habari ya "tushaongea katika baraza la mawaziri" ni sawa sawa, na tunahitaji wabunge wengine wengi wawe na independency hii.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Achilia uwezo wa urais kwa Shibuda na muonekaniko wake, awe na presidential pasonality ama hapana, kwa kitendo chake tuu, cha kujitokeza hadharani kuwa 2010,atampinga JK ndani ya CCM,ni cha kustahili pongezi kwasababu ana uthubutu, he can dare, he has a darring heart, hata kama kwenye vita hii, Shibuda ataonekana kama dare devil, ujumbe utakuwa umefika kuwa JK is not everything na atalizingatia hilo.
  Kwenye CCM, bado kuna viongozi wazuri, wenye uwezo wa kweli wa uongozi, wanaoweza kulinusuru taifa hili kutoka hapa tulipo na kutupeleka kwenye nchi ya maziwa na asali lakini they can't dare. Hawana uthubutu alionao Shibuda, hivyo kwa hili anahitaji uungwaji mkono.
   
 7. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kazi imeanza sasa
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  p53.....vipi tena Mkuu............
   
 9. w

  wasp JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania hahitaji personality ya mtu kwa maendeleo yake. Tunachohitaji ni IQ na Brain yake katika kuleta na kutetea maendeleo ya watanzania wote. Ufafanuzi alioutaka Mh. Shibuda kuhusu huo mkataba wa bonde la Zambesi ni mzuri kabisa. Yaani Tanzania itafaidika vipi na huo mkataba? Kama hakuna faida basi let us throw it overboard. Kama hawataki kumpa cheo kwenye serikalini ya chama chake basi hizo ni chuki zao binafsi. Hongera Mh. Shibuda kwa kutetea maslahi ya taifa letu. Tanzania kwanza hayo mengine yatafuata baadae.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ni gia tu za kuonyesha upo makini lakini Shibuda hana lolote hapo zaidi ya unafiki tu
   
 11. E

  Engineer JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Posho ya kikao kingine imeshatengenezwa hapo, Wajinga ndio waliwao!
   
Loading...